Align CenterSalamaleko Ankal Michuzi,

Naomba leo nije na mada hii ili wadau waweze changia maoni yao.

Naona sasa wengi wameamka na vile vile kujua kwanini wanaitwa walala hoi au maskini kwa sababu ya kupoteza Time kuangali mpira.

Karanga zitauzwa, mahindi yatalimwa na vilevile ofisini kazi zitafanyika na hope..

Ndio vipo vitu vingi vinavyofanya wanaume wawe kwenye mabaa mpaka saa nane usiku kila siku kisa mpira.
Lakini, ni lazima wote tutimize majukumu kwa familia zetu, wake zetu na vile vile girlfriends zetu sio kila saa mpira.

Sasa hapa ipo Kazi.. maana mada mpya inahusu negative effects.. (oPPS) MATATIZO .. yanayoletwa na kupoteza muda kwenye mabaa.

1) Pesa kuisha haraka
2) Kitambi
3) Kufa haraka
4) Kuibiwa simu
5) Wanawake wengi sana Bongo TZ wanatoka na wanaume wengine kwasababu wanaume wao wako kwenye bar au kushangaa mpira wa manchester. ( Mada ndio hii)

Kwanini nasema hivi.. ok

Unajua sisi wabeba maboksi kila tukitua Tanzania kutoka USA, UK AU PARIS tuko FULL kila dola na tumewiva sanaaa .. pamba kali..
Sasa wasichana wengi wa kibongo hata wale kwenye ndoa wanapenda sana watoroke na sisi kwani wanasema tupo different.

Hii inatokea sana, yaani demu yupo na rafiki wako ambaye ni boyfriend wake, lakini akipata muda tuu.. Demu anataka kutoka na mbeba box.

Wabeba maboksi wengi watakwambia, tukiwa TANZANIA kwenye vacation, wasichana wengi wanasema mimi nina boyfriend au Husband na wanataka kutoka na sisi vilevile. SIO WABEBA MABOKSI TU BALI NA WANAUME WENGINE AMBAO WAMEENDELEA KIUCHUMI..


Asilimia kubwa ya wabeba maboksi AU vijana wachapa kazi wakiwa Tanzania wanatoka na mpenzi wako wakati unacheck soka.
Sasa sijui kwanini? Ni swagger yetu au walalahoi wa Bongo hawajui mapenzi.

Wasichana wengi wakijua huyu jamaa ni wa Marekani, UK au Paris... basii boyfriend , mapenzi sahau.
Huyu mrembo atafanya juu chini amtoroke husband au boyfriend ili ale bata na mbeba boksi.

Hivi ni kwanini tunapendwa sana na wasichana wa kitanzania kiasi ambacho hawajali ndoa au WANAUME zao ...
Wanataka tuu kutupata jambo weekend. "Kiasi wanasema Nina boyfriend lakini sasa hatupo vizuri... "

Wengi wanapenda mavazi yetu, miili yetu ni safi na vilevile tumeshiba na afya. (HAMNA KITAMBI)

Cha msingi , wanapenda marashi ya Gucci na Polo..

Sasa mlalahoi anakesha kwenye soka, sisi tunapiga shoka kwa better half wake.

Kuna siku nilikua nimetulia White sands na demu mkali sana akaanza kuniambia bwana wake anamtesa, kumpiga na hata mapenzi hajui kabisa..

Sasa mimi naona tujadili hii mada.
Je ni kweli Wabeba maboksi wako romatic na wanavutia wasichana wa kitanzania zaidi ya wabongo wa hapo tanzania??

Na kwanini wanaume wengi (sio wote) wahajui jinsi ya kuspend time na wifey kazi kukaa bar peke na wanaume wezako.. we shoga?

Asante.. Michuzi hii inagusa sana lakini usiogope.

