habari yako anko michu

nakutaarifu wewe kama mwana habari kuwa kesho asubuhi kuanzia saa 1 wanafunzi wa ifm chuo kizima kutakuwa na mgomo kupinga wanafunzi wenzao kuzuiwa kufanya mitihani kwasababu tu hawakumaliza kulipa ada ya semester ya kwanza

wanafunzi wanapinga uonevu na mfumo mbovu unaofanywa na chuo hiko kwao wakati serikali ilishaweka wazi kuwa hakuna na marufuku kwa wanafunzi wa vyuo vya umma kuzuiwa kufanya mitihani

haya ankal nisiwe mbeya sana fika pale asubuhi angalau kupata vijipicha na taswira kidogo

mwanaharakati wa Globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwa mimi naona wanafunzi waachiwe wafanye mitihani...wasiwape ma-stress wakishafanya mitihani hiyo...kama mtu hajamalizia ada asipatiwe matokeo yake hadi amalizie...ila kumzuia mtu kufanya mtihani si sahihi. Nashangaa sana uongozi(Administration) ya chuo wa Tanzania huwa wanafikiria pafupi sana. Sasa mtu asipofanya mtihani ataufanya lini? hiyo ni kuharibu ratiba ya chuo na pia kuwafanya wanafunzi washindwe kufaulu vizuri. Uongozi wa IFM liangalieni suala hili kwa upya tena.

    ReplyDelete
  2. ahh hiki chuo toka kilivyobadili uongozi kimekuwa vituko tu, huu uongozi uliopo madarakani ni wa kubabaisha na mambo yanapelekwa ili mradi kesho kukuche

    ReplyDelete
  3. Hii TABIA NI MBAYA SANA KWENYE ELIMU YENU HATA WAKIFANYA MTIHANI-----

    WAKIFANYA HUO MTIHANI BASI RESULT ZAO WATAWABANIA VILEVILE SIJUI TUNAENDA WAPI SIE???????? NCHI ROHO MBAYA TUUUUUUU. INGEKUWA MAMBO YA KIJINGA BASI WANGEWARUHUSU ILA ELIMU WATABANIA WATU MAENDELEO..

    ReplyDelete
  4. Mhhh mmezidi sasa. Na watu wataishi vipe msipolipa ada? Msipopewa vyeti on time mnalalamika hakuna huduma nzuri wakati hamtaki kulipa ada...Njooni mpige box huku munakwenda shule na bills mlipe on time. Mnadeka sasa...Huku hujalipa ada wala hiyo semester hutaingia darasani ndugu yangu na wakuongea naye au kumgomea ni machine tu...Unaregister online, pay your tuition fee online na usipomeed dead line madarasa yanaondoka safasi anapewa muingine. Siku ukija register tena ndio hivyo schedule yako inakua haieleweki...Mshukuru hata mliweza kukaa darasani...Lipeni na nyie mnaosupport mnasupport ujinga saa nyingine...Wao watalipaje wafanyakazi wao?...Hata huku states college kibao na bado hawaendi kienyeji enyeji. Ati kwa vile ni public college...You pay brother before you get served..Pay the piper

    ReplyDelete
  5. wewe anonymous wa 01:22:00 sijui umesoma wapi? kwa taarifa yako States colleges hazikuzuii kufanya mtihani kama hujamaliza ada,wanakuachia umalize mitihani yako vizuri tuu lakini hawakupi matokeo mpaka umemaliza ada yote

    ReplyDelete
  6. Uliyetoa maoni hapo juu saa 01:22:00 am unaongea ugoro hata kama uko States. Kumbuka Tanzania siyo States, States unaweza ukafanya kazi na ukalipa ada, na wengine huko States wanaahirisha miaka kibao ili wafanye kazi waje kumalizia ada. Issue hapo ni kwamba si kwamba watu hawajalipa ada..ada imelipwa angalau nusu au robo tatu. Vyuo kibao Ulaya mwanafunzi anaruhusiwa kuingia darasani na pia kufanya mitihani iliyo mbele yake. Baada ya mitihani kama mtu hajamalizia ada hatopewa matokeo hadi awe amemalizia ada yake. Sasa wewe unaongea pumba..nani anadeka hapo? Ninachojua si kila mwanafunzi anakuwa hajamaliza kulipa ada huwa kawaida ni wachache tu and not the majority. Sasa unadhani katika jumuiya kukiwa na mgomo unadhani mtu ataacha kuushirikiana na wenzake? Wewe Mr. States acha kuongea ugoro. Na ubaki States hukohuko waachie Watanzania wanapoangalia namna ya kupata Elimu ambayo watoto wengi wa mafukara wanaikosa. Wewe umeshaenda States...usijidai kuchangia maoni yako ya kipuuzi hapa!..Bado tunasema..IFM wajaribu ku-review taratibu zao, na wawaruhusu wanafunzi kufanya mtihani isipokuwa wasiwapatie matokeo ya semester. I am sure watu wakienda nyumbani baada ya semester lazima warudi na ada ya kulipa. Mgomo oyeee!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...