wadau tunaomba maoni yenu. miaka ya 60 Mwalimu na wenzie waliisha tuonesha njia kuhusu vazi la Taifa. kwa twasira hii mwasemaje??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-12415348


    Hiyo Link hapo juu BBC wanataka kumjuwa waliombeba Nyerere kama wapo Hai wawaulize siku hiyo ilikuwa vipi na furaha yao?

    ReplyDelete
  2. Swaafi kabisa. Imekosekana kofia tu hapo. Lakini wabunifu wazitofautishe na za Nigeria.

    ReplyDelete
  3. Hikli haliwezi kuwa vazi la taifa. Labda husema vazi la kabila fulani ok. Mavazi ya kuwa nusu uchi si vazi hata siku moja.

    ReplyDelete
  4. iko poa kabisa uyo jamaa aliyevaa kama msuli juu na chini imetulia pia ata kivazi cha mwalimu kipo poa. ivyo vitengeee sio deal vileeeeeee

    ReplyDelete
  5. Hii ilikuwa ni wakati wa "zidumu fikra sahihi" sasa unataka kuturudisha huko?

    ReplyDelete
  6. Nimekaa miaka 15 Bolgatanga Ghana hilo vazi alilovaa Nyerere Wanavaa sana watu wa Ghana na Raisi Kwame Nkurumah lilikuwa ndio vazi lake mara nyingi.Sijui kwa nini Nyerere hakuamua kuvaa vazi la Kizanaki au watani wangu wazanaki hawana vazi rasmi la asili hadi wavae la waghana.

    ReplyDelete
  7. Kwa mtazamo wangu!! haitakaa itokee eti wabunifu wakae na kubuni vazi la Taifa na watu kulifuata...kwani jamii ni watu na kamwe mtu hawezi kuwaingiza watu maabara na kuwafania uchunguzi.Naomba niulize...ni nani alibuni watanzania kula mlenda, ugali,senene?????....huu ni utatamaduni ambao hutokea tu...pia kwa mavazi nayo hutokea tu kulingana na mila na destuli zilizojificha...hebu tuache kupoteza muda kwa jambo ambalo haliwezekaniki.

    ReplyDelete
  8. HUYO ALIYEVAA WAUITA KAMA MSULI JUU NA CHINI NI MTEMI ABDALLAH SAID FUNDIKIRA NA NI VAZI LA KINYANYEMBE !
    Kassembo

    ReplyDelete
  9. Nisomavyo mimi picha hiyo: Mwalimu alivaa vazi la Ghana, kama ilivyoonyeshwa na mfano wa Nkrumah. Wazo kuu wakati huo ilikuwa ni utaifa na pia Pan-Africanism. Je, mnakumbuka jinsi Mwalimu alivyokuwa msatari wa mbele katika kuhimiza umoja wa Afrika? Nadhani inafahamika pia kwamba wimbo wetu wa taifa ni ule uliotungwa na mtu wa Afrika ya Kusini, ukikusudiwa kuwa wa huko. Lakini kuupokea na kuutumia kwetu inaweza kuhesabiwa kama hatua za kujitambulisha na watu wa pande zote za Afrika kwa matumaini ya kufanya taifa moja la Afrika.
    BTW siyo kila kitu kilichokuwa cha enzi za "Fikra sahihi" ni kibaya.

    ReplyDelete
  10. Yaani, kweli wazee waachane na suti!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????na tai za hariri!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!??????????????????SIJUI.

    ReplyDelete
  11. Hilo vazi linafaa sana. Waanze viongozi wa serikali na wafanyakazi halafu sisi tutafuata ili mradi liwe na bendera yetu ya Taifa. Wanaotafuta waliombeba mwalimu ni wapuuzi tu wanaka kusanifu kuwa mbona mlimbeba ili wao waondoke, sasa mbona ndio wanakula mali ya taifa letu, madini wanachua kama yako chumbani kwao

    ReplyDelete
  12. They can go to hell. Vazi la taifa ndio nini bwana kila mtu avae anachopenda.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2011

    yes ni chief A. S. Fundikira na vazi la kinayanembe, la waaaa he is handsome

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...