MKURUGEZI WA WABEBA MABOKSI

CALIFORNA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 59 mpaka sasa

  1. KWA TAARIFA YAKO WEWE NA HAO WABEBABOKSI WENZAKO AMBAO MNAFIKIRA FUPI KAMA ULIZO ZIANDIKA HUMU.MNATAKIWA MUWAHI LOLIONDO KWA BABU AMBI MKAPATE KIKOMBE,KWANI MADEMU WOTE HAO AMBAO MLIWABATUA WANA NGOMA (UKIMWI)NIYO MAANA WANAWAKIMBILIA NYIE AMBAO HAMJUI TAARIFA ZAO.HAWAFANYI MAPENZI NA WAUME ZAO KWANI TAYARI WAMEKWISHA ADHIRIKA NA NGOMA.UNGELIKUWA UNAAKILI USINGEWEKA MADA HII MBELE YA KADAMNASI NA KAMA NYINYI NI MASHUJAA ANDIKENI NA MAJINA YENU ILI TUWAPE ZAWADI YA KWA UJINGA MLIONAO WA KUNUNUA NGOMA KWA JASHO LENU LA KUBEBA MABOX
    MDAU

    ReplyDelete
  2. we we weeeeeeeee. Wape wape wape mtu wangu. Tena umenikumbusha mbali sana ulipotaja perfume ya Gucci. Mi ni wa kike na naona umeongea ukweli sana. Kiufupi umeweka mambo hadharani. Yani hata mie huwa najiuliza hawa men vp. Most of the time nkiwa online nachati na wakaka wa mamtoni wananipa rahaaa. Mara atume gift(Gucci perfume) na dollars za kununua bando za internet ili tu asikukose online. Men wa bongo wanaota vitambi age 27 yani tayari ashakuwa mvivu hata mambo flan anasweat hadi basi hata kaama kuna ac, ukimshauri aende gym mbishiiiiii anakimbilia kucheki mechi na kuongeza kitambi na marafiki zake. Sasa wakati huo huo unasikia kifaaa kiimeshuka kinanukia . Kwann usiende kupata advanture. Na nyie wa nje msijisifu sana huwa girls wanafata adventure tu. Muwe makini pia. UKIMWI UPO NA UNAUA.

    ReplyDelete
  3. Sikubaliani na wewe kwamba wanawake/wake za watu hapa bongo wanatoka na wabeba mabox kwa sababu ya kuangalia mpira. Inaonyesha dhahiri kwamba wengi wa wabeba mabox walikuwa wanawafahamu hao wanawake kabla ya kwenda huko waliko. Mchachofanya ni kuwarubuni tuu wake za watu, na hiyo siyo tabia nzuri na atakayekamatwa atafanyiwa kitu mbaya aende kuwahadhisia wengine na ndiyo itakuwa mwisho wa tabia zenu chafu.

    My few cents

    ReplyDelete
  4. Kaka ao madem wa ivyo wapo si tunaita selua wanapenda tu kula bata na wewe na of course lazima ajiweke katika mazingira ili uwe interested ndo anaanzia hapo mume wangu hivi au boyfriend wangu vile wako after your money. Najua mkitoka uko manua loaded mshajinyima sana kwaiyo vacation ya two weks au three weeks na dolari ulizosevu mwaka mzima lazima utatesa. Jaribu kukaa miezi mitatu ivi uone kama reception itakuwa the same everyday. utachoka watakukimbia. Lakini wapo madem wa maana apaapa bongo iyo tabia hawana hata utoke sehem gani ya dunia hawababaiki. Whitesands kwa taarifa yako wako madadapoa wanaokuja kudaka wazungu isjekuwa ndo umekutana na mmoja wapo! Kuchukuliwa mke au dem ni hulka mbaya ya huyo dem wala sio kwasababu ya kuangalia mpira baa wapo ambao wanaenda na waume au boyfriends wao mpirani au hata baa na sio siku zote watu wanashinda baa kuangalia mpira frequency kubwa iko wakati wa world cup, Kwaio kaka ukiona umepata dem kirahisi ivyo ujue ama umechukua changu maridadi au selua.

    ReplyDelete
  5. Wewe mtoa mada hii hakika akili yako ni fupi sana na sio uongo wahitajika kwenda Loliondo kuwahi kikombe cha Babu maana nyuma ya pazia unataka kujisifia kuwa nyie mlio nje ni bora zaidi ya walio bongo, pole yako! Kwa wanawake wengi siku hizi hawajali mapenzi, pesa mbele na sio kwa vile wewe ni mbeba box au laa...watambabakia hata kijana mchafu toka Mererani kwa vile tu ana mshiko. Ndugu yangu naomba ufahamu kwa kubabaikiwa na mademu wakati uko vacation sio sababu ya kuwa wewe uko nje ni kwa vile umewaonyesha kuwa una pesa. Kuweni kama wabeba maboksi wa Kenya, Rwanda, Uganda...listi ni ndefu ambao hutumia pesa zao kwa kuziendeleza familia zao na kijiji walichotoka na sio kutumia pesa kuhonga wanawake kama wewe mtoa mada!
    Hakuna uhusiano wowote wa kuangalia mpira na kutorokwa na wapenzi/wake wetu.

