Kaimu mkuu wa mkoa wa Kagera Samuel Kamote akimpatia zawadi ya shilingi laki mbili Mkuu wa upelelezi mkoani Kagera Peter Matagi kutokana na kazi nzuri aliyoifanya ya kufanikisha kukamata silaha 8 za kivita.
Askari ambalo jeshi la polisi mkoani Kagera limewazadia vyeti vya utumishi uliotukuka na pesa tasilimu shilingi 200,000 kila mmoja baada ya kufanikiwa kizinasa silaha nane za kivita ambazo ni AKA 47 na SMG,kutoka kushoto ni Dc Masalla, mkaguzi msaidizi Haji, Dc Amos na mkuu wa wa upelelezi wa mkoa wa Kagera Peter Matagi. Picha na habari na mdau Audax Mutiganzi wa Globu ya Jamii, Bukoba.

KAIMU mkuu wa mkoa wa Kagera Samuel Kamote amelitaka jeshi la polisi lisibweteke na sifa za mafanikio liliyoyapata ya kupambana uharifu badala yake liendelee kufanya kazi kwa bidii ili liweze kuukomeshe uharifu kabisa mkoani Kagera.

Kamote alitoa kauli jana katika hotuba yake wakati wa hafla fupi ya kuwazadia maofisa wa jeshi la polisi vyeti vya utumishi uliotukuka na fedha taslimu ambao walifanikiwa kunasa silaha 8 za kivita zilizokuwa zinatumiwa na majambazi kuteka magari kwenye mapori mkoani Kagera iliyofanyika kwenye makao makuu ya kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Kagera.

Kaimu mkuu huyo wa mkoa alisema jeshi hilo mkoani Kagera kwa sasa lilivyo linao uwezo mkubwa wa kukabiliana na janga lolote linalojitokeza mbele yake linalohusiana na matukio ya uharifu yanayojitokeza ndani ya jamii kwa kuwa limejipanga vizuri.

Alisema serikali mkoani Kagera itaendelea kulipa ushirikiano wa karibu ili liweze kufanikisha mikakati yake, Kamote alisema askari wa jeshi hilo hawapaswi kulala kwa kuwa waharifu huwa kila siku wanabadili mbinu za kutekeleza uharifu.

Alilitaka jeshi hilo liendelee na misako yake na doria zake ambazo linazifanya kwenye maeneo mbalimbali mkoani Kagera hasa kwenye mapori ya ambako utekaji wa magari huwa unafanyika.

Alilipongeza jeshi hilo kwa kazi linayoifanya ya kupambana na uharifu, alilitaka jeshi hilo liendelee kuwa karibu zaidi na wananchi ili liweze kukabiliana kwa urahisi na vitendo vinavyopangwa kutekelezwa na waharifu ndani ya jamii.

Alilitaka pia jeshi la polisi liimarishe pia mfuko wa kuwazadia wananchi wanaotoa taarifa zinazohusiana na masuala ya uharifu kwa jeshi hilo pia askari wanaoshirikia katika matukio ya kupambana na uharifu, kaimu mkuu huyo aliuchangia mfuko huo shilingi 500,000.

Kwa upande wake Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Henry Salewi alisema jeshi hilo limewazadia askari ambalo wlishiriki kwenye operation ya kukamata silaha nane zilizokamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo ya Chato na Kahama mkoani shinyanya zilizokuwa zikitumika kutekeleza vitendo vya uharifu hasa utekaji wa magari.

Alisema kwa mujibu wa upelelezi uliofanywa na jeshi hilo silaha hizo zimeishafanya matukio makubwa ambayo ni pamoja na mauaji, alisema silaha hizo zilimuua mmiliki wa kituo cha mafuta cha mwendo wa saa, wizi wa vocha za mamilioni uliofanyika wilayani Chato.

Salewi aliwapongeza wananchi walitoa taarifa za upatikanaji wa silaha hizo, aliwaomba wananchi waendelee kuwa karibu na jeshi la polisi ili lieendelee kuongeza hali ya amani mkoani Kagera.

