Jopo la Makocha likiongozwa na mkongwe Mohamed Msomali (shoto) akifuatiwa na Amri Ibrahim wakifuatiklia kutangazwa kwa matokeo ya washindi wa uchaguzi mkuu wa nafasi mbalimbali ya chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro ( MRFA).
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Mpira Mkoa wa Morogoro ( MRFA), wamefanya mabadiriko makubwa katika safu ya uongozi wa juu baada ya kuwatema Katibu Mkuu na Mwenyekiti wake na kuingiza safu mpya.
Katika mkutano huo uliofanyika kwa amani na utulifu mkubwa kwenye ukumbi wa Jeshi kla Kujenga Taifa ( JKT) Nane Nane, Mjini hapa, wajumbe hao walimchangua Mfanyabiashara na mwanamichezo, Pascal Kihanga kuwa mwenye kiti mpya wa MRFA, kwa kura 19 kati ya 14 dhidi ya mpizani wake , Mwenyekiti wa muda mrefu, Athumani Kambi.
Akitangaza matokeo ya washindi katika uchaguzi huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenda michezo wa Mkoa wa Morogoro, Mwenyekiti wa Kamati ua Uchaguzi ya MRFA, Fikiri Juma, alisema kuwa wajumbe 33 walipiga kura na kwamba hapakuwa na kura iliyoharibika kwa nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi huyo, alitaja kuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho imechukuliwa na Athuman Lujuo aliyepata kura 23 dhidi ya mpizani wake Mwamuzi wa siku nyingi, Msafiri Mkeremi aliyeambulia kura 10 .
Nafasi ya Katibu Mkuu iliyokuwa ikishikiliwa na Aristos Nikitas , imetwaliwa na Mchezaji wa zamani wa timu ya Reli ya Morogoro, ambaye pia aliwahi kuwa Katibu Msaidizi wa Chama hicho , Hamis Semka kwa kupata kura 19 dhidi ya 14 ya mtetezi wa kiti hicho,Nikitas.
Wengine waliochanguliwa kwenye uongozi huo utakaokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka minne ni kwa nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi, iliyonyakuliwa na Emmanuel Kimbawala aliyepata kura 18 dhidi ya mpizani wake Ramadhan Kiholele aliyejipatia kura 15.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, wengine kwenye nafasi zao na kura zao katika mabano ni pamoja na Mweka Hazina Mkuu Msaidizi , Peter Mshighati aliyekuwa mgombea pekee na kupigiwa kura za ndiyo 30 na hapana mbili , sambamba na Mweka Hazina Mkuu , Abdallah Mkali aliyepigiwa kura 32 za ndiyo na hapana moja.
Nafasi ya nyingine ni ya mwakilishi mmoja wa vilabu kuwakilisha Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF) ambapo Farid Nahd alifanikiwa kutetea nafasi yake kwa kupata kura 17 dhidi ya 16 za mpizani wake wa karibu Mwandishi wa Habari zikiwemo za michezo , Nickson Mkilaya.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, wengine waliochanguliwa kwa nafasi moja ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ni Hassan Bantu aliyeliwa mgombea pekee na kupigiwa kura 28 za ndiyo na tano za hapana kati ya kura 33 za wajumbe wa Mkutano huo huo Mkuu wa Uchaguzi.
Wengine waliobahatika kuchanguliwa katika nafasi tatu za ujumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Chama hicho kati ya wagombea saba walioomba nafasi hizo ni pamoja na mwandishi wa habari , Yahaya Limangwe , aliyapata kura 19, mchezaji wa zamani wa timu ya Polisi Morogoro , Clement Mbazo aliyenyakua kura 23 na Selvanus Kunambi aliyapata kura 30.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...