Frank Kutoka Urban Pulse akiwa na tina kutoka Miss Jestina Blog wakila pozi baada ya harambee.

Salam,

Tunapenda kutoa shukrani zetu za Dhati kwa watanzania wote waishio Reading UK walioweza Kuja Vincent kuchangia wahanga wa Gongo la Mboto Tanzania. Kwa muda wa saa moja tumekusanya Jumla ya pesa taslim Pounds £200 Pia tumekusanya Nguo nyingi kutoka kwa watu mbalimbali. Tafadhali Kumbuka bado hujachelewa kwa wakazi wa Reading ambao hawakuweza kufika leo mnaweza kupeleka michango yenu Vincent siku ya mwisho ya kukusanya ni jumanne ijayo tarehe 1.3.11.

Ningependa kutoa shukrani za dhati kutoka URBAN PULSE,MISS JESTINA BLOG,AIL TV, LOCUS IMPEX SHIPPING CO, SHILLA FRISCH, MRS NASIBU NA Utawala wa Vincent Restaurant Reading kwa kusaidia zoezi la leo.

Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania
Asanteni


Mkurugenzi Mtendaji wa LOCUS IMPEX SHIPPING MR B CHISUMO akifungua Harambee.
Mdau akichangia mada.
Wadau wakiendelea kutoa michango yao katika harambee hiyoo.
Mtoto Chanele akimpa Mchango wake Miss Jestina.
wadau wa UK wakifuatilia mpango mzima wa Harambee.
Baada ya kazi, kutoka kushoto JJ, Chisumo, miss Jestina,Gardol na Frank.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Matangazo kibao, kelele nyiiiiingi na mbwembwe zilizopitiliza halafu mnatangaza hapa mmepata pound 200. Acheni hizo, by the way misaada ya kununua biscuits imepigwa marufuku. Kwani hizo hela mlizochanga zinatosha kununua biscuits tu. Halafu ukizingatia gharama za kutuma hizo pound 200 kuja huku Tz ni sh ngapi,mpaka zimewafikia waathirika zitakuwa zimebaki pound 30, si mnajua watz tulivyoo kwa ufisadi ht kwenye hela la janga la namna hii watu wanapiga tu.
    Ni ina nipa picha ya zile kelele za dual citizenship, mara serikali inakosa mambo mengi iruhusu watu kuwa na dual citizenship ili kuweza kuinua pato la taifa,blaah blah nyingi. At the end of the day pound 200? Shame on you.
    Ankal usibanie hii ili ujumbe uwafikie.

    ReplyDelete
  2. hawa si wale kati ya wanaodai dual, Hapa unaona sura ya Ami yoyote? jibu hapana tatizo hii shughuli imefanyika Bar au Pub kwa lugha nyingine kwa hiyo watu wa mtazamo wa upande wa pili si pake hapo hilo ndio tatizo.
    Na bila kusahahu hawa waliochanga hapa ni wabeba boksi kwa hiyo hapo ndio mkono wao unapofika baba.
    Thanks

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa hata namimi naona sio sawa kabisa,sasa kelele zooote zile kweli mnaelewa hali iliyotokea huko,halafu eti mnasubutu kusema mepata £200,hiyo siangeweza kutoa mtu moja?acheni ubahili nyinyi wabeba mabox kutoa ni moyo na wala si utajiri,nibora msingefanya hiyo harambee kuliko kutia aibu kiasi hicho nasema tena shame on u

    ReplyDelete
  4. Siyo, walisahau kutia zero moja, ni £2,000!

    ReplyDelete
  5. Acheni maneno kutoa ni moyo ...Wooote mnaoyapa yapa hamjatoa hata cent...Wametoa walicho nacho wewe fisadi umetoa nini zaidi ya maneno tu....Toa za kwako utangaze tukuone hapa...Si tunaona kila siku makampuni tu ya bongo? mbona sioni hata fisadi mmoja amemega zake kusaidia hii janga...Kama hawapo vile bongo au hawajasikia hii kitu...Hao wapiga box wametoa walicho nacho na wewe je umetoa nini zaidi ya kuona donge....

    ReplyDelete
  6. We Mla vumbi wamekwambia kwa muda wa saa moja walikusanya £200, na wao nakumbuka walikuwepo pale kwa masaa manane hivi.
    Sasa 8x£200 = £1600. Sasa kelele zako za nini?

    ReplyDelete
  7. namsaidia mdau so umeona iyo paundi 1600 ni nyingi sana kama wewe upo huko toa basi 2000 kama wewe kweli una kazi ya maana mmejilundika room 1 huko mamntoni mnajionaaaaaaaa kuvaa na starehe mmeona ni dili sana,eti mla vumbi wewe si ajabu ndio kidampa wa vibibi vizee huko

    ReplyDelete
  8. Msiwalaumu sana wamejitahidi kwa uwezo wao na kwa upande mwingine mwisho wa mwezi umeshafika hao waliochangia wanahitaji kulipia nyumba wanazoishi pamoja na bili nyinginezo,vile vile wamesema michango bado inaendelea mpaka siku ya jumanne(kesho).

    ReplyDelete
  9. MIMI NAWAPINGA WOTE MLIO WAKASHIFU HAWA WATU WALIOKUSANYA PESA,WALITOA MATANGAZO WATANZANIA MWENDE TOA MICHANGO MBONA HAMJAENDA ?MLIDHANI ZINGEFIKA POUND 10000 BILA NYIE KUTOA MICHANGO YENU ,ACHENI USWAHILI NA MAJUNGU YASIO NA MBELE WALA NYUMA,NA KAMA HAMKUWA KWENYE HUO MJI SI WALITOA ACC NUMBER MNAEZA WEKA PESA,JE MLIWEKA?
    HONGERENI KWA KIDOGO MLICHO CHANGIA NYIE WENYE KUTAKA NYINGI NA HAMCHANGII POLENI HABARI NDIO HIYO.
    ASANTE MDAU SWEDEN

    ReplyDelete
  10. Jamani tusitukanane kiasi hicho, eboh!
    Ujue tatizo ni kuwa wengi wangetamani kuchangia ila hawakuchangia,
    kutokana na kuamini kuwa hizo pesa hazitawafikia walengwa, kutokana na tabia iliyokithiri ya ufisadi wetu wa kibongo. Watu wengine hawaogopi hata laana kwa kula pesa za misaada kwa wahitaji.
    Hivyo mtu anaona akitoa ni kama ametupa heri atume kwa jamaa zake ziwasaidie.
    Tusidharau wabeba box jamani wana-struggle sana, na ni wachapa kazi, wewe uliosema wanalundikana room 1 hujui ukisemacho, watu wanabana matumizi kuleta maendeleo nyumbani kwao.
    Tukumbuke pia hata wenzetu wazungu wako makini sana katika matumizi, kwasababu kila senti uipatayo unaitolea jasho, si kama sisi hatujali kwasababu baadhi yetu vibaka, utapeli tapeli tu, ufisadi nk, hivyo hatuoni uchungu wa fedha, utakuta wengine wanatanua kwa pesa za wizi.
    Tuheshimiane jamani, kazi ni kazi, iwe box nk, ndio maana wenzetu wako mbali kimaandeleo, haijalishi unafanya kazi gani, cha muhimu ni unapata pesa na haki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...