Maofisa wa jeshi la polisi waliopewa zawadi ya vyeti vya utumishi uliotukuka na pesa tasilimi kila mmoja shilingi 200,000 ni pamoja na Mkuu wa upelelezi wa mkoa Peter Matagi, Dc Amos, Dc Masalla, Dc Tumaini na Mkaguzi msaidizi Haji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Common mwananchiMarch 31, 2011

    Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza sana hao askari kwa kitendo chao cha ushujaa cha kukamata hizo silaha, maana raia hawana sababu ya kuzimiliki silaha za kivita kwani ni hatari kwa usalama wa raia wengine.

    Pia napenda kupongeza jeshi na serikali ya mkoa kwa kutambua hilo na kuwazawadia, sina tatizo na cheti cha utumishi uliotukuka LAKINI nahisi motisha wa fedha ulioambatana na cheti hicho ni kidogo. Yaani mtu aliyekamata silaha nane za kivita anapewa sh 200,000/= tu? Sina hakika kama hiyo ni motisha stahili ya kuwafanya wao na wengine kuweza kukabiliana na makosa mengine mengi na pengine makubwa zaidi. Najiuliza askari hao au wengine wasio waaminifu ikitokea siku nyingine wakikamata wahalifu (ambao wana pesa za kihalifu na mchezo) na wakapewa hata laki tano tu ili kushiriki au kuruhusu uhalifu utendendeke hawatashawishika kweli???? Hii ni mantiki tu, ni mantiki tu


    Nafikiri askari wakiwa wanapatiwa motisha wa kutosha basi itawaongezea nguvu za kupambana na makosa mengine na kukataa vishawaishi kama vya ruswa au hata kushirikiana na wahalifu. Katika mazingira ya laki mbili haziwezi kufua dafu kwa fedha za hongo (kama wataamua kupokea) za wahalifu. Pia hii inaweza kuwafanya wahalifu kupanga bei za hao askari kulingana na uhalifu wanaotaka kuufanya kwa kujua watapewa motisha kiasi gani na wao kuzidisha dau. Basi ifike mahali serikali na jeshi vitoe motisha wa kutosha zaidi ili kuongeza morali ya askari kukabiliana na uhalifu na vitendo by rushwa. Vinginevyo kama ni zawadi za laki mbili kwa silaha za kivita nane basi ni vizuri makabidhiano hayo yakifanyika kimya kimya ofisini ili hata wahalifu wasiweze kujua na kuwapangia bei au wapewe vyeti tu. Dadisi

    Naomba kuwakilisha Ankal

    Common mwananchi

    ReplyDelete
  2. Napingana na mtoa maoni kwa jina la Common mwananchi, kimsingi motisha wa laki mbili kwa polisi ni sawa kabisa, kwa nchi nyingine unapewa cheti tu kinatosha na skari anakuwa ameridhika kwa mchango wake kutambuliwa kwani kukamata silaha na majambazi ni wajibu wa jeshi la polisi. Hapo kilichofanyika ni sawa tu na hata wasingepewa pia ilikuwa sawa kwani wametekeleza majukumu yao kama askari wa polisi. Ingekuwa ni raia ndio wamekamata hapo sawa

    Naomba kuwakilisha hoja

    Igwamanoni Lufulundama, Mwanza

    ReplyDelete
  3. Hamuoni kuweka picha za mashujaa hao hadharani ni hatari?

    ReplyDelete
  4. Sikubaliani kabisa na mchangiaji wa kwanza aliyejiita common mwananchi kuhusu motisha kwa polisi. Kimsingi hiyi ni kazi yao na hivyo anapofanikiwa kufanya jambo kama hilo anapaswa ajipongeze kwa ushujaa kuwa kumbe anaimudu kazi yake hata sipopewa kitu. Huo ujambazi unaathiri hata ngugu zake, watoto wake, rafiki zake n.k. kwa hiyo ni wajibu wake kuwaepusha. Pia pesa haitoshekwi. hata ukiwapa milioni tano bado watataka zaidi. Kwa hiyo uadilifu ni hulka ya mtu na sio pesa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...