Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika eneo linalojengwa nyumba ya makazi ya Spika wa Bunge lililoko eneo la Uzunguni Dodoma leo na kupokelewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Bw. Didas Wambura na Mhandisi Philemon Mzee .Jengo hili linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei 2011.
Spika akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi kutoka kwa Mhandisi Mkuu wa eneo la Ujenzi (site engineer) Bwana John Thomas Mwonekano wa jengo kwa nyuma na ujenzi unaendelea.
Picha na mdau Prosper Minja wa Bunge



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera mama Makinda. hapo bila kupitapita, miaka mitano shaaaa! Ataishia kukaa Sita mwenyewe 2015!

    ReplyDelete
  2. ukisikia nyumba ndio kama hii sio unapangapanga matofali unasema umejenga nyumba,safi sana sasa kazi ya uspika itakuwa dili.

    ReplyDelete
  3. kwa kazi unayoifanya bungeni kwa sasa nashauri na ulinzi uzidishwe. nyumba nzuri kama hii inastaili kwa nafasi yako. kwani Spika aliyepita alikuwa nakaa wapi?! au amekataa kuhama?!

    ReplyDelete
  4. safi kabisa jamaa zangu, kitu ambacho hampendi kukisema ni kwamba limegharimu kiasi gani cha fedha za walipa kodi?

    ReplyDelete
  5. Na hii colonial hang'over tuiache jamani,hadi hivi leo miaka 49 ya uhuru imepita,bado katika nhi yetu kuna sehemu zinaitwa "UZUNGUNI"??tujitahidi kufuta majina haya ya kikoloni na kuweka majina yetu yenye asili ya kiafrika ili
    tuweze kujivuna na kuthamini u afrika wetu.
    J.j.london,Uk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...