JK akiongea baada ya kutembelea kambi ya JWTZ ya Gongo la Mboto mapema jana kujionea madhara ya milipuko ya mabomu ambapo takriban wato 20 wamepoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa na makazi yao kuharibika. Chini ni video ya sehemu ya alichokisema, ambapo amewatoa hofu wananchi kwamba hali sasa ni shwari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mbagala, Gongo la Mboto...Next ni Mlalakuwa, Lugalo na Ngome hapo Upanga...wananchi jiandaeni tena ....

    ReplyDelete
  2. Kwa raisi kusema kwamba hakuna hatari tena na watu wawe watulivu, sijaelewa anammanisha nini? Mwaka 2009 haya mabomu yalipuka mbagala na mwaka huu 2011 yamelipuka gongo la mboto. Haijulikani nini kinaendelea na ninadhani rais wetu kuwa muwazi na kuwaeleza wananchi kinachoendelea au kama kuna mahali pengine wanahisi kutakuwa na milipuko ili wananchi waweze kufanya maamuzi kama wataendelea kukaa huko au kuama kwa ajili ya usalama wao. Hili litakuwa ni jambo la haki na kila mwanachi anastahili kuwa na uhuru wa kujua ni nini kinaendelea. Nimeona picha za watoto kupoteza wazazi wao, familia kupoteza makazi inasikitisha sana na inabidi serikali yetu ianze kuangalia maslahi ya wananchi na kufanya maaumizo kutokana na hilo. Viongozi wetu ni wawakilishi wetu na hizi itakuwa ni muda mzuri kuanza kuangalia jinsi utendeja wa kazi unavyokwenda. Natoa pole kwa watanznia wote waliopo Tanzania na waathirika wote kwa ujumla.

    ReplyDelete
  3. Sasa inamaana kila eneo la Dar.kuna kambi ya Jeshi, Kama mtu alihama Mbagala mwaka juzi na kwenda G.mboto, sasa hivi inabidi ahamie wapi sasa he! Kaazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  4. kwa hali hii ni hatari mwaka 2009 mkuu wa majeshi alikuwa huyu huyu waziri alikuwa huyu huyu sijajua wakuu wa vitengo kama nao ni walewale au la.kwa kuwa viongozi hawa hawa walituakikishia kwamba yaliyotokea mbagala hayatotokea tena lakini yamejirudia nashindwa kuelewa kwanini hawajajihudhulu mpaka sasa je wanangangania nini watu wanapoteza maisha au mpaka ikilipuka mlalakua na kuua vigogo ndio watawajibika je kambi ya gongolamboto ilikuwa na sehemu maalumu ya kuifadhia mabomu au yalikuwa yamewekwa kwy store ya nguo.inasemekana changanyikeni mabomu yanaifadhiwa kwy mabanda ya bati na juzi tu paa limeezuliwa na upepo je nini kinakujakutokea huko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...