    ReplyDelete
  6. kaka hujatulia naona una mambo bado ya 80's kwamba ukitoka nje watu wanakupapatikia. mkuu hayo mambo ya polo na gucci zipo bongo kwa swala la pamba nazo zipo the only different huku bado hatuzipati kwa wingi kama nyie huko.na nauhakika soon mambo yatakuwa tambarare. wewe huko unaishi maisha ya stress sana na hauna mda wakutosha wa kula bata kama sisi huku ndio maana ukija huku likizo na vipesa vyako vya credit card unakuwa na mda wa kijinga wa kwenda kujirusha maana huko nauhakika hauna mda wa kujirusha. angalia na huko watu wasikugongee demu wako maana kila wakati wewe upo schedule kubeba mabox.

    ReplyDelete
  7. mchangia mada wa kwanza inaonekana ni mwanamke,point yake ni nzuri lakini tu ameongea kwa jazba lakini hata mimi (bila jazba) naungana nae kuwa most of hawa wanawake wana scandal mbaya za kimapenzi sasa unapotokea wee mbeba box ambae huna scandal zake yeye huwa ni mwenye amaani nakuona kuwa amepata men wa kuspend nae bila presure ,hilo moja lakini pia tukubali tukatae ni kwamba huku nje ya nchi tuliko ambako kuna good human resources management ni kwamba hakuna muda wa kupoteza kwa mambo ya kipuuzi so mtu unapokuwa tanzania kama ambavyo tunajua nchi yetu ilivyo kwamba mtu mmoja anafanyakzi na analisha na kuwapa huduma zingine watu kumi kwamba watu wako so idle kwahiyo tunapata ule muda wa kuwa free na kufanya mambo ya kipuuzi sana kuliko kutumia muda wako kwa mambo yako ya msingi kwahiyo suala la kutokuwa na shughuli yakufanya linachangia kwa wanawake hawa kufanya mabo haya mbona huku ughaibuni tuliko hakuna rate kubwa ya watu kuwa na mambo ya kipuuzi kama hayo ? kwakuwa tu watu wana mambo mengi ya msingi ya kufanya ikiwemo kazi ,kusoma na kadhalika

    ReplyDelete
  8. duh.. sasa hii kaZi. Kwanza mimi nin hasira sana na hawa wabeba maboksi wa ulaya na marekani. Kuna Girlfriend wangu alidanganyika na hawa watu. Jamaa alikua rafiki yangu na tulisoma wote sekondari. Sasa aliporudi kutoka Texas nilimkraribisha home kwa dinner.
    Yaaani demu wamgu kila mara anamtizama jamaa...mara oh napenda kofia yako, mara napenda raba.
    Mimi baada ya dinner.. jamaa akaondoka. Niligombana sana na girlfriend wangu. Tukaachana kesho yake..

    Nilikua Rose garden na check soccer..mara nikamwona ex girlfriend wangu na yule jamaa.

    Yaaani basi.. nilitaka nipige uwe lakini najua hamna haja.. Demu alidanganyika na jamaa..
    eti katoka marekani??
    Basi baada ya muda jamaa akarudi marekani na sasa anamtumia demu hela. mimi nilirikasika sana.
    Yaani mapenzi hakuna.. wasichana wa tanzania wengi wanatafuta hela

    ReplyDelete
  9. Mkurugezi wa Califona, kwa nini unatufanya wabeba boksi tuonekane mabwege hivyo? Ankal, pumba kama hizo tupa kapuni bwana!

    ReplyDelete
  10. PASUA BABA PASUA JIPU PWAA!

    Mimi ni mwanamke na wewe 110% wanaume wa kibongo hawana time na wake zao kama hakujitia overtime basi weekend atajitia yuko kazini kumbe yuko kwa kimada na tena jioni ndio usiseme hawarudi kuwapa tafu wake zao hawajui kucare kutwa mikelele eti wao head of household, head gani hata nyumbani huonekani?

    Wanawake siku hizi wala hawawapigizi kelele tena saa 1 tu inatosha mwanaume mwingine kukutimizia haja zako kisawasawa unasuuzwa vizuri machungu yote ya kuachwa peke yako yanaisha tena gemu la kuiba tamu si mchezo.

