Kiongozi, mtunzi na mwimbaji wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yusuf, ambaye amevumishwa wikiendi yote hii kwamba katangulia mbele ya haki, yu hai na yuko kwao Unguja anakouguza kidonda cha gotini kufuatia operesheni ndogo aliyofanyiwa mwishoni mwa wiki iliyopita huko Kibaha.
Kwa mujibu wa dada yake, Khadija Yusuf, na mkewe, Leila, Mzee Yusuf amepewa 'ED' ya takriban mwezi mmoja na daktari wake, hivyo katika kupunguza usumbufu wa kutembelewa ama kupigiwa simu na ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzie, ameamua kwenda Unguja kupumzika.
"Mama alikuwa na wasiwasi sana aliposikia Mzee Yusuf amelazwa baada ya operesheni na akataka kmuja Dar lakini Mzee alimzuia na kumwambia ataenda yeye huko Unguja baada ya kuruhisiwa.
"Mzee Yusuf ni buheri wa afya na ukiondoa kidonda cha operesheni ya goti hajambo na wala homa hana. Wanaomzushia kifo na wakome kwani si uzuri", Khadija Yusuf amesikika jioni hii akiiambia Clouds FM katika kipindi cha kila Jumapili cha Taarabu.
Bi Khadija kasema Mzee Yusuf anauguzwa na mama yao na hivi sasa hata simu kazima kutokana na usumbufu wa kila mtu kutaka kujua hali yake. Inasemekana ataanza kazi baada ya mwezi mmoja ambapo goti lake, lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu baada ya kuumia kwenye mazoezi ya soka, linatagemewa kupona na atakuwa anatembea kama kawaida.
Hakuna ajuaye chanzo cha uvumi huo ambao umeenea kila mahali kiasi hata simu za Globu ya Jamii zime-jam jioni hii kwa wingi wa wapigaji wakitaka kujua ukweli wa mambo.
Tumepokea simu toka Mombasa, Marekani, Uingereza na hata Australia ambako wadau wamepata habari hizo zenye utata.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...