Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sumaye mjini Morogoro wakimsaidia mwanafunzi mwenzao baada ya kutelemshwa kutoka katika gari la wagonjwa eneo la Mapokezi Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo. Wanafunzi 16 walipatwa na kitu kilichosemekana ni mapepo kuanzia majira ya saa 3 Asubuhi na kulazimika uongozi wa Shule na Serikali ya Wilaya ya Morogoro kuchukua hatua ya kupeleka gari la wagonjwa shuli kupeleka wanafunzi hospitali ya Mkoa kuweza kupatia tiba na kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Wanafunzi wakipatiwa huduma
Mwanafunzi anapimwa huku akijieleza
Daktari akiwa na wanafunzi waliopatwa na mstuko huo
Mwanafunzi mwingine akifikishwa hospitali
Wauguzi wakimsaidia wanafunzi
Wanafunzi wakimsaidia mwenzao.
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ni macho yangu au mapepo haya yamewaandama wasichana tu.

    ReplyDelete
  2. Ivyo Hizi Pepo mnazoziongelea zinawapata Wanawake tu?????? na kwanini zinawapata wanawake tu???? kifanyiwe uchunguzi lazima kunadawa imepulizwa ya kulaainisha hapo haya mambo ya mapepo jini mie siyaamini mbona wanaume hayajawapata? MZ

    ReplyDelete
  3. Kama wamethibishwa kuwa na mapepo kwanini wanapelekwa hospitali inabidi aitwe mchungaji au mtu mwenye imani na waombewe yatoke!

    ReplyDelete
  4. hivi kaka michuzi haya mapepo? au hali flani ya mazingira ambayo huwakuta hawa wanawake. hebu nisaidieni jamani kwa nini katika hali hii mambo haya yanaowakuta ni wanaweke tu . katika uchunguzi wangu mara zote ninaowaona wakina dada , jamani hapa kuna nini hasa ?swali linakuja kwako kaka pamoja wanadau wenzangu wa libeneke.

    ReplyDelete
  5. midudu tuu inawanyevua hao watoto, hawana lolote. Waongezewe "town live" tatizo litakuwa limekwisha.

    ReplyDelete
  6. Hayo mapepo yanawakumba madem tu? hao wana ishu zao wapewe holiday ya wiki wakirudi wazimaaaa

    ReplyDelete
  7. Sasa hayo mapepo yanawapata wasichana tu?

    ReplyDelete
  8. mi kinachoniuma ni hizi hospital zetu tu ata vitanda vinatushinda, yaani wagonjwa wanalazwa chini kama vile magimbi sasa ndio aseptic gani hiyo waziri wetu wa afya?na hiyo ni hospital kuu ya mkoa inasikitisha kwa kweli, na hapo hapo ukiangalia picha za chini kuhusu kikao cha bunge dodoma unawaona wenyewe wamekaa kwenye viti vizuri vizuri na mauwa wameekewa mezani nini wanachofanya ata hatukioni, kweli sisi masokwe haswa.

    ReplyDelete
  9. Si kweli mapepo yanawapata wasichana tu, ila ni rahisi zaidi wao kuyapata kuliko wanaume. Ukizama kwenye dini na kuelewa nguvu za giza ndipo utaelewa vizuri zaidi. Kweli hapa ilihitajika Padre/Pastor aliye na upaku wa juu aitwe ili akemee haya mapepo.

    Poleni sana, inabidi kusali na kumuomba M'Nyezi Mungu awasaidie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...