Kiongozi wa African Stars band 'Twanga Pepeta' Lwiza Mbuttu akimtambulisha Venance, mwimbaji mpya kutoka Bwagamoyo Sound, wakati wa shoo ya bendi hiyo ya kila Jumapili pale Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar leo.
Lwiza akimtambulisha mwimbaji mwingine mpya wa Twanga Pepeta, Haji Ramadhani, ambaye aliwakilisha mkoa wa Mwanza katika Bongo Star Search mwaka huu.

Bendi ya Africans Stars almaarufu kama Twanga Pepeta leo imetambulisha rasmi waimbaji wapya wawili ambao kwa mujibu wa kiongozi wa bendi Lwiza Mbuttu wameletwa 'kuziba 'mashimo' mawili yaliyokuwa yanapiga mwayo kwa muda kundini mwao.

Mwimbaji Venance, ambaye ametoka bendi ya Bwagamoyo Sound inayoongozwa na Prince Muumini Mwinjuma, pamoja na Haji Ramadhani aliyekuwemo katika kinyang'anyiro cha Bongo Star Search 2010 wameanza kazi rasmi Twanga Pepeta na kama kushangiliwa na kutuzwa na mashabiki wakati wa onesho la leo pale Leaders Club jijini Dar kunamaanisha lolote, basi mashimo aliyoyasema Lwiza Mbuttu yatakuwa yamezibikwa kabisa.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Da'Asha Baraka ameiambia Globu ya Jamii jioni hii kwamba Haji na Venance wamekwenda kuziba mapengo ya Kalala Junior na Khalid Chokoraa ambao wamejikita kwenye ujasiriamali na bendi yao ya 'Mapacha Watatu' wakishirikiana na Jose Mara wa FM Academia, ambao pamoja na kuwa na maonesho kila Jumanne pale Coco Beach jijini Dar pia tayari wameshatoa albamu yao ya kwanza na wanaendelea na bendi yao vyema.

"Ni kama nyie kwenye habari kama mwandishi akionekana anaelemea kufanyia kazi chombo kingine inabidi umuache aende na kutafuta mbadal wake chap chap", alisema Da'Asha, kuthibitisha rasmi talaka ya Twanga Pepeta na waimbaji hao wawili machachari.

Walipokuwa wakitambulishwa, Haji na Venance wameonesha uwezo wa hali ya juu katika kuimba mistari na sauti za Kalala Junior na Khalid Chokoraa utadhani ndio wenyewe. Maseneta wa Twanga pepeta, Mudi Pizzaro na Papa Freditto na wengineo wote walitoa alama ya dole gumba na kusema vijana hao wanafaa, na kwamba Twanga iendelee Kupepeta bila wasi...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. acha kupotosha watu na habari za starehe tu turushie habari za kongamano la katiba?

    ReplyDelete
  2. Inaonyesha kuwa ankal una fungu lako huko Twanga,maana kila kukicha ni habari za Twanga pepeta ktk blog yetu hii ya jamii,jitahidi kutuletea na habari za kisiasa na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi yetu na siyo kila siku twanga pepeta !!nchi yetu itakuja kuuzwa au kupinduliwa bila wenyewe kujua,kwa sababu ya kuwa "bussy"na mambo ya anasa na starehe,wakati tunaongoa kwa umaskini duniani.ni ushauri wa bure,na ninaomba usiiminye hii message yangu.mdau
    London

    ReplyDelete
  3. nenda dodoma bungeni ukajadili hiyo katiba yako we hapo juu,na pia jitahd KUFUNGUA website za hyo katiba na co huku!katiba iliyopo tu huijui lkn unataka mpya a hata hujui unataka nn

    ReplyDelete
  4. safi sana huyo anaetaka maendeleo ya siasa ende kwa ccm na chadema na wewe wa katiba hayo ni yenu wenyewe msitushirikishe wengine hatuna habari zenu hizo za katiba unafiki ww hiyo siasa na ww hiyo katiba ss wengine inatusaidia nn?minimtoto wa mkulima tu wakawaida tena wa chini mungu kaniwezesha nimesoma na ninachukua phd sasa nchi za watu tumewachoka na habarizenu za bila mpango za kutakakuipeleka nchi yetu pabaya unafikiri nani atakaekuja nyumbani kwenu kukupamaendeleo kama si kumlilia mungu wako ww mwenyewe?acheni ujinga mijitumizima bado inamawazo ya kijinga nanialiwaambia mapunzi hayaji bilakumwaga dam kama si akili ya bange iliyochanganywa na mavu ya mbuzi?msikariri hatuendi hivyo msilazimishe wenzenu wanawaponza kwa ujingawenu watu wanakufa bure kwa upumbafu wenu mnatukera anko hayupo hapo kwa ajili ya habari mnazotaka nyie anzisha ya kwako midomo tu yakusema mnayo uwezo hamna mlimsaidia kutengeneza hii blog kamasijuhudi zake binafsi na maarifa aliojaliwa na mungu wake?msimfundishe kazi nendeni zenu huko na mambo yenu ya siasa na katiba hiyo ya kwanza tu hamuijui ya pili ndio mtaijua?hata kama anahisa huko twanga kwani ww nani kakukataza usiwe nayo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...