Baadhi ya wafanyakazi wa Daily News na Habari Leo wakiangalia noti fekiza sh. 10,000/- (ya kulia) ambazo wamegundua kuwapo kwake mara tu baada ya mhasibu kuwashikisha alawansi ya Maulid Day jana na leo na kugundulika kuwa ni feki. Wfanyakazi kimabo wamemrudishia mhasibu noti hizo feki ambaye naye akazirudisha kwenye benki alikochukulia (jina kwapani kwa sasa) ambako kijasho kilimtoka kwani jamaa walimruka kabisa kuwa hawajampa wao ikabidi arudi nazo tu. Maafisa wa benki kuu walikuwa wanahaha kuisaka benki hiyo kwa udi na uvumba bila shaka kuanza uchunguzi lakini kwa sababu za kimaadili jina limehifadhiwa hadi muda muafaka utapofika.

Noti mpya zikinadiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. utamaduni wa kuchakachua ukiingia katika jamii, umeingia!!!

    ReplyDelete
  2. Hahaha kina michuzi wanalipwa Mshahara kwa kuchakachuliwa lol! bongo kunalisilowezekana jamani watu wameipa Pesa Miezi miwili tu duh hii hatari..... huyo Boss tu angekuwa mtu wa kawaida wangemgombania kama mpira wa Kona au Gombania Goli... XtoZ

    ReplyDelete
  3. Hivi finger prints na DNA ya tellers wa Benki hazipo ktk noti hizo na kwa nini jeshi la Polisi na BOT wasitumie forensic investigation kutambua ni nani kwa CCTV films(toka benki),time za kukabidhiana cash(benki/habarileo), DNA tests na finger prints?

    ReplyDelete
  4. hii ni kashfa kubwa sana ila kwa bongo utashangaa watu watapeta tuu..

    ReplyDelete
  5. mambo ya wanaigeria hayo,kazi kwenu wabongo

    ReplyDelete
  6. hivi zilizokuweppo zilikuwa na tatizo gani, kwa nn wasingeboresha hizo hizo?
    Kwa bongo kuchapisha fedha kunasababisha inflation kwa kiasi kikubwa kwani:

    1, feki nazo zinatolewa kwa kiwango kikubwa, huku elimu kwa watumiaji wa fedha hizi hawajapewa elimu ya kutosha.

    2. lazima kunakuwa na uchakachuaji wakati wa destroy au kuchoma hela za zamani zilizotolewa kwenye mzunguko.

    HIVI hebu tujiulizeni kwa nini US dollar haibadiliki badiliki? miaka tuu na vitu vichache ndo inabadilika.

    ReplyDelete
  7. Huyo mhasibu anajua dirisha gani alilochukulia pesa, ni rahisi kumpata mhusika. Noti feki huingia mtaani kwa msaada wa watumishi wachache wabenki wasio waaminifu. Midamu imekwishajulikana ni benki gani ni muhimu BOT na polisi kuikagua hiyo benki kikamilifu.

    Na nyie mambo ya mwaka 47 ya kulipwa pesa kwa keshia kwani hamna akaunti pesa mkachukue kwenye akaunti zenu? Hata kama ni shs 10,000 unapewa mkononi ya nini? Na huyo mhasibu si ni kutaka kuhatarisha maisha yake tu kubeba pesa za watu. Yeye angempa kila mtu payslip kuwa umepata shs 5, 10, 20 basi haya mambo ya kulipana mikononi ndio yanasababisha yote hayo! Badilikeni mnalipwa keshi nyie manamba?

    ReplyDelete
  8. SASA KAKA MICHUZI, MBONA SWALA LA KUCHUJA HALIJAELEZEWA KAMA ALAMA YA USALAMA WA NOTE, AU HUYU DADA HAFAHAM HILO? AU ZINAZOCHUJA NDIO FEKI? WHICH IS WHICH? HATUELEWI JAMANI. HILI NI SWALA NYETI.

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi samahani, mimi nimeulizwa swali ambalo nimeshindwa kulijibu naomba unisaidie, eti mtu akija na Japanese yen,yaani pesa ya Japan, anaweza kuibadilisha huko nyumbani kwa Tanzania shilings? na kama anaweza ni sehemu gani kuna hiyo huduma? Nisaidie Kaka,huyu mgeni anataka kuja huko hivi karibuni.

    ReplyDelete
  10. we anony uneyeulizia kubadilisha hela za kijapani si uende ukaulize benki au madukani. mbona unakuwa mvivu wa kufikiri?

    ReplyDelete
  11. Mdau wa Japanese Yen,

    Ankal Michuzi huwa mara kwa mara anabandika picha za mabango yanayoonesha bei za fedha za kigeni kwenye Bureau de Change.

    Kama hii hapa: http://issamichuzi.blogspot.com/2011/02/bei-ya-madafu-leo.html

    Kwa hiyo utagundua kwa mfano hilo duka aliloweka ankal linabadilisha Japanese Yen.

    Na sio hilo tu, bali maduka mengi yaliyoko Samora Avenue, Posta jirani na Mnara wa Askari na Kariakoo jirani na Barabara ya Msimbazi, Mtaa wa Congo na Soko Kuu huwa yanabadilisha Yen.

    Kwa hiyo njoo nazo tu usiogope.

    Ila nakushauri ukitaka kupata hela nyingi za Tanzania nunua dola za Kimarekani huko huko Japan, halafu ukija Bongo badilisha dola kwa shilingi. Utapata shilingi nyingi zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...