Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Peter Kallaghe

JUMUIYA YA WATANZANIA- TANZ-UK ikishirikiana na tawi la Reading (TA Reading)
Inapenda kuwatangazia watanzania wote waliopo Reading, Slough, Oxford na vitongoji vingine vya karibu kuwa Imeandaa ziara maalum ya Mheshimiwa Balozi Kallaghe ya siku tatu itakayofanyika katika mji wa Reading kuanzia tarehe 8-10/4/2011. Sambamba ya ziara hii Mh Balozi atapata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali za kimaendeleo zifanyazwo na wajasilimali wa kitanzania na pia kukutana na wanajumuia wote.

Hivyo basi kutakuwa na sherehe maalum ya kumkaribisha Balozi wetu hapa Reading tarehe 9/4/11 kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 12 jioni baada ya hapo kutakuwa na tafrija pamoja na mziki kuanzia saa 1 usiku mpaka saa 6 usiku. Tafadhali wahi mapema

Ukumbi na adreess ya kwenye sherehe
Amersham Road Youth & Community CentreAmersham Road,
Caversham,
Reading,
Berks,
RG4 5BP

Tunawomba watanzania wote mjitokeze kwa wingi ili kumkaribisha Balozi wetu. Kuja kwenu ndio kufakisha kwa ziara hii muhimu, tafadhali mjulishe mwenzio.

Ratiba Rasmi ya ziara kamili itatolewa baadaye.

Asanteni kwa ushirikiano wenu,

Mwenyekiti
Tanz- UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Karibu sana Balozi wetu.

    http://www.youtube.com/watch?v=Mp-N4gSkaEg

    ReplyDelete
  2. Mhe. Balozi Kallaghe,
    Watanzania wataendelea kukukaribisha Reading na mikoa mingine yote ya UK. Tanz UK msisite kuyashirikisha makundi na taasisi zote za Watanzania ktk mchakato wa Kumkaribisha na kumshirikisha Balozi wetu Kallaghe katika harakati za maisha yetu hapa Ughaibuni.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    MAINA A. OWINO
    CCM UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...