Ankal!
Hahahhaahaaaaaaaa....mada za wadau wako wallahi tena zinaniua. Unajua mie ni juzi juzi tu nimeanza kusoma blg yako. Nikawa sielewi kwa nini wadau wanakupapatikia, ikizingatiwa kuwa habari ni zile zile, sema zinawahi kutoka kabla ya chombo chochote cha habari huko Bongo. Kwa hilo nakupa FIVE!! Maana sijaona blg yoyote ya mfano wako – unahabarisha, unaburudisha, unasikitisha na saa ingine unaelimisha. Ubarikiwe ndugu yangu.
Pamoja na kukufagilia huko, Ankal, name pia nina kashida kadoooogoooo naomba wadau wa blg yako ya jamii wanisaidie. Ila hala hala ndugu yangu, email yangu usianike hewani maana ni soooo wakinijua ni mimi.
Ni hivi ankal. Mie niko huku ughaibuni (naomba nisitaje mji kwa sababu z kiusalama) na ni mwaka wa tisa sasa. Boksi nimebeba, vibibi nimeosha na pasi za mashuka hotelini nimepiga sana tu. Hivi sasa mambo yamejipa, sibebi tena boks, na wala siko katika home za vizeei. Nna kazi yangu ya maana na bonge la mshahara. Nadhani hata mshkaji wako JK haingii.
Vile vile (i might be blowing my own whistle, but hey, it’s true, man, so let’s move on!) mie ni bonge la handsome. Yaani kuhusu maswala ya totozzz wala sina shida. Wanajiletaga wenyewe tu. Ila nna tatizo sugu ambalo naomba wadau wa blg yako ya jamii (wataalamu tu, sio vilaza tafazali) wanisaidie.
Mie bwana kaka Ankal, pamoja na yote hayo nna bonge la tatizo moja. Kikwapa sina na nikikohoa wala sibanji. ukiniona kwa haraka haraka, kama we ni demu, lazima ugeuze kichwa. Tatizo ni kwamba nna mtindio wa MVUA YA DENDA.
MVUA YA DENDA niliyonayo ni kwamba kila ninapoongea na mtu mate huwa hunitokaga kwa wingi na kumpakaza nnaeongea naye. Na wakati wa kula i.e. mishikaki ama msosi wote wa jumuiya, kila nifunuapo kinywa mvua hiyo hunitoka, na kuwa kero kwa wenzangu.
Nina miaka 35 sasa na nshakula nondozzz hadi ya masta (taaluma siitaji, nisije stukiwa bureee), na sijui hii gharika ya DENDA imeanza lini. Maana niko fiti, ngoma sina (napima kila baada ya miezi 6, mara ya mwisho Ijumaa ilopita – niko swafiiiii). Ila tatizo ni hiyo MVUA YA DENDA ambayo imenifanya niwe gumzo kwa wenzangu.
Hivyo basi kwa heshima na taadhima naomba kujua mie nna tatizo gani, na nifanyeje ili nikaushe MVUA YA DENDA nilioyanyo. Na, je, ni mie peke yangu ama kuna mwenye tatizo kama langu?????
NA JE TIBA NI NINI?????
Ankal naomba kuwasilisha. Ila Chonde , chonde na Chonde chonde tena na tena, email yangu kapuni tafazali
MDAU WA Desh Desh Desh....
Wewe ni ZERO kabisa. Hapa kwa michuzi ni kukali sana.. moto umewaka na nyie wabeba maboksi mmeanzisha haya mambo. MTAKOMA.. Wewe NAHISI umelogwa kwasababu umetoka na mke wa mlalahoi ulivyokua bongo.
ReplyDeleteInabidi urudi Bongo na uwende Loliondo.
Mshikaji ibuka Loliondo, kama kuna dawa ya magonjwa sugu, nadhani hili lako ni cha mtoto. Utapigwa na nusu kikombe tu, Mvua itakuwa ukame. Then mademu hawatakuwa na haja ya myamvuli wakionge na wewe.
ReplyDeleteInaonekana una maradhi ya KIHERE-HERE
ReplyDeletekama uko ughaibuni kinachokushinda kwenda kwa daktari ni nini? au unataka tu kujishaua kua umesoma,una hela na ni handsome?? hebu peleka stress zako huko.hapa kwa michuzi hakuna wa kukupa wa attention..
ReplyDeletepole ndugu yangu, nakushauri usiwe unaongea kwa haraka haraka, unaweza punguza tatizo hili kwa asilimia 30% mwanzoni na baadae litaisha endapo utamanage kujicontrol.
ReplyDeletemjita(cherkasi)
Mama mbavu zanguu mieee oooh Michuzi ita ambulance mwenzio mbavu zimevunjikia kwenye blogu! Loooh kweli duniani kuna watu mwee!
ReplyDeleteumeshaenda kwa dentist kuangalia meno yako? Inawezekana kuna meno ambayo yapo sawa lakini hayakutakiwa kuwa hivyo. Kama umeanza siku za karibuni basi kuna meno yamesogea kama umeanza toka ulivyozaliwa basi hukupelekwa kwa dentisty ukiwa mdogo wakaangalia meno yako yanavyokua. Lazima kuna meno yako vibaya..au unainfections in the oral cavity.
ReplyDeleteand as for spitting while you talk, you might try slowing down a bit. You could be a little hyper or over excited about talking and you get ahead of yourself.
HAHAHA JAMANI MICHUZI UNA VISA WEWE ETI UMEANDIKA ANGALIA TUSIJE KUCHAFUA HALI YA HEWA HAHAH HUJAACHA TU MAMBO YAKO
ReplyDeleteMIE YANI HATA LA KUSEMA SINA JAMANI NIMECHEKA KW AJINSI ALIVYOANDIKA HAHAHA NA HUYO DADA ALIETAKA MSAADA WA MUME MHHH NAHCEKA TU HAPA HATA SINA USHAURI KWAKELI MICHUUUZI UKO JUU KAMA NDEGE ZA GADDDAFI HAHAHA
KIDUME NENDA HOSPITALI UKO MAJUU KWANI HAKUNA MADOCTA AU HUNA INSUARANCE HAHAHAH NENDA HOSPITALI .AU NJOO NIKUSINDIKIZE KWA BABU
YABINTY
umeshapata DAWA tayari, wasiliana nami nimetibu watu wenye maradhi kama yako na wamepona kabisa.Dawa yangu nilioteshwa miaka 5 iliyopita ila tu sipendi sana kuitangaza kwani ninaowatibu ndio watatangaza.
ReplyDeleteNipo kijiji cha Kirima Kidachini Kibosho km.4 toka Moshi Mjini uliza kwa Mzee Kitakita
Kweli huyu ana kiherehere, kama ana mshahara hata wa kumzidi JK iweje aulize kwenye blog tatizo ambalo huko alipo kuna hospitali waliobobea kwenye fani zao kwa nini asiende kujua tatizo lake na kupata matibabu? kama ni bahili sana basi hata nauli ya kuja Bongo kwa babu itamshinda???
ReplyDeleteanatuzengua huyu so unataka dawa za miti shamba au? magonjwa hayo huu nje ndo yanatibika fresh iweje utake kuazima jamvi msibani?
ReplyDelete