Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifunguwa kongamano la siku moja Juu ya kuzungumzia Masuala ya Amani Duniani katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Blue Pearl Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es salaam. Kongamano hilo lilihudhuriwa na Viongozi wa Madhehebu mbalimbali ya Kidini na Baadhi ya Viongozi wa Kitaifa, limeandaliwa na Jumuiya ya Hiyari ya Lions Club.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe. K. V. Bhagirath kushoto na Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Hiyari ya Lions Club, wakiwa katika mshikamano kwenye maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yaliyoadhimishwa leo katika Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti Mtoto Areez Shakil (8) mwanafunzi wa Darasa la 3 katika Shule ya Layot jijini Dar es salaam kwa ushiriki wake Bora kwenye Maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yaliyoadhimishwa leo katika Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal, akiangalia vitabu kwenye maonesho ya Maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Hiyari ya Lions Club katika ukumbi wa Blue Pearl Hoteli ya Ubungo Plaza jijini Dar es salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya Hiyari ya Lions Club baada ya kufunguwa Kongamano la siku moja juu ya kuzungumzia masula ya Amani Duniani katika maadhimisho ya siku ya Amani Duniani iliyoadhimishwa leo katika Hoteli ya Ubungo Plaza Dar es salaam.Picha na Amour Nassor - VPO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...