Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Serengeti Breweries SBL Bw.Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzi za Diageo Africa Business Reporting 2011,uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski mapema leo asubuhi jijini Dar,kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano SBL Bi. Teddy Mapunda.

Bw. Richard Wells amesema kuwa tuzo hizo zitajulikana kwa jina la Diaego Africa Business Reporting Awards 2011, ambazo zitafanyika nchini Uingereza katika jiji la London Juni 30- 2011. Amesema waadishi wa habari za biashara wa tanzania ni nafasi yao kujitokeza katika tuzo hizo ili nao waweze kushindania tuzo hiyo na wanaweza kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki kwa njia ya mtandao kupitia www.diaegoafricabusinessreportingawards.com na mwisho wa kujiandikisha ni Machi 2011 mwaka huu. Diaego ni kampuni kubwa duniani inayomiliki viwanda vya bia na ndiyo inayoendesha mashindano hayo ya Tuzo za Diaego Africa Business Reporting Awards, ilianzisha shindano hili mwaka 2004 na jumla ya washiriki 700 kutoka nchi zaidi ya 25 katika Africa wameshashiriki katika tuzo hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...