Vikombe vikiwa vimejazwa dawa inayodaiwa kutibu magonjwa mbalimbali sugu inayotolewa na Dada Fatma Said Senga ( 41) mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, ambapo watu zaidi ya 200 wamepata kikombe hicho ambapo gharama ni shilingi za kitanzania 200 tu.
Dada Fatma Said Senga akiwa na mjukuu wake Ashinuli Ally Pitchuo ( 4) ambaye ni mgawaji wa dawa yake kwa wagonjwa na kulia ni mmoja wa ndugu yake anayeishi nae nyumbani hapo
Dada Fatma Said Senga akiwaonesha viongozi waliomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichangani, Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu tiba yake hiyo ( anaye mfuatia ) ni mwandishi wa habari aliyetembelea eneo
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( kulia) akimpatia maelekezo ya Dada Fatma Said Senga anayewatibia ya watu wenye magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu kikombe cha dawa aweze kusajili huduma hiyo na kupimwa dawa yake ili kulinda usalama wa afya ya watumiaji
Dada Fatma Said Senga ( 41) mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro, ( mwenye ushungi mwekundu ) akimwaonesha viongozi waliomtembelea nyumbani kwake eneo la Kichangani, Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu tiba yake hiyo ( anaye mfuatia ) ni mwandishi wa habari aliyetembelea eneo hilo Machi 31, mwaka huu wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu ( hayupo pichani), kazi hiyo ameianza machi 30, mwaka huu na kikombe ni 'bati' (sh. 200/-). Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Listen-acheni kuchonga. Mimi napiga vikombe vyooooooooooooote kila mahali naenda. U neva know unaumwa nini na ukimaliza vyote uwezekano wa kufa ni mdogo sana.

    Nyie mnaochonga ni kwakuwa mko nje ya nchi na hamuwezi kuja kunywa dawa. Sasa pandeni ndege mje ama sivyo kaeni kimya.

    Nakunywa vikombe vyote-mbeya, Tabora, Morogoro, Moshi, Arusha. Mkisikia mwingine msisite kunijulisha

    ReplyDelete
  2. Simwamini kabisa!!! Utapeli umeanza!

    ReplyDelete
  3. sasa hii imepitiliza manake kila mkoa atatoka mtu kaoteshwa na MUNGU nasikia pia mbagala charambe yupo tena na wote wanatoa vikombe ,inabidi watanzania tuwe makini sana na hizi tiba japo kila mwenye tatizo la maradhi akisikia tiba kwa imani yake atataka kupona,ila sasa tunaelekea mikoa karibia yote watoke watoa kikombe.


    mama p

    ReplyDelete
  4. In fact, this is too much kwa kweli. Tubadilishieni wimbo huu maana kila kikucha kikombe, kila mahali kikombe. Wote hawa walikuwa wapi kabla ya babu?

    ReplyDelete
  5. Musa alipotumwa na Mungu kufanya miujiza na waganga wa Pharaoh walifanya miujiza hata kutengeneza nyoka hai kabisa. Haya yote yanatokea ili kutengeneza mazingira ya mashaka ili watu wasio na imani waingie mashaka juu ya mchungaji Mwasapile.

    Hebu tujiulize kwa nini ijapokuwa kumekuwa na waganga wengi sana Tanzania hakujawahi kuwa na ushindani wa ghafla wa namna hii. Halafu Mchungaji Mwasapile hakujitangaza, watu ndiyo waliyemtangaza.

    Kuna wakati fulani alitokea mtumishi wa Mungu (Nabii) kule Naigeria akaanza kutabiri matokeo ya kombe la dunia. alipofanya hivyo tu akatokea Pweza Paulo akaanza kutoa matokeo.

    Kazi ya shetani ni kupinga watu wasimwamini Mungu.

    Sasa uamuzi ni wa kila mtu aamue mwenyewe.

    ReplyDelete
  6. Hamna lolote, hawa wengine wanakuja tu kumvurugia "Babu" ila hawamuwezi hata kidogo, Mungu wake yuko juu!

    ReplyDelete
  7. heeheeeeeeeehee kaaaaaaazi kweli kweli mwaka huu. iankuaja tu hiyo mwisho kila mkoa wa tanzania kutakua na babu au bibi kikombe .ujue kama hili dili tu apa .

    ReplyDelete
  8. hahahaha kazi ipo, kila mtu anatoka na kikombe nani atatoka na KIBAKULI?

    ReplyDelete
  9. wataibuka matapeli kwenda mbele you wait.

