Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Nyumba Poa Huko Kigamboni Jijini Dar es salaam jana, Mradi huo unaendeshwa na Kampuni ya Nyumba Poa LTD inayoendeshwa na vijana Watanzaia walioamua kutoka Ughaibuni na kurudi nyumbani ili kuwekeza katika kusaidia kukuza uchumi wa nchi yao lakini pia kusaidia jamii katika kupata nyumba bora kwa bei nafuu.

Nyumba iliyozinduliwa inagharimu Milioni 25 za Tanzania na inaweza kupanda kutegemea na mahitaji ya mteja mwenyewe anataka nini kiongezeke katika kuboresha zaidi nyumba yake, Lakini pia nyumba hizo zimebuniwa ili kusaidia watu wenye kupato cha kawaida ambao kwa upande wao kujenga inakuwa ni kazi ngumu hivyo kupitia mradi huu wa Nyumba Poa Model House watu wa kipato cha chini wanaweza kujipatia nyumba bila matatizo

Akizungumza katika uzinduzi huo Mh. Bernald Membe ameishukuru kampuni ya Nyumba Poa LTD kwa kuanzisha mradi huo hapa nyumbani kwani wameamua kuitikia wito wa serikali na kuja kuwekeza nyumbani, amesema Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete pamoja na yeye mwenye wamekuwa wakiwaasa Watanzania wengi walioko nje ya nchi kurudi nyumbani na kuwekeza au kuwekeza nyumbani wakiwa hukohuko nje jambo ambalo Kampuni ya Nyumba Poa LTD imeitikia kwa vitendo.

Wanaoshuhudia ukataji wa utepe kutoka kulia ni Daniel Mziray Mkurugenzi wa ufundi wa Kampuni ya Nyumba Poa LTD na Peter Malika Mkurugenzi wa Kampuni hiyo.

Kwa Hotuba kamili ya Mh Membe
BOFYA HAPA.
Mkurugenzi wa Nyumba Poa LTD Bw. Peter Malika akizungumza katika uzinduzi huo na kutambulisha wafanyakazi wenzake wa kampu ni hiyo
Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Nyumba Poa LTD Bw. Daniel Mziray akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kiamataifa wakati alipokuwa akitembelea na kujionea nyumba hiyo.Model ya Nyumba poa
Waziri Bernald Membe wa pili kulia akizungumza na wakurugenzi wa Kampuni ya Nyumba Poa LTD mara baada ya kuzindua mradi huo jana kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni hiyo Daniel Mziray katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Peter Malika kushoto Mwisho ni Mama Bertha mkuu wa Kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya nje.
Waziri Bernald Membe akiwasikiliza Investors Strateges Partiner wa Kampuni ya Nyumba Poa kushoto anayezungumza ni Gerald Heyder na katikati ni Pramod KumarJain wa Interglobe Export Corp. ya New York Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. na uraia wa nchi mbili je?

    ReplyDelete
  2. Tupatie contact address zenu maana hizo ndiyo nyumba type yetu sisi wafanyakazi wa Serikali.

    Mikopo benki haichukuliki kwa riba tunatarajia nyinyi mutakuwa na makubaliano yaliyo na unafuu.

    ReplyDelete
  3. hii ni safi sana. watanzania mlioko nje endeleeni kuwekeza nyumbani.
    msisahau kilimo na mambo mengine. serikali inatakiwa kuwapa kipaumbele
    watanzanio walioko nje na ndani ya nchi kuwekeza tanzania. serikali isipendelee matapeli kutoka nje.

    ReplyDelete
  4. Mutalemwa baitaniMarch 03, 2011

    Hongera sana ndugu Peter Malika kwa maamuzi uliochukua ya kuwekeza katika nchi yako ya Tanzania,pia hongera kwa kuleta maendeleo katika jamii yako kwa ujumla na watanzania wote,Mungu akubariki sana na kukupa akili ya kugundua uwekezaji mwingine zaidi ya huu kwa ajili ya maendeleo ya taifa kwa ujumla..
    Pia napenda kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh jakaya Mrisho Kikwete kwa kutoa changamoto zidi ya Watanzania waishio nchi za nje kuja na kuekeza nchini mwao,pia shukrani zingine zimwendee Waziri wa nchi za nje Mh Benard Membe kwa kauli nzuri ya kuwatia moyo Watanzania wanaotaka kuwekeza nchini mwao..

    Mungu akubariki sana Peter Malika katika uwekezaji wako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...