Safu ya uongozi wa muda , kutoka kushoto_Misso Temu katibu wa Uchumi na Fedha,Abdallah Nyangasa Katibu mkuu,Novatus Simaba Mwenyekiti na Salum Rajabu Katibu wa Habari,Itikadi na Uenezi

Katika sherehe za kuazimamisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,zilizo fanyika Siku tarehe 5, February 2011, Katika jiji la Houston, TX.Uongozi wa muda wa Tawi la CCM-MAREKANI unafuraha ya kuwatangazia wapenzi na wanachama wake wote ufunguzi wa shina Jipya la HOUSTON NO. 1; shina hilo lilichagua viongozi wao wakiwemo ,mwenyekiti Cassius Pambamaji na katibu Shaibu Said.Pia katika sherehe hiyo Tawi lilifanikiwa kuandikisha wanachama wengine wapya kumi na wawili.

Pia ungozi wa Muda wa Tawi unapenda kuchukua nafasi hii kuutangaza uongozi wao ambao utakuwa madarakani kwa siku 120 toka ulipochaguliwa tarehe 2, January 2011.Viongozi hao wa muda ni kama wafuatao;

Novatus Simaba-Mwenyekiti

Abdallah Nyangasa-Katibu

Salum Rajab-Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi

Misso Temu-Kaitbu wa Uchumi na Fedha.

Kazi ya uongozi huu ni kuandaa na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi wa viongozi wa Tawi.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Salum Rajabu,

Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi, Tawi la CCM-MAREKANI

Abdallah Nyangasa akibadilishana mawazo na Viongozi wa Shina jipya
Lambaert na safu nzima ya uongozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hongereni sana wanachama wa CCM jijini Houston... kidumu Chama cha mapinduzi...
    Ninafurahi ninapoona vitu kama hivi, kwa sababu inamaanisha kuwa chama kinazidi kuwa karibu na wanachama NA wapenzi wake popote pale waishio duniani..
    Kupitia shina hili NA wao pia watapata kutoa maoni NA michango yao.

    ReplyDelete
  2. nyie nanyi hata hamuelewi mnaona CCM ya maana sana njooni kaeni muone kulivyo na maisha magumu kukaa gizani kukosa maji kwa wiki mara 2 maji ya natoka ndio mtajua.maana ulaya umeme kukatika ni ndoto na maji kukosekana ni ndoto,njooni home TANZANIA hahahaaaaaaaaa Dowans imekolea shida tupu

    ReplyDelete
  3. Wait a minute, naelewa CCM inataka kuwa na mashina mengi ila kusema ukweli kwa watanzania tulioko nje kujihusisha na politics instead of policies ni kukosa mwelekeo... Who doesn't understand our politics are misguided? In the end, sitaki nitaje majina ila kweli CCM imejaa mafisadi mpaka Marekani. Chipps zimegoma sasa tuna siasa

    ReplyDelete
  4. nyie watze wa ughaibuni mtaacha lini ulimbukeni wenu?mna exposure lkn bado ni bongolala,.anzeni kupigania haki yenu ya kupiga kura mkiwa uko na si mambo aya ya matawi ya chama.

    ReplyDelete
  5. Safi sana CCM Houston. Sky is the limit tumie fursa zozote zinazopatikana kujihusisha na mambo ya nyumbani. Dunia iko kama kijiji sasa hivi matawi ya CCM nje yanawezekana.

    ReplyDelete
  6. Mimi ningetegemea sisi tulio nje ya nchi esp Western countries ndo tungekuwa wa kwanza kuikosoa CCM kwa machafu yote wayafanyao. Kwani nchi tulizopo (za ughaibuni)zipo makini sana na mafisadi na zinasikiliza wanainchi, hivyo basi tuache tabia ya kuangalia tutafaidika vipi tukiwa wanachama wa CCM (kwani naamini ndo sababu ya wana CCM wa nje kujiunga na CCM). C'mon hakuna chochote CCM kinachofanya tunahitaji mabadiliko.