    Na tunaombea muendelee na mchezo huo huo, wewe ukila vya wenzio na vyako vitaliwa, habari ndio hiyo!

    ReplyDelete
  11. Sipingani na unachokisema , kwani kweli vitendo hivi vya kifisadi vinafanyika katika jamii mbali mbali duniani, sina data za kutosha kusema kwamba Tanzania wanendekeza tabia hiyo kuliko kwingineko.

    Ila kuna vitu vya msingi sikubaliani na wewe:

    1: Sidhani kama mada hii ulivyoiweka inaweza kuleta mjadala mzuri (There is agenda framing problem, and it distracts the audience by providing a biased view). Pamoja na mapungufu hayo mimi binafsi nahisi ni tatizo lilopo kwenye jamii na linapsawa kuongelewa , ila sijui kama liko kwenye platform sahihi

    2: Unaonekana kuwa unamaanisha kuwa wabeba maboxi mnajua sana mapenzi na mna mvuto sana. Sina uhakika na hili, nafikiri hapa umeshindwa kabisa kuelewa ukweli wa msingi. Tabia ya umalaya iko ndani ya mtu binafsi na hutofatiana kati ya mtu na mtu. Angalia sana usije kuta hata wewe mwenyewe hapo ulipo kuna garbage cleaner anatoa huduma kwa mke wako wakati uko kwenye kazi ya kubeba maboxi

    3: Sidhani kama nyie ni mhimu zaidi kuliko watu wengine , kwani historia inaonyesha kuwa kuna watu kama Lyumba walisemakana kutembea na utitili wa wanawake. Sidhani kama yeye ni mbeba maboxi wa USA,UK etc

    4: Kwa kifupi nilipoisoma hii insha yako inaonekana una shida ya kutojiamini , baada ya kubeba maboxi na kurudi nyumbani hukuamini kama ungebahitika kumpata uliyempata (inferiority complex)

    5: Ushauri wa bure , umepotea njia, chukua mda pekee yako , angalia ni wapi ulikoangoka , simama imara , beba maboxi vizuri kwa manufaa ya wazazi wako huko kijini waliko na familia yako.

    6: Historia ya umalaya na ufuska ilikuwepo toka kuumbwa kwa dunia , wala ulichokileza hakuna kipya.

    7: Mwisho, zingatia sana ushauri wa mdau aliyetoa comment za mwanzo i.e. anagalia usije ukawa unashabikia kuruka kutoka kwenye moto na kudumbukia kwenye kikaangio cha mafuta.

    MDAU Kutoka North America

    ReplyDelete
  12. Msibishe jamani.. wabeba box wanashobokewa sana bongo.

    ReplyDelete
  13. mtoa mada naona ni mtoto si rizki.njoo unguja ntakupeleka mpaka mombasa
    mambo ya gucci nini sijui unataka tupoteze muda kuchangia

    ReplyDelete
  14. huyo mtoa mada kweli ni mshamba,.hio ilikua zamanji enzi za mabaharia, either way, naona huko ulaya umeanza kuwa idle, recession imepunguza idadi ya mabox ya kubeba, rudi bongo

    ReplyDelete
  15. NunguNunguMarch 23, 2011

    Ankal michuzi sasa wewe unatuzingua na hizi topic zako za Kutunga wewe mwenyewe hapa mimi naona hakuna lolote hakuna mtu anayeleta hizi topic ni wewe mwenyewe unaziweka,Lengo lako ni nini?unataka kutugombanisha sisi wa ughaibuni na ndugu zetu bongo?ama umekosa ya kuweka? weka topic kama za babu wa Loliondo watu wajadili kama ni kweli ama ni mchanga wa macho? mambo ya Libya? na mengine mengi.
    ni hayo tu mithupu najua utaibani kwani nimekubaini ha ha ha ha
    Mdau Uk

    ReplyDelete
  16. Huyu Mtoa mada Hana akili nzuri....halafu amecomment tena kama mara tatu akijipalilia kama mtu mwingine.
    mi niko mamtoni maika 26 sasa na sifanyi ujinga huu.

