Kwa niaba ya Tanzanian Canadian Association (TCA), chama cha jumuiya ya Watanzania tunaoishi Toronto , Ontario , Canada na vitongoji vyake, tunapenda kuchukua fursa hii kwanza kabisa, kutoa rambirambi zetu kwa familia za wananchi waliopoteza wapendwa wao katika ajali ya mabomu yaliyolipuka katika kambi ya jeshi eneo la Gongo La Mboto, Dar-es- Salaam , Tanzania .

Tunawaombea wote waliopoteza maisha yao Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani; tunawatakia majeruhi waugue pole, wapone haraka ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku. Vilevile, tunawatakia wote waliopotezana na ndugu zao hususan watoto waliopotezana na wazazi wao waweze kupatikana na kukutana tena.

Tumesikitishwa na taarifa za maafa hayo na kuhuzunishwa kuona kwamba ni mara ya pili tukio kama hili linatokea nchini kwetu. Wengi watakumbuka siku si nyingi janga kama hili lilitokea kule Mbagala. Tunapenda kuuomba uongozi wa jeshi uangalie upya namna silaha kali zinavyohifadhiwa; katika utaratibu wa kuhifadhi mabomu, tunapendekeza yafanyike marejeo na marekebisho yatakayozingatia usalama wa raia.

Katika kuhitimisha, tunalisisitizia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), lichukue hatua madhubuti na za haraka katika kuhakikisha majanga yanayoweza kuepukika kama haya hayatokei tena.

Mungu Ibariki Tanzania .

Uongozi – Tanzanian Canadian Association (TCA)

www.tanzcan.blogspot.com

www.tanzcan.org

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Jamani, tuache longo longo, kila mtu anatambua ukubwa na madhara ya milipuko ya mabomu Gongo la mboto. Mali na Maisha vimeteketea, wengi wao bado wanahangaika kutafuta matibabu,malazi,nguo,chakula na counseling... ili kurudi hali ya kawaida ya mwanadamu.

    Mimi, leo hii naelekea kutoa damu kama mchango na nguo chache kama msaada wangu na familia.

    Je, wanajumuiya wa Canada, zaidi ya maneno meeeengi ndani ya e-mail yenu, mnawasaidia nini watanzania walioathirika? tuwe wa kweli, na mvae viatu vya waathirika.

    Muntansir Gulamhussein,Tanzania

    ReplyDelete
  2. Muntasir,
    Msaada wa kweli ni ule usiotangazwa kwa minajili ya kujitafutia sifa.Kama unaenda kutoa damu(na ipimwe kwanza vizuri)au nguo au chakula,fanya hivyo bila kujitangaza tangaza.Kwa mila na desturi zetu,mwenzako anapopatwa na msiba unamfariji kwa kila hali ikiwemo pole kama walivyofanya wenzetu kutoka huko Canada.Ile tu kuonyesha kwamba ingawa wapo mbali,wapo concerned na kinachoendelea nyumbani ni faraja muhimu kuliko sifa za kipuuzi unazojaribu kujiletea hapa.

    ReplyDelete
  3. Bora mdau umesema kweli, wangesema sisi watz tunaoishi bongo tuna tuma kiasi kadhaa cha pesa kusaidia ndugu zetu huko home, maneno meengi, fanyeni kweliiiii
    MONEY FIRST LOGOLOGO BAADAYE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...