Dkt. Islam S. Salim,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (pichani) akizungumza katika Mkutano wa 49 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu (CSD).
Akichangia mjadala kuhusu maendeleo endelevu na uondoaji wa umaskini, Dkt. Islam Salim aliyeongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo, Pamoja na mengine alisisitiza uwekezaji katika miundombinu kama moja ya njia ya kuwasaidia wananchi kuondokana na umaskini hasa wale wa vijijini.
Aidha amesema pamoja na nchi zinazoendelea kujitahidi sana katika kuwaletea maendeleo wananchi wake, pamoja na kutambua hali ngumu ya uchumi inayoendelea dunia kote hivi sasa, amesisitiza haja na umuhimu wa nchi tajiri na zilizoendelea kutimiza ahadi zake za utoaji wa misaada ya kiuchumi kwa nchi maskini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...