    ReplyDelete
  7. kabebeni mabox acheni upuzi wenu kujipendekeza

    ReplyDelete
  8. Acheni kuuza sura bwana huu ni utani wa hali ya juu mbona. Eti CCM MAREKANI mbona usiite CCM HOUSTON. Sasa CCM MAREKANI nani anawajua kama sio nyie tuu hapa. Give us a brake please.

    ReplyDelete
  9. Kaazi kweli kweli ila tutafika tuu hata kama baada ya miaka mia.

    ReplyDelete
  10. Kweli CCM chama kubwa, yaani imeshajieneza ktk mataifa manne yenye viti vilivyo na kura ya VETO- Umoja wa Mataifa ( USA, UK, Russia na China) bado kumalizia FRANCE ndio sijasikia.

    Kilichobaki ni CCM kuomba kuwa Mwanachama wa Kudumu Umoja Wa Mataifa aliye na kura ya VETO.

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

    Mdau
    Mkereketwa wa VETO.

    ReplyDelete
  11. Nyie kweli hamna kazi za kufanya,ccm ccm upuuzi mtupu.Mungefanya la maana mukaanzisha chama cha kusaidiana maziko,sio mtu akifa munaanza michango michango munashindwa kuzikana kwa kuendekeza upuuzi wa ccm.Hivi nauliza mbona ukitokea msiba hiyo ccm yenu haiwasaidii kusafirisha marehemu munabaki kuja hapa kutangazia michango,munaacha marehemu anateseka mochary mpaka anakaribia kuoza.

    ReplyDelete
  12. Hakuna kitu kibaya kama umasikini wa fikira.

    ReplyDelete
  13. UMASIKINI MBAYA BWANA!! PEOPLE WILL DO ANYTHING!!!
    ILA TUNAOMBA TU KWA NIABA YA WAMAREKANI TULIOKO MAJIMBO MENGINE. HILO JINA LOTOLEWE NA LIBADILISHWE LISIWE CCM MAREKANI!!! NYIE NI CCM HOUSTON, MAREKANI NI KUBWA NA INA-MAJIMBO ZAIDI 50 YANAYOJITEGEMEA. KAMA TEXAS MMEAMUA KUANZISHA CCM BASI NAMJIITE CCM-TEXAS AU HOUSTON NA SIO MAREKANI KUJIPA JINA MSILOLIWEZA. HIYO CCM MAREKANI INAWAKILISHWA NA NANI TOKA STATE NYINGINE, EBU MSITUTIE AIBU WENGINE HAPA. YOU ARE ON YOUR OWN!

    ReplyDelete
  14. HII HAINA HATA HADHI YA KUITWA CCM HOUSTON, ACHILIA MBALI CCM TEXAS. HAWA JAMAA WAKO KUMI NA MBILI TUU THEN WANAJIITA CCM MAREKANI, KUNA WATZ WANAGPI HAPA HOUSTON??? GIMME A BREEAAK!!!! HAPO KUNA JAMAA MMOJA KAMA SIKOSEI MAMBO YAKE HAYAJAKAA FRESH ALIKUWA ANAKIMBIKIMBIA TUU, MARA BONGO MARA UK MARA HUKU BASI SHIDA TUU. SASA ANATAKA MADARAKA. KWELI CHIPS NOMA......

    ReplyDelete
  15. HONGERA WANA CCM USA.

    HAKI YA KUSHIRIKI SIASA POPOTE PALE NI YA KILA MTU.
    CCM HAIMBAGUI MTU YEYOTE MAHALI POPOTE KUJIUNGA NA KULETA MAWAZO MAPYA.

    TAYARI TUNACHO CHAMA CHA MAPINDUZI(CCM)KILICHOTANDAA KWA WATU;SHINA HADI TAIFA, TUKIONGEZA WATU SAFI,SIASA SAFI TUTAENDELEA KUIMARISHA UONGOZI BORA...JIUNGE NA CCM SASA ILI TUIJENGE TANZANIA KWA PAMOJA KWA WAKATI MPYA. NCHI NI YETU WOTE.
    MAPINDUZI DAIMA SI LELEMAMA.

    MAINA OWINO.
    CCM UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...