    ReplyDelete
  10. kaaazii kweli kweli sasa hivi utasikia kikombe UK au US tusubiri kwa wapiga maboksi

    ReplyDelete
  11. pakakalakashataMarch 31, 2011

    HAHAHA JAMAANI WATANZANIA KUNA MSIBA MKUBWA UNAKUJA KAMA MUNAFANYA MASIHARA NA VIKOMBE SHAURIYENU KILA MTU AKITOKEZEE WATU TELE WANAKIMBILIA KUNYWA KITU WASICHOKIJUWA JAMAANI JAMANI KUWENI MAKINI HILI JAMBO SIO MASIHARA LITAKUJA KUWA BALAA KUBWA SIVYO MUNANYO FIKIRIA

    ReplyDelete
  12. michuz ulitakiwa uende loliondo utupe habari wewe mwenyewe kuliko ya kuambiwa ingia kwenye blog ya frolah saloon kaweka story nzuri sana yeyey mwenyewe alikwenda huko. mdau wa texas

    ReplyDelete
  13. sasa mwendo wa kikombe ni mwendo mdundo kwa kwenda mbele kila mtu yeye kakazana na kikombe daaa kazi kweli kweli hii Tanzania, kumuon babu ambi tuu na kikombe imekuashida kila mtu naye aiga kikombe, basi imekua tabu.

    ReplyDelete
  14. Yule dada wa Tabora alisema wako watatu! Sasa kumbe wanne!!

    ReplyDelete
  15. hamna kitu,wote hawa wanataka kumuaribia tuu babu by the way mbona hawa wote walojitokeza baada ya babu cjackia hata mtu mmoja katoa ushuhuda kuwa kapona kutokana na dawa alopewa na hao watu kama kwa babu?jamani tusimameni imara na tusiwe na imani duni




    winnie

    ReplyDelete
  16. huu ni mwaka wa vikombe ,kwa hakika Tanzania ni nchi ya kishirikina

    ReplyDelete
  17. MGANGA WA KIENYEJI HUYO KUANZIA JINA MPA MUONEKANE WAKE

    ReplyDelete
  18. Hivi jamani haya mambo ya kuchangia hivi vikombe ni hatari kwa maradhi ya kuambukiza sasa sijui hawa wagawa vikombe wanaruhusu kuchukua kikombe chako mwenyewe?Au ndio lazima ananihii!!

    ReplyDelete
  19. KIKOMBE KIKOMBE KIKOMBE

    ReplyDelete
  20. ah..sasa huu ni upumbavu...kila mtu anajitokeza kila baada ya cku tatu..!!!watu wameshaona jinsi ya kutengeneza hela fasta eeh..playing with pples beliefs..

    ReplyDelete
  21. kwani huyo babu naye ni mganga wa kienyeji tu, kwani jina lina maana gani, acha hizo. wote ni witch doctors tu hakuna babu wala nini

    ReplyDelete
  22. I knew it. It seems like a game now.

    I'm currently preparing my trip to Loliondo; now, I can't go any more.

    Mdau Ethiopia.

    ReplyDelete
  23. ebu watoe upuuzi wao sisi tunamjua mmoja tuu mwasapile hawa wengine wapuuuuuuuuuuuziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  24. Jamani huyu mama ASHINDWE ktk jina la YESU!!! Hawa watoa vikombe walikuwa wapi siku zote?? Mpaka babu Ambi katokea na kaanza kazi toka last year mwezi wa nane(8)tena babu wala hajajitangaza hata siku 1 kwa vyombo vya habari ni watu waliopona au kupata kikombe kwake ndio wamefanya ajulikane! walikuwa hawajaoteshwa tu jamani? Kweli maisha magumu UTAPELI kwa kwenda mbele.Kwanza huyu mama asije mfundisha huyo mjukuu wake mambo ya ajabu na uchawi na shule asiende kabsa.

    ReplyDelete
  25. SASA DADA UMEMALIZAYOTE, YAANI WEWE UNA VIKOMBE MCHANGANYIKO HATA VYA KIOO NIMEONA AMABAVYO HAVIJAWAHI KUTUMIKA NA TENA NI MUISLAM. MAANA NILIKUWA NAJIULIZA WAKRISTO TUU KOUTESWA! KWA KUWA TIMU IMEKAMILIKA, KAZI ILIYOBAKI NI KWA WANYWA HIVYO VIKOMBE. KAZI IPO!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  26. Wabongo wana tabia za ajabu sana!! Kuona babu mambo yanakwenda vizuri kila mtu sasa anajifanya ameoteshwa dawa!! No wonder kila mtu huku sinza anafungua bar au grocery!

    ReplyDelete
  27. this is madness!!!

    ReplyDelete
  28. Waganga wa kienyeji wamechukia sana kufahamika kwa Babu kwani Kuku walizokuwa wakiwaagiza wateja wao hawapati tena, wote wamekimbilia Loliondo.

