Ankal Saalekoo,
Hii ni hali ilivyokuwa jana huko Mbezi Makabe mara baada ya kunyesha kwa mvua kwa takribani lisaa limoja na kupelekea maji kujaa namna hii barabarani na kulazimika kusubiri maji yapungue ili tuweze kurudi mjini.

Je serekali iko wapi?? ni lini tutawekewa Calavati hapo kwani ni pakorofi mno

Mdau James
wa
Mbezi Makabe.
watu wakilazimika kupita kwenye maji ili kuweza kuendelea na safari zao.
hapa chombo kimekwamba na mpango wa kukichomoa ndio ulikuwa ukiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Nawapeni pole sana sana
    Wasema serikali iko wapi?
    Why dont you organise yourselves and solve the problem,na jamaa mliozaliwa hapo wajitolee kwa misaada na umatamaduni
    We can do a lot all that is needed is determination and leadership

    ReplyDelete
  2. Mdau pole sana. Mmeishaambiwa sio kila kitu msubiri serikali! By the way, Mbezi Makabe nayo iko Dar es Salaam?

    ReplyDelete
  3. Ankal, habari za kazi.

    Niungane na watu wa Makabe. Ankal mie niko Mbagala. Tuna tatizo la kipande kifupi tu kuanzia Zakhem kuja Rangi 3. Sehemu imeharibika, mashimo kuliko handaki, lakini hakuna hata media inayotoa kipaumbele kutahadharisha na hata kustua watendaji. Ni sehemu ndogo, lakini foleni yake ni kuanzia dakika 45 hadi masaa 2. Vurugu za madereva, na sasa matope kama tuko Undendeule. Ankal tukuombe basi, kupitia blog yako, wastue hawa watu huko Tanroad au hata Hamashauri ya Temeke. Hii ni aibu sana, kura wameomba wamepewa, basi watekeleze ahadi zao. Sisi hatujasahau walivyosimama na kujinadi...... wakati ndo huu, na mvua ndio hizi zimeanza. Tutafukuzwa kazi kwa kuchelewa, na kuamka usiku wa saa 9, tutakumbana na matofali au visu vya wagombea senti 50. Hebu saidia, tembelea,chukua picha then weka bayana, tuone.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi munaosema raia wako wapi, kwani kodi zetu zote tunazolipa huwa zinakwenda wapi?

    Tusikubali tu kwamba tujitolee ni wajibu wetu kuulizia hizi kodi zetu nani anayezila????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...