Assalaam a'laykum,

Salama Trust inafuraha kuwatangazia kuanzishwa kwa jumuiya ya Tawhiyd Muslims Organisation ambayo makao makuu yake yapo Northampton.

Nia na lengo la jumuiya ya Tawhiyd ni ile ile ya kufuata na kuendeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu (S.W.) na kufuata yale aliyoamrishwa Mtume wetu Muhammad (S.A.W.) kwa kufuata Sunna na Sharia za Kiislam.

Jumuiya ya Tawhiyd imeanza kutoa huduma za Maziko kwa Waislam wa UK na hivi sasa kwa wale ambao wameshasikia faida (benefits) zinazopatikana katika kujiunga na Mfuko wa Maziko wa Tawhiyd, tayari wameshajiunga na mfuko huo katika mikoa miwili mpaka mitatu ya UK ikiwemo London; na Jumuiya ya Tawhiyd inataraji kuwa na matawi mbalimbali katika miji ya UK kwa kutoa huduma za Maziko na kuwa kama Jumuiya mama ya Mfuko wa Maziko UK.

Tawhiyd yenyewe, tayari imeshajizatiti katika kutekeleza suala zima la Maziko, lakini itaweza kufikia malengo yake kikamilifu kwa kushirikiana na Jumuiya mbalimbali za Kiislam ambazo zipo UK kwa kuwapa mafunzo kamili ya kukafini maiti kwa njia za Kiislam na mafunzo mengineyo muhimu kuhusu Maziko iwapo jumuiya hiyo itahitaji.

Kuna jumuiya ambazo tayari zinazo mfuko wa maziko na baadhi ya jumuiya hizo zipo katika meza ya mkutano na Jumuiya ya Tawhiyd katika makubaliano vipi wataweza kufanya kazi pamoja ili mfuko uwe mkubwa si kwasababu nyingine ila kwa ajili ya kupatikana faida (benefits) nyingi kwa kiwango kidogo kwa manufaa ya jamii nzima na hususan pale mmoja wetu anapofikiwa na msiba.

Kama upo UK katika kijiji au mji ambao hakuna Waislam wengi au hakuna jumuiya inayotoa huduma za Maziko, tunakuomba wasiliana na Tawhiyd ili wachache mliopo katika mji huo mpate kujiunga iwapo mtaridhia. Jumuiya ya Tawhiyd itatoa mafunzo ya kukafini maiti iwapo mafunzo hayo yatatakikana, na si lazima uwe ni Jumuiya. Ama ikiwa ni Jumuiya, wasiliana na jumuiya ya Tawhiyd ili mpate kujua undani wake na vipi mtaweza kuwa pamoja katika jambo hili la Mfuko wa Maziko UK.

Kwa kumalizia, na kwa nia njema kabisa, ningependa kutoa rai kwa wale ambao wapo nje ya UK na nje ya Tanzania, wachukue mfano kama huu kwa kuanzisha Mfuko Wa Maziko na kamati maalum ili tunapofikwa na msiba kuwe na wepesi wa kushughulikia mwili wa maiti baada ya kututangulia mbele ya haki.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jumuiya ya Tawhiyd na njia ya kujiunga,bonyeza hapa au piga simu

07735075803 Abdullah (UK),

au

07985517163 Saleh Ali (UK),

au

07886535282 Saleh Jaber (UK).

Kwa niaba ya Tawhiyd,

Saleh Jaber

Mdhamini Salama Trust

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. sasa WEWE USITUZINGUE WE UNADAI ETI HII HOUSE NI GOOD INVESTMENT ASA MBONA UNAIPIGA BEI? ACHA MIKWALA YA KICHAA CHA DOGI

    ReplyDelete
  2. waswahili husemaga chema chajiuza kibaya chajitembeza

    ReplyDelete
  3. Bro nyumba imetulia ila mbona data za ukweli hukuweka eg
    1. ina hati?>
    2. kuna master?
    3. vyumba vina ukubwa gani?
    4. why unaiuza mbona inaonekana mpya au kuna majini?
    5.ina maana mi naingia tu ndani ya nyumba kisha benki wanakulipa wewe kisha wananikata mimi kila mwezi?
    6. inauzwa kiasi gani? kutotaja bei kwako kunatutisha

    ReplyDelete
  4. wewe mzee hivi huku kigamboni si wanabomoa? sasa unataka kuliza watu tu hiyo sio roho nzuri mzee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...