    ReplyDelete
  17. Hahaaa that is true wanaume wakibongo hamna kitu kazi kuwause wanawake badala ya kuonyesha mapenzi. Big up mbeba box :-)

    ReplyDelete
  18. Sijawaahi soma mawazo yakijinga kiasi hiki muda mrefu kumba wajinga kama hawa bado wapo dunia hii bila shaka ubongo wamleta mada una walakini atakuwa alkiwahi kuumwa mtindio wa ubongo siku za nyuma
    ndio maana hao wabeba box wanishia kunanihiwa na kuva mijihereni alafu anasema wakija huku wana danki wake zawatu kumbe jamaa kwisnney.

    ReplyDelete
  19. hahahahahaaaa haluuu mana si halooo.watu jazba humu kasheshe.langu jicho.jamani nyinyi kitu kimoja hakuna haja ya chuki,mbeba box anatumia nguvuze na mkaa baa atumia helaze.acheni mambo yasiyokua na msingi.

    ReplyDelete
  20. Ni ujinga tu kudhani kwamba ukiwa nje basi ndio unapapatikiwa. Yaani mtoa mada uwezo wake wa kuelewa ni mdogo mno, kwa taarifa yako sisi hatuna stress huko na BONGO TAMBARARE. mademu wanataka hela tu, eti mpaka leo unazungumzia Gucci? Pole sana kwa akili yako fupi.

    ReplyDelete
  21. Wabeba maboksi zamani walikuwa wanaitwa mabaharia. Sasa kilichotokea hapo sikijui nini kilichofanya hayo mabadiliko. Hawa jamaa wameshawaliza watu wengi ambao waliokuwa na tamaa. Wenye tamaa za kuolewa, kuchukuliwa huko ughaibuni, n.k. Mbeba boksi wa ughaibuni anakula vizuri na kuvaa vizuri ukilinganisha na mfanyakazi wa kima cha chini bongo. Wabeba boksi wengi wa ughaibuni wanaishi kama bongo tu, nyumba moja mtu kibao, pengine chumba mtu nne. Ukitaka kuishi vizuri inabidi ufanye kazi masaa mengi, huo mpira pia utakushinda kuutizama maana unataka kulipiwa. Maduu wa ughaibuni pia na wanamikwala yao. Wanataka mtu atakayewapa creditcard au makaratasi ya kuishi. Hata akipata kuwa na uwezo huo ameshazeeka, mambo hayawezi tena baada ya miaka mingi ya maboksi. Maisha ya ughaibuni ni kutumiana tu, wewe unachokitu fulani na mimi nakitaka na wewe unataka kitu fulani na mimi ninacho basi. Maisha ni yale yale ukisoma sana utapata kazi mzuri popote pale duniani. Wezi na dadapoa wataendelea na kazi yao hiyo.

    ReplyDelete
  22. Duuuuh......! Kumbe kuna wabeba maboksi washamba kiasi hiki.....? Bongo ya sasa vijana wana shule na mkwanja wa kueleweka..... hizo pamba na perfume zote zipo bongo. wewe beba boksi mpaka ufe. ukija bongo na vidola vyako vya kuzuga hata mwezi haufiki umeishiwa unakimbia. Tuachie vijana wa mjini tunakimbiza january mpaka December full mkwanja. Ishu za kujisifu mademu za zamani sana mshikaji tena inawezekana hao ni machangu. Au ulifungwa ndio umetoka.....?

    ReplyDelete
  23. TEMBO DUMEMarch 23, 2011

    Hehehehehehehehe niache nicheke kwanza ndugu mtoa mada. Ingawa sikubaliani na yote uyasemayo, lakini bado nashindwa kujizuia kucheka.
    Mimi binafsi ni wa ughaibuni, na miongoni mwa mambo niliyojifunza huku ughaibuni ni nidhamu. Sijawahi kwenda bongo na kutembea na demu yoyote yule, achilia mbali demu/mke wa mtu. Ninapoenda bongo huwa sifanyi ngono nzembe kwa sababu huku nilipo ninaye demu wangu na siwezi kufanya mambo ambayo nisingependa yeye anifanyie mimi. Ingawa ni kweli, kila ninapotua bongo kuna videmu vingi tuu huwa vinajileta na vinanikabidhi kisu kisha vinalala chini na kuelekea kibla wenyewe, lakini huwa nakataa kuchinja. Ukikataa kumchinja ataanza kukuonyesha kwamba eti labda wewe siyo rijali, mwanamme gani anakataa kumuangusha mwanamke.
    Sasa hapo ndipo tunarudi palepale kwenye nidhamu, na nidhamu ni kujiheshimu wewe mwenyewe kwanza kisha kuwaheshimu wenzako. Niliondoka bongo kwa mara ya kwanza nikiwa na miaka 21 na sasa hivi nina miaka 32. Miaka 21 yangu ya bongo, sijawahi kushuhudia watu kuheshimu ndoa zao au mahusiano.
    Wakati nipo university mwaka wa kwanza, ndipo nikaanza kujifunza kwamba,...alaaaa...kumbe inawezekana mtu mmoja kuwa na mpenzi mmoja tuu...; Ingawa bongo hicho kitu nilikuwa sijawahi kukiona.

