Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,Christopher Mutamakaya akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa viwanja vitatu vya netiboli, wavu na kikapu vilivyojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi. Katika shamra shamra za mbio za Kilimanjaro zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro. Mbio hizo zinafanyika leo kwenye uwanja huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja,Naibu Mkuu wa Chuo, Leoe Donge, Mkuu wa Chuo hicho,Profesa Faustine Bee, Mshauri wa wanafunzi wa chuo hicho, Dk. John Haule na Meneja wa TBL Kanda ya Kaskazini Mashariki, Kasiro Msangi.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,Christopher Mutamakaya akijiandaa kurusha mpira golini wakati wa uzinduzi wa uwanja wa kikapu uliojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi. Katika shamrashamra za mbio za Kilimanjaro zinazodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, TBL ilikadhi pia viwanja vya netiboli na wavu kwa uongozi wa chuo hicho leo.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA,Lucy Owenya akijaza fomu jana katika Hoteli ya Keys Mjini Moshi, kushiriki mbio za Km 5 katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro 2011 yanayofanyika leo hapa Moshi.Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inadhamini mashindano hayo.
Mama Mkazi wa Moshi mjini, Esther Lubalaje (47) akijiandikisha jana katika Hoteli ya Keys Mjini Moshi, kushiriki mbio za Km 5 katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro 2011 yanayofanyika leo hapa Moshi.Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inadhamini mashindano hayo.Baadhi ya washiriki wa mbio za Kimataifa za Kilimanjaro 2011, wakijiandikisha leo katika Hoteli ya Keys, mjini Moshi, tayari kushiriki mbio za umbali wa Km 42 leo. Mbio hizo zinadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Watoto wakijiandikisha leo katika Hoteli ya Keys Mjini Moshi, kushiriki mbio za Km 5 katika mashindano ya kimataifa ya Kilimanjaro 2011 yatakayofanyika kesho mjini Moshi.Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inadhamini mashindano hayo.(Picha na Mdau Richard Mwaikenda)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...