Waendeshaji wa Mdaharo wa kujadili swala la Katiba mpya ya Tanzania kwa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA),toka kushoto ni Prof. Issa Shivji,Dr. Kitila Mkumbo pamona ja Ndg. Jenerali Ulimwengu wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa mdaharo huo mchana huu katika ukumbi wa Nkurumah,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Ndg. Jenerali Ulimwengu akizungumza katika mdaharo huo ambao ulikuwa na changamoto nyingi kutokana na mada zilizokuwa zikijadiliwa.
Prof. Issa Shivji azungumza katika Mdaharo huo huku akinukuu baadhi ya maneno yaliyokuwa yakitamkwa na Hayati Mwl. Nyerere kuhusiana na swala la Katiba Mpya.Mdaharo huu umemalizika hivi punde katika ukumbi wa Nkurumah ulipo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mchana huu.
Mmoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Mzee Ibrahim Kaduma akichangia mada zilizokuwa zikutolewa na baadhi ya wajumbe waliohudhulia Mdaharo huo kuhisia na swala la kupatikana kwa Katiba mpya ya nchi yetu.Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake nchini (TAMWA),Mama Ananilea Nkya akichangia mada katika Kongamano hilo.
Mmoja wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada.
Baadhi ya Wanataaluma na wanasiasa wakongwe wakifuatilia Mdaharo huo.
Kila mmoja alikuwa akitaka kuchangia jambo katika Mdaharo huo uliomalizika hivi punde katika ukumbi wa Nkurumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Ukumbi ukiwa umefurika kusikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na wajumbe mbali mbali katika mdaharo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Sorry, ni mdaharo au mdahalo?

    ReplyDelete
  2. Hawa wote waliokaa mbele wote ni CHADEMA,haki itapatikana kweli?

    ReplyDelete
  3. lazima suala la Muungano lifumbuliwe kwa kupigwa kura ya maoni. tuamue kama tunataka muungano, au tuwe majirani tu kama nchi nyingine za Afrika Mashariki.

    ReplyDelete
  4. "Hawa wote waliokaa mbele wote ni CHADEMA,haki itapatikana kweli?"
    Jamani wabongo tutoke ndani ya box. Suala la katiba sio ushindani kati ya CCM vs CHADEMA au vs. CUF. Ni suala la wantanzania wote. Kwa hiyo tusijali nani anatoa maoni yake, bali tuyasikilize na kuyachuja ili hatimaye yale yote yatakayotolewa na waCCM, waCDM, waCUF, waNCCR, nk. na yakaonekana yanfaa basi ndio tuyazingatie. ukianza ku-label kila kitu kichama, hatufiki mbali. Of course, wachache (walalaheri) wataendelea kupata lion's share ya 'keki ya taifa' (kwa njia za kifisadi), na walio wengi (walalahoi) wataendelea kunyanyasika bila kujali ni waCCM au ni waCHADEMA!!!

    ReplyDelete
  5. Tunaomba kujua kilichojiri kwa kirefu katika mdahalo huo. Watu wana jazba utafikiri wanataka kuuwa mtu? Na je mapendekezo yao yanakwenda popote au ndiyo hiyo kwamba angalua wahusika wamesikia hoja zetu. Angalie tunahitaji kumwomba Mungu atujalie hekima katika maamuzi

    ReplyDelete
  6. We michuzi wapostie hao wabeba maboksi, wawasikie Watanzania wenzao walivyoamka nakutetea haki zao. Mdahalo ulikuwa umeenda shule, Big up ITV kwkuturushia live hapa Bongo, TBC mpo?

    ReplyDelete
  7. CHADEMA walisusa au walikuwepo,sio haoakina Mkumbo?, Chadema wenyewe!

    ReplyDelete
  8. Michuzi!

    Heshima yako mweshimiwa sana.

    Jitahidi kufanikisha swala la video ya mdhahalo huo tuweze kuelewa yaliyojiri.

    Kama unaweza kufikisha ombi hilo kwa waendesha mdahalo kuweka kwenye youtube n.k ili iwe rahisi kupitia midahalo yote.

    Kingine waendesha mdahalo huo wasiishie mijini na vyuoni tu. ni vizuri pia wakawafikishia nafasi hiyo mashambani, kwani huko nako kuna wapenda maendeleo wengi, tusiwasahau ni vzr kujua upeo wao

    ReplyDelete
  9. KATIBA YA NCHI NI KITI HAI KINACHOKUWA KUTOKANA NA MATAKWA YA NCHI, KADIRI NCHI INAVYOENDELEA NA MAHITAJI MENGINE KUJITOKESA, HIVYO, KATIBA LAZIMA IFANYIWE MAREKEBISHO, SIYO KUFUTWA NA KUTUNGWA MPYA. NATEGEMEA HILO LILIJADILIWA, MAANA HATA HATUJUI WALIZUNGUMZA NINI.

    ReplyDelete
  10. Lakini katiba ni ya nchi nzima sio wasomi tu...kura za maoni ni muhimu na kila raia aruhusiwe ....kuna mengi tu ambayo watu hata kama hawana elimu lakini watakuonyesha pale katiba ilivyokua so outdated...tembeza na midahao vijueni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...