    Kwenye hili suala la kukaa sana baa na kumuacha mpenzi wako nyumbani peke yake, huu ni ujinga wako mwenyewe mwanamme, na kila kitakachotokea nyuma yako, basi umejitakia mwenyewe. Inakuwaje mtoto wa kiume unaacha familia yako nyumbani, halafu eti wewe unaangalia manchester united na rafiki zako? Wewe kunywa bia tuu, ndovu, serengeti, gold, lager, lakini ujue kwamba mpenzi wako machizi wanatafuna, na wakani wewe unashangilia Rooney kupiga bao wakati upo baa, basi ujue wakati huohuo kuna mchizi anapiga bao nyumbani kwako.

    ReplyDelete
  24. MICHUZI HII BLOG SASA INAGEUKA KWENDA KUBAYA RUDISHA HAZI YAKE JAMAA INAONESHA KABISA HAJAELIMIKA KWA USTAARABU, HATA CALIFORNIA ANAKOSEA KUANDIKA WAKATI NDIO YUPO HUKO? MWENYEWE UMEKAA UMEONA ULICHOKIANDIKA CHA MAANA KWELI... MNAJIVUNJIA HESHIMA TU INAONESHA WEWE SI MBEBA BOX NI ZUNGU LA UNGA TU HUNA LOLOTE. MSAFIRI

    ReplyDelete
  25. Akili zako ni timamu kweli? acha uwendawazimu!

    ReplyDelete
  26. Hiyo Mada unayoongea ni sawa ila mbona hata sisi wa bongo tukijaga huko tunawagongea sana madem/wake zenu? nyie hamlali saa zote mko kazini. Tena madem zenu wanatupenda sana tuliotoka huku.Na jinsi mlivyotawaliwa na tabia za kimagharibi basi ni mteremko tu.... Madem wa bongo hawa wababaikii nyie,... ukiona anakubabaikia huyo papa... Pole sana ndugu.

    ReplyDelete
  27. Mimi sielewi kwani kuna maada muhimu za kuchangia na hapa tunaongelea mapenzi. Hali ya watanzania wengi ni ngumu, nafikiri wakati huu ni muafaka kuchangia maada kuboresha hali ya uchumi wa nchi yetu ambayo kwa sasa inaenda mrama. Mimi nasikitishwa sana na hali ya maisha ya wengi kwani nchi imejaa rushwa, hakuna utawala wa sheria, umaskini umekithiri na hata elimu bora imekuwa kwa wachache.
    NIKIMKUMBUKA BABA WA TAIFA MACHOZI YANATOKA.

    ReplyDelete
  28. maisha ya utani yanawasumbua hao wabeba box. kwanza mkae mkijua huko ulaya hakuna uchaguzi yaani mtu ili mradi ana jinsia ya kike basi wanaume watakaba. sasa wakija bongo inakuwa ni ushamba maana madem wametulia wanaita yaani tafrani akilini. demu wa ulaya au states mara nyingi nae anakuwa resi so sio kila siku anajipamba lkn madem wa kibongo wana time ya saa zote kujipamba so hujui yupi wa ukweli yupi feki. kaka nakushauri kama mbeba boksi mwenzio kuwa makini sana sio ukimwimwi tu bali jasho lako madem wa kibongo majority ni gold diggers.
    MAISHA UTANI ndani ya holland

    ReplyDelete
  29. Man wa Rose garden stori yako ya kutengeneza...ushamba tu umewajaa wabeba boxi...ikiwa mkurugenzi wenu tu ndio huyu je nyie mkoje? Mna akili kweli?

