Salaam katika muumba wa mbingu na nchi.

Kwanza kabisa wana jumuia wa shina la CHADEMA jijini Turin -Italia tunapenda kuungana na watanzania wenzetu woote popote pale walipo duniani kujumuika pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kihistoria katika majanga yasababishwayo na siraha za kivita nchi kwetu Tanzania. Ni janga kubwa kwa maana kwamba ndugu zetu wamepoteza maisha, ndugu zetu wamepoteza mali, ndugu zetu wamepoteana na familia zao hususani watoto wadogo.

Ni hudhuni kubwa miongoni mwa wale wakazi wa Gongo la Mboto ambao hali yao ya maisha imeweza kudhoofishwa na tukio hili la aina yake. Watanzania katika hali moja au nyingine hili tukio limetugusa woote kwani sisi ni wamoja, watoto wa nyumba moja Gongo la Mboto ni ndugu zetu. Gongo la Mboto poleni.

Wana tawi la chadema Turin - Italia tunawashukuru viongozi wa serikali yetu tukufu, Taasisi mbali mbali, madhehebu ya dini, watu binafsi na wale wote walioweza kusaidia katika hili tukio kwa kuweza kuufikisha misaada kwa wahanga wa hili tukio bila kuchelewa. Serikali asante kwa kuweza kuhudumia ndugu zetu. Pia tunaomba juhudi zisikome , ziongozeke mara dufu "Aksanteni saana" huu ndio uzalendo, utoto wa mama mmoja ambaye ni "Tanzania".

Ni kilio kwa watazania wote, tungeomba jeshi letu tukufu na vyombo husika kuchukua hatua mahususi kuzuia na kukomesha janga la aina hii lisiwezeze kutokea tena nchini kwetu. Tulinde maisha ya raia wema wa Tanzania. Tunaweza njooni tujumuike kuwalinda watanzania kwani tupo kwa ajiri yao.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki ,wape nguvu ,ustahimilivu na roho ya ujasiri kuyashinda haya yoote wale woote walioathirika na hili janga !

AMENI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kweli mabomu yamefichua mambo, nyie Chadema kila siku mnawakandya CCM na matawi nje ya nchi kumbe na nyie mlikuwa na yenu yamejichimbia hehee ama kweli kilio au msiba hufichua mengi. Cha kushukuru ni kuwa mmekuwa wawazi mmejitokeza kutoa rambi rambi kama wenzenu walivyofanya bado matawi ya CUF nayo yaonyeshe ubinadamu wao.

    Poleni tena kwa mara ya pili watu wote walioathirika na hili janga kwa namna moja au nyingine.

    ReplyDelete
  2. safi sana wakuu na huku parisi tunajipanga kufungua tawi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...