

Afisa wa Msalaba Mwekundu,Mama Jane Lweikiza akiwa amembeba mtoto aliekutwa maeneo ya Sitaki Shari,Ukonga mchana huu kutokana na kutojulikana walipo wazazi wake mara baada ya kutokea kwa milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto usiku wa kuamkia leo.Wahanga woote waliokumbwa na mkasa huo wapo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar kutokana na hali ya usalama wa maisha yao pamoja na kupatiwa misaada mbali mbali.

Bw. Salum Madaba wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na Mwalimu Kiondo wa Shule msingi Tandika wakimnywesha maziwa mmoja wa watoto waliopo katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar ambaye haijulikani wazazi wake walipo mpaka hivi sasa.

Watu Msalaba Mwekundu wakishusha Maji ya Kunywa kwa ajili ya Wahanga hao waliopo ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar hivi sasa.Misaada mbali mbali inaendelea kuleta Uwanjani hapa ili kuweza kuwasaidia watu mbali mbali waliopo uwanjani humu kutokana na kukumbwa kwa tukio hilo la milipuko ya mabomu katika makazi yao huko Gongo la Mboto na maeneo ya jirani na hapo.

Wengine wakiwa nje ya uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kupumzika chini ya vivuli vya miti kutokana na kutolala usiku wa kuamkia leo kwa hali ya milipuko ya Mabomu iliyotokea maeneo ya Gongo la Mboto katika maghala ya silaha ndani ya kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Mtoto Gerald Samson akiwa na Mareraha usoni mara baada ya kuumia wakati akijaribu kutaka kujinusuru na milipuko hiyo jana usiku.

Kamanda wa Scout akiwapanga vijana wake katika makundi mbali mbali ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar,mchana huu.

Sehemu ya Matenti ya dharula yaliyowekwa ndani ya uwanja wa Uhuru,jijini Dar.

Hawa ni Watoto ambao waliokotwa huko Gongo la Mboto wakiwa wako peke yako kutokana na wazazi wao kukimbilia sehemu zisizojulikana kutokana na milipuko ya mabomu yaliyokuwa yakilipuka usiku wa kuamkia leo katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) huko Gongo la Mboto.

Sehemu ya Wahanga wa Mabomu ya Gongo la Mboto wakiwa ndani ya uwanja wa Uhuru jijini Dar wakisubiria kujua nini kinaendelea kwa upande wao.

Baadhi ya watoto wakiendelea kuletwa uwanjani hapa kwa ajili ya mapumziko na kama kuna ndugu wa karibu aweze kuwatambua.

Bado watu wanaendelea kuelekea uwanja wa Uhuru hivi sasa.