    Kafanabo

    ReplyDelete
  30. jamani mambo yote wanaume wa kizungu, wanajua sana kulea familia na wake zao! mie niko na mzungu and got 3 kids, baada ya hapo nilikuwa na mbongo from my own village( uchagani) lol alikuw ahana la mahana hata, kazi kuwinda wasichana and kushida bar kuangalia mpira, so wadada wa kibongo tugeuze kabao lol

    ReplyDelete
  31. Wewe mtoa mada utakuwa unakutana na vicheche tu, msichana wa maana kwanza hanaga time na masharobaro wa kuvalia suruali matakoni na kofia, wasichana wa maana hawapo hivyo unavyoongelea wewe, akiamua kuwa na wewe hamuongelei mtu wake kabisa huyo ndio tabia yake na nia yake ni akuvute tu kwa wakati huo ujione wewe ndio mwanaume ila kiukweli hana mapenzi nawewe, acha kuwa mgeni wa wanawake wa bongo ukadhani akikusifia basi ndio sifa za kweli, waangalie wenzenu mliokuwa nao huko Texas (Othman na Jeshi)waliorudishwa na hawawezi kuja tena huko wananuka jasho huku hata hakuna mwanamke anayewatizama, huo ndio mfano hata wewe ukishaishiwa hela huku bongo unaonekana kinyesi tu!

    Acha ulimbukeni, mwanaume mjanja wala hawezi kusema maneno hayo kuhusu wanawake hata kidogo. Halafu kingine ujue hata hao mademu wenu mlionao huko wakija huku tunawala mbaya, na tena wanasema maneno hayo hayo kuwa hamuwaridhishi kimahaba sasa ndio ujue wanawake wa bongo wote ni mafia tu wanakwambia maneno mazuri ya kukupanga ujione wewe ndio shujaa wakupunge urudi zako huko uanze kukopa na kununua chakula madukani kwa card ha haa haaa.

    ReplyDelete
  32. Sasa nimemwelewa mbeba maboksi, kumbe yeye hobby yake kubwa ni ngono, sasa hataki wengine wawe na hobby tofauti, yeye anataka kila mtu awe na hobby kama yake. unasemea mpira tu, what about movies, music/ kama kweli ungekuwa sincere, ungezungumzia suala hata la vijana wa kibongo, ambao wamesomeshwa elimu ya mwanzo kwa gharama zetu, wengin empaka university, wana mikopo ambayo hawajalipa, wameishia kuwa vibaraka kwa kuishi marekani na kwingineko, kufanya kazi kwa nguvu kujenga marekani badala ya kujenga tanzania, tuambie umeinvest wapi kwa ajili ya TZ? kama si unafiki tu? kuishi marekani si ushamba na kuwa kibaraka, na kuwa mkataa kwenu? what's the difference? kwa nini usirudi hapa na kutumia u hardworking wako na resources ulizonazo, badala ya kuhonga usomeshe angalau watoto 20 ili wasaidie kwenye maendeleo ya nchi, badala ya kukemea ufisadi, na ngono nzembe, wewe unajisifia kwa kuhonga na kuwasakama watazama mpira. kwanza how many times a week tunaangalia? mostly at weekends, muda ule ule ambao ma sharobaro kama wewe mnajirusha na machangu.
    kwani muda unaotumia kujirusha na mademu wa marafiki zako, kwa nini usiproduce na wewe? kama baa kunapoteza hela, kwani kuhonga hakupotezi hela? Kama unachangia changia kwa issues ambazo ni productive oriented, na si reproductive oriented ( forgive my english, lugha ya tatu kwangu)!
    unawaambia watu wasome vitabu, we umeandika kipi ili tuwe wazalendo, au kusoma vitabu walivyoandika wazungu ni sawa! hata wewe huko marekani hutakiwi, lakini umengangania, na kwa akili yako unaona kuwa kunukia gucci and whatever ndio maendeleo?
    katika anga hizi za kupambana na UKIMWi na moral deterioration wewe bado unajisifia kwa kufanya ngono hovyo? Grow up please! Manchester UTD hoyee!

    ReplyDelete
  33. I'm afraid that America is changing our brothers to this extent. Man whatever you do, you do it because you made that choice.

