Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakizungumzia mustakabali wa kambi ya upinzani Bungeni katika kipindi cha asubuhi cha TBC 1 leo katika kufafanua kilichojiri jana wakati wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya ukumbi wa bunge kwa muda kupinga upigaji wa kura kuidhinisha marekebisho ya kanuni kinyume na matakwa yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndugu Mbowe justice (haki) unayoisema ni ya kuwashirikisha wabunge wa vyama vyote ya Upinzani katika kambi ya Upinzani. Na hapo ndipo inapokuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa na UMMA wa Tanzania. Lakini kinyume chake nyie mnatafsiri kinyume chake eti justice (haki) ni kuwaacha chadema tu ndio mmunde kambi ya Upinzani hiyo ndio haki!

    Elewa nchi hii ni ya Watanzania wenye chama na wasiokuwa na Chama. Lakini pia tatizo liko wapi kuwashirikisha wabunge wengine ili kujenga ngome imara zaidi! Kama isingekuwa uroho wa madaraka, yaani nyie ndio mngekuwa wa kwanza kuaomba waje muunde hiyo kambi ya pamoja. Kinyume chake hayo ndio tunayaona sisi wananchi! Hii inanipa taswira kuwa mkombozi wa kweli Tanzania hajazaliwa bado au bado anakuwa! Oh Mungu turehemu sisi wana wako wa TANZANIA

    ReplyDelete
  2. Anonymous wa kwanza uko right kabisa. Lakini kwa mfumo wa siasa tulio nao Tanzania kwa sasa kuna tatizo kubwa. Kama alivyosema Mh. Mbowe inakuwa vigumu kuelewa kama CUF kipo upande wa serikali au upinzani. Kule Z'bar CUF kinaunda serikali ya umoja wa kitaifa. Huku Bara, chama hicho hicho cha CUF kipo upande wa upinzani. Nimesikia kuwa kuna mbunge wa CUF kwenye bunge la Tanzania ambaye pia anashikilia cheo cha uwaziri huko Zanzibar. Sasa hapa kunakuwa na tatizo.

    Michuzi kuna suala kubwa na la msingi hapa. Hata ingekuwa wewe Chadema, how could form kambi ya upinzani na chama ambacho kinaform serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...