Kwa Picha Zaidi
BOFYA HAPA
POLENI SANA NDUGU ZETU MLIOPOTEZA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KUTOKANA NA JANGA HILO LA MILIPUKO. TULIO MBALI NA TANZANIA TUMEZIPOKEA KWA HUZUNI KUBWA HABARI HIZI KWAKUWA SIO MARA YA KWANZA, (SOMEONE SLEEPING SOMEWHERE SERIKALINI). CHA KUSIKITISHA NI KWAMBA MPAKA SASA HAKUNA KAULI YA SERIKALI. MMMM...YALE YALE YA EGYPT
ReplyDeleteThis country of ours! I thought when similar accident happened we would have learned a lesson? apparently not! They should move these bombs to the state house and if they go off there maybe something will get done. I look at these people who are now displaced, for once most of them are poor, and I know they are not going to be compensated for their losses. Lets hope, someone or even a cabinet minister gets fired for this and the poor people get compensated fully because they are not responsible for this carelessness.
ReplyDeletekisidumu chama cha mapinduzi.
Inshallah mwenyezimungu atawatizama na kuwaweka kwenye usalama.
ReplyDeletegood job red cross team, please lets keep it up!!, may God bless u...!!!
ReplyDeletepoleni sana ndugu zangu!!
yani napatwa na hasira jinsi nikiona watanzania wezangu wakiteseka haswa hao malaika wakati hajulikani kama wazazi wao ndio wameoteza maisha ama vipi mimi kama mama nalia kweli michuzi hebu tuwekee jinsi gani tuliokuwa nje kama tukitaka kusaidia hao waithirika tufanyaje ? them mbona masaki na mikocheni hakutokei ni sisi tuu ndungu zetu walalaoi ,lakini kila kitu kina mwisho MUNGU NI MWEMA
ReplyDeleteNa hivi ndivyo itakavyokuwa siku ya mwisho, siku ya kiama wazazi watawakimbia watoto wao, yaani kila mtu atajali nafsi yake tu na hapo kuna mafundisho kwa wale wenye kuamini, hebu angalia hao watoto wadogo wazazi wamekimbia kunusuru roho zao bila kukumbuka hao watoto wadogo watanusuriwa na nani. Kisha tazama uwezo wa Mungu ulivyo mkubwa hao watoto hawana majeraha hata kidogo ila hao wazazi waliowakimbia pengine wamevunjika mikono, au miguu au hata kupata majeraha sehemu nyingine. Eeh Mungu tunusuru waja wako!
ReplyDeletepoleni sana
ReplyDeleteaibu kubwa kwa taifa hakuna vita hali ni kama hiyo watu wanawekwa viwanjani je kukitoka vita
ukiangalia picha za majeruhi waliofikishwa hospital amana au muhimbiri utaona wamelala chini sasa hakuna vitanda au vipi?
watu 10 tu vitanda hamna je yakitokea ya wenzetu egpty wagonjwa watapelekwa wapi??
nchi inatia aibu sana
vingunge wa nchi endeleeni kutumia mashangingi na majumba ya kifahari lakini mkae mkijuwa mbele ya mungu kila goti litapigwa
Kaka Michuzi, Asante kwa picha. Kama una utu utalia ukizitizama. Unasema yaani yametokea Tanzania kweli? Hivi serikali ina Disaster Management Plan? Au ndo hiyo tegemeo ni Red Cross itasaidia? Watu walivyoambiwa waende Uwanja wa Taifa, kulikuwa na mpango wa kuhahikisha watapata chakula, maji safi, vyoo vya kutumia? Ninangojea kwa hamu kusikia Rais Kikwete atasemaje kuhusu tukio.
ReplyDeleteBwana Michuzi kwa kweli nawapa pole wote waliopatwa na janga hili.Lakini ni serikali inatakiwa kulaumiwa sana na kitu kingine kiongozi wa majeshi lazima atoe maelezo kamili kwa maana hakuna kilichofwatilia mlipuko kama huu ulipotokea mara ya kwanza.Hii ni aibu sana hamjali maisha ya binadamu hivi vifaa vinatakiwa vihamishwe mbali na makazi ya watu au kama watu walijenga kiholela hawakutakiwa kujenga huko kwa nini serikali haikuwakataza.Kwa hili swala linahitaji kufwatilia kiundani zaidi.Maana mwisho wake watatutekezea ndugu zetu waishio huko kwa ajili ya uzembe unaoendelea.
ReplyDeletepoleni sana wahusika na watanzania wote kwa ujumla. kwakweli ili
ReplyDeletejambo linasikitisha sana. hii ni mara ya pili kutokea milipuko
ya mabomu dar, kwanini serikali isiamishie hayo mabomu sehemu
nyingine ambapo hawaishi watu wengi. nchi nyingi hufanya hivyo. serikali pia inatakiwa ku destroy mabomu yaliyo chakaa.
Watu wengine kila mahali wanaingiza siasa, unalalamika watu wamepelekwa uwanja wa taifa ambako kuko wazi, hivi hujui kuwa wamewekwa eneo lililo wazi kwa usalama wao?
ReplyDeleteSio kila kitu mnajidai mnajua je wakiwekwa uwanja wa ndani wa taifa au ndani ya jengo lolote kisha bomu likafika huko na kutua itakuwaje? Halafu unataka vitanda kwenye ermegency na rescue operation kama hiyo wapi uliona vitanda?
Poleni wote mlioathirika na matatizo ya kufiwa na juumia auu kupotolewa na watoto katika janga hili.
Hivi Dar es Salaam kuna vituo vingapi vya kijeshi, maana du, hii ni hatari sasa, Mbagala, Gongola mboto halafu wapi kinafuatia.... hatujui, ni siri kubwa. Tunamuomba Mungu aiepushe nchi yetu na majanga kama haya.
ReplyDeletepoleni wote mlioathirka na matatizo ya kufiwa na juumia au kuptolewa na watoto katika janga hili. serikali inatakiwa kulaumiwa sana kwa sababu ya uzembe wao.
ReplyDelete