    ReplyDelete
  29. hahahaahha jamani kweli huu mwaka wa kikombeee!!! alafu why wote bei 500shs???

    ReplyDelete
  30. Yote haya ni heri labda itasaidia kufungua macho watu kujua hivi vikombe vyote hivi ni uongo. Wananchi wamekata tamaa na tiba za hospitali either hakuna tiba za uhakika au hawawezi kuzidumu.

    ReplyDelete
  31. Shilatu.
    Natoa mwito kwa kila mtanzania kuwa mwangalifu maana serikali imeshindwa kazi, haiwezi kumlinda mlaji, au mnywaji. Tutanyweshwa hata sumu.
    Fikiria huyu wa moro kesha wanywesha 200 kabla dawa yake haijathibitishwa, je ikijaonekana ni sumu au si chochote?
    Pia je tunazipima hizo roho zinazoambatana na uganga huu?

    ReplyDelete
  32. Wakuu, huu ujasiriamali jamani sasa. MKURABITA na MKURUKUTA vimekuwa ni hadithi na ndoto za mchana kwa walala hoi, kwa hiyo kila nafasi inapogundulika ya kujipatia kipato, basi wenzangu na mimi lazima waiibukie kama hawana akili nzuri. Maisha magumu jamani tuelewe, kama ninyi ni watoto wa vigogo wa CCM mnaokula kwa mirija na kuandaliwa vyeo nchi hii mtuache sisi jinsi tulivyo tupambane na maisha. Akili kichwani, hata viongozi wa serikali za mitaa wanaunga mkono, si unaona kule loliondo wanakatiwa kiasi na babu. Kwa hiyo acheni longolongo, hata mikoa yote wakiibuka sawa maana ni mbadala bora kuliko hizo ndoto za MKURABITA na MKURUKUTA.

    ReplyDelete
  33. Serikali inatakiwa kua makini na hawa watoa vikombe,si raia km 500 wanakunywa dawa mfamasia ndo anakuja kupima

    ReplyDelete
  34. Huyu SHANGAZI wa MOROGORO anataka kukamata vichwa vingi MKWALA wake BEI yake shilingi 200.
    Haya tunasubiri mwingine tena MPYA wa kuoteshwa ili tuone atakuja na staili ipi

    ReplyDelete
  35. Huyu nae kaoteshwa au anatumia mikoba ya kwao? Ole wake amzulie mtume s.a.w kumuotesha, niwajuavyo waislam watamtenbezea bakora hata alitamani kaburi.

    ReplyDelete
  36. MIMI KWA KWELI SITILII MASHAKA IMANI ZA WATU.NI VIZURI WATU WAKAAMINI WANACHOAMINI NA UHURU WA KUFANYA HIVYO UKAWEPO; ILA SERIKALI INATAKIWA KUWA MACHO NA VITU HIVI SASA KWA KUWA VIMEANZA KULITIA TAIFA DOA. KITENDO CHA HATA VIONGOZI WA NCHI KUHUDHURIA KUPATA VIKOMBE IWE NI KWA IMANI YAO; LAKINI BASI KUWE NA TARATIBU AMBAZO ZIMEWEKWA ILI TAIFA LISIWE NA MUONEKANO TOFAUTI NJE YA MIPAKA YETU. KWA HIVI SASA BAADA YA MFUMUKO WA HAYA YOTE; TAIFA ZIMA LINAONEKANA NI LA WASHIRIKINA KWANI HAKUNA TARATIBU ZOZOTE ZINAZOONEKANA KUWA ZA KUELEWEKA ILI YANAYOTOKEA YAWE YAMAERATIBIWA KWA KUFUATA KANUNI ZA AFYA; TARATIBU ZA NCHI NA IMANI ZA WATU. SASA TUNAONEKANA WOTE HATUNA MSIMAMO; NA BAYA ZAIDI SERIKALI INAONEKANA KUBURUZWA.
    KINACHOFUATA NI WALE WAGANGA WALIOKUWA WANAWAAMBIA WATU LETENI KUKU; MBUZI; NGOZI YA MTU; KIDOLE NK NK WATAANZA NAO KUJITOKEZA NA KUCHEMSHA MIZIZI ILI WAPATE IDADI KUBWA YA WATU KAMA WANAOPATA HAWA. WENGINE WATAANZA KUWADANGANYA WATU MKINYWA KIKOMBE MTAKUWA MATAJIRI. HII INAANZA KULETA HOFU YA KITAIFA. SERIKALI INAPASWA KUINGILIA HAYA MAMBO KATI NA KUSEMA 'SASA BASI'!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...