Na Tiganya Vincent_MAELEZO-Dar es salam
Serikali imeliagiza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa maeneo ya Kigamboni na jirani yake.
Daraja hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 130 hadi litakapokamilika kwa ajili ya matumizi ,ambapo NSSF itatoa bilioni 100 na Serikali bilioni 30.
Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kutembelea eneo la Kurasini Vijibweni ambapo Daraja hilo linatarajiwa kujengwa.
Alisema kuwa asilimia 60 ya fedha walizonazo NSSF ambazo ni sawa na bilioni 100 zinatosha kuanza ujenzi wa daraja hilo wakati Wizara ya Ujenzi inatafuta asilimia 40 sawa zaidi ya bilioni 30 zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa daraja zima.
"Tumezungumza siku nyingi kuanza ujenzi wa Daraja la Kigamboni ifike wakati tuanze kwani Serikali haiwezi kukosa asilimia 40 ya fedha zinazohitajika kukamilisha ujenzi huo" alisema Magufuli.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali itajitahidi kutafuta fedha ikiwemo kutenga katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa Daraja hilo unakamilika kabla ya uongozi wa awamu ya nne haujamaliza muda wake.
"NSSF nawaomba mjitahidi kukamilisha taratibu zote na kisha wiki ijayo (Ijumaa ) mtangaze zabuni ili ikiwezekana ujenzi uanze mara moja ...ili likikamilika litusaidie katika kupunguza msongamano katikati ya Jiji kwani feli zitaanza kusafirisha abiria kwenda Tegeta na Bagamoyo badala ya kutumia barabara" alisistiza Dkt Magufuli.
Alisema kuwa ki msingi NSSF kutokuwa na asilimia 100 za fedha zinazohitajika katika ujenzi wa daraja hilo hakuwezi kuwafanya wasianze mradi kwani katika mradi wowote mkandarasi anaanza kwa kulipwa fedha kiasi na kisha anaongezewa kulingana na anavyoondelea na mradi.
Dkt. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa Daraja la Kigamboni ni muhimu kwa kuwa eneo hilo linachukua wananchi wengi wanaofanyakazi katikati ya Jiji la Dar es salam halikadhalika kuna miradi mingi inayotarajiwa kuanzishwa ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Mabasi yaendayo katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na kuwepo kwa viwanja 10,000 vya NSSF.
Kufuatia umuhimu wa Daraja hilo Waziri huyo aliwahakikishia viongozi waandamizi wa NSSF kuwa Serikali kupitia Wizara yake watachangaia asilimia 40 ya fedha zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi wake.
Alisema watatumia kipindi cha miaka mitatu kuhakikisha wanamaliza fedha hizo ambazo Serikali inapaswa kuchangia.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Crescentius Magori alisema kuwa NSSF hadi hivi sasa ina kiasi cha bilioni 100 kati ya bilioni 130 zinazohitajika ili kukamilisha ujenzi haraka.
Alisema kuwa daraha hilo litakuwa na njia nne za magari na mbili kwa ajili ya watembea kwa miguu kupita.
Hivyo Magoro amemuhakikishia Waziri huyo kuwa watajitahidi kutangaza zabuni wiki ijayo mara baada ya kuhakikishiwa kuwa Serikali itachangia asilimia 40 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo.
Daraja la kigamboni linatarajia kuchukua miaka mitatu hadi kukamilika pindi ujenzi wake utakapoanza.
Viongozi wetu wa ngazi za juu wanampunguzia Dr. Magufuli (mzee wa kazi) morari wa kufanya kazi, hili daraja litajengwa kweli! unaweza usikie kesho waziri mkuu anasimamisha mpaka kikao cha baraza la mawaziri kitoe maamuzi!
ReplyDeleteHapo daraja linapoishia , zinaendelea njia ngapi, msisahau kuwa pale BENDERA TATU huwa pana foleni ya kufa mtu
ReplyDeleteOne thing I am certain is there are few leaders in the government like Magufuli this guy is a genius and I have said this time and time again.We need such people in most important field wish there was one like him in ministry of energy no offense but the current one sux
ReplyDeleteSafi sana NSSF, Safi sana Dr. Magufuli, hiyo ndiyo kazi kwa vitendo ambayo Watanzania tunasema kila kukicha. Inakuwaje Waheshimiwa wengine wanashindwa kufanya kazi kwa vitendo? Napendekeza pia mashirika mengine au taasisi nyingine za kifedha ziige mfano wa NSSF kuipenda nchi yao na kufanya kazi kwa ajili ya vizazi vijavyo, wagawane vipande vya barabara, wengine watengeneze Fly overs, wengine wapanue barabara zetu, wengine wajenge madaraja, yote hii ni katika kuiletea Tz maendeleo. Hebu tuache kufikiria matumbo yetu, tuamke tuonyeshe mifano hai. Binafsi nawapongeza sana NSSF. Kuna shirika fulani wakati fulani lilijitolea kuweka alama za barabarani Dar es Salaam, sikumbuki ni shirika gani, ila nao nawapongeza sana. Tunaomba na wengine wajitolee kuweka hata taa za barabarani, kwenye vivuko n.k, watu wanagongwa na magari kila siku. Mungu ibariki NSSF na Magufuli, na uiinue Tanzania. Chapa kazi Magufuli usisikilize story!
ReplyDeleteHata kama watu wataweka matumbo mbele lakini kazi ikaonekana na ugumu wa maisha ukapungua, sisi hatuna shida. Hata ulaya, marekani na asia kula kupo ila kazi zinaonekana. acha wale lakini kazi ionekane. Ben na Ruksa walikula lakini kakazi kalionekana. si haba.
ReplyDeleteWaziri Magufuli ni mtu wa kazi si rahisi kumzuia kufanya kazi. Anapenda kazi yake na kasi yake ni ya juu sidhani kama Waziri Mkuu ataweza kumzuia kwa hilo maana amezaliwa nalo. Hongera sana NSSF. Hongera sana Waziri Magufuli.
ReplyDelete