Familia ya Mzee Emily (Nembo) inawatangazia kifo cha mtoto wao na ndugu yao mpendwa Aisha Famau (Aida) kilichotokea tarehe 03/02/2011 nyumbani kwa marehemu Leicester (UK).
Mazishi yatafanyika JUMATATU 21/02/2011.
Nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu itaanza Saa tatu asubuhi hadi Saa Nne asubuhi kwenye anwani ifuatayo:
Co-operative Funeral Services,
131 Humberstone Road, Leicester, LE5 3AD
Baada ya hapo utafuata msafara wa kupeleka mwili wa marehemu kanisani, msafara huo utapitia St Mattehws eneo alilokuwa akiishi marehemu.
Ibada ya mazishi itaanza saa nne na nusu asubuhi katika kanisa la
Sacred Heart Church, 25 Mere Road, Leicester, LE5 3HS.
Baada ya ibada mwili wa marehemu utapelekwa kwenye makaburi ya Gilroes Cementry ,
Groby Road Leicester, LE 3 9QG – saa sita mchana kwa mazishi
Baada ya shughuli za mazishi kumalizika kutakuwa na chakula cha mchana kwenye ukumbi wa kanisa ilikofanyikia ibada
Kwa ushirikiano wetu wa dhati tutafanikisha safari hii ya mwisho ya mpendwa wetu.
Usafiri utakuwepo kwa wale wasiokuwa na usafiri
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.
AMINA
Kwa maelezo zaidi wasiliana na :
Asela: 07932841352
Abdullah: 0791957846
Moses: 07405272879
Poleni sana wafiwa. Mwenyezi Mungu awajaze faraja na kuipokea roho ya marehemu mbinguni.
ReplyDeleteMdau
London
I deeply saddened to hear the loss of Dear Sister Aida. May she Rest in Eternal Peace. Amen.
ReplyDeletePoleni sana ndugu zangu jamani, ni machungu mazito yasiyoelezeka kwa kumpoteza ndugu yetu,rafiki yetu na mpendwa wetu Aida,Mungu awatie nguvu na awape faraja ya pekee katika kipindi hiki kigumu.Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi basi tumuombee apumzike kwa amani.Faraja ya pekee iwaendee hasa watoto wake na mume wake.
ReplyDeleteR.I.P Aida pumzika kwa amani mama.
Rafiki wa rafiki zake
London