    ReplyDelete
  34. Babu saafi saana pakaaaaa hao wala vumbi, mimi nakuambia viwanja maisha si mchezo yaani hata kama huna gari wala nyumba lakini maisha babkubwa lazima utawaka tu, halafu maisha sio pesa eti ohh wabeba boksi wamechoka huku bongo watu wanahela za kumwaga, hamna kitu, maisha ni huduma bora, kama afya, elimu, hali ya hewa safi kupumua sio vumbi tu, hivi vinakufanya kuwa na upeo wa intelijensia, sababu hakna ujinga wa kibongobongo, sasa ukirudi bongo mentality inakuwa tofauti wakati kukaa maskani ndio ujeshi au uwanaume, viwanja ni mashoga ndio wanakusanyika mahala pamoja bila kazi wala nini,kwenda bar au pub kama kundi wote wanaume mnaonekana mashoga, watu wanaenda na wake zao au girlfriend.

    ReplyDelete
  35. MSHESHIMIWA MICHUZI! MIMI NAFAIDI HII BLOG JA JAMII, LAKINI NISHAANZA KUONA UZITO KUITEMBELEA,NILIKUWA DAILY NA ITAMBELEA MARA MBILI MPAKA TATU. SIKUHIZI MARA INGINE SI ITEMBELEI WIKI NZIMA!! KWANINI? KWA UJUMBE KAMA HUU, KWANINI UTUJAZIE NAFASI YA BLOG NA MAONI AU USHAURI USIOKUWA NA KICHWA WALA MGUU? BORA HATA UTUEKEE MANDHARI (MAPICHA) YA BONGO TUTAFAIDI. HUYU JAMAA ANAONYESHA ALIKUWA BORED AKAJIANDIKIA TUU, NA WIKI ILIYOPITA ILIKUWA MHISHIMIWA TOKA CA AKAANDIKA UTUMBO HUMU, TENA MREFU TU! KAMA UNAKATAZA MATUSI YATAWAUDHI WATU KWENYE GLOB BASI JARIBU KUZUIA UTUMBO PIA. KILA NIKITEMBELEA LAZIMA NITAKUTA TOPIC ISIYOKUWA NA MAANA, NAUDHIKA PIA!! SI MATUSI TU YANALETA MAUDHI..HAYA MAUTUMBO NI ZAIDI YA MATUSI! CHUKULIA UNASAFIRI KWA BASI KWENYE KWENU (MAHENGE) KITI CHA PILI NI HUYU JAMAA, ATAKULETEA STORY KAMA HIZI MPAKA UFIKE, SI UTAMUUA? UTUMBO HUU KAKA MICHUZI! TAFADHALI TUWEKEE MAMBO YA MAANA SI KAMA TVZ ENZI ZILE;) UNAJUA NASEMA NINI, EENH?

    ReplyDelete
  36. dah watanzania taaaabu kwelikwel yaaani badala ya kurudi kwenda kuwasaidia bibi zako huko mchuchuma majita rukwa na kwingineko ambako wanashea maji ya mtoni na wanyama wengine we unahangaika na wake za watu town afu unakuja kujisifia,acha ushamba kka pafyum ya gucci kitu gani au haitoki mwilini throughout fanya vitu vya maendeleo afu kaka michuzi thread kama hizi za watu wenye fikra zisizo endeleza taifa uwe unazikata juu kwa juu sasa hvi watu wanazungumzia Diaspora and African development,how Africans abroad can transfer capital nikimaanisha human and financial capital kwa maendeleo ya waafrika wote,afu we dada uliechangia sio kabisa yaani kununuliwa bandwith ndo na gucci pafyum ndo unamsaliti mwenzako daaaaaah kazi ipoooo!

    ReplyDelete
  37. huyu mjomba inaelekea pia hata shule haimo kichwani,na kama kasoma hajaelimika pia,maana kwa haraka tu NIDHAMU kwake inaoneka kapata F.
    huwezi kujisifia kuwa wewe ni kiboko wa ngono ukienda bongo unaifanya sana, hii inakuonyesha unakua mwili tu akili bado imelala.
    anyway kama zimo kichwani mkuu panga mipango yako na ukienda bongo utakuta unaishughulikia hata muda wa ku buzz na machangu hutaupata. lakini kama ndo wale kina yakhe ambao ukivikusanya kwa kuhenya unakwenda kuvitumbua kwa kujinunulia kimdudu,muda si mrefu tutakusikia nawe unakimbilia loliondo,ilimradi tu usichelewe.

    ReplyDelete
  38. Je umewahi kusikia maafa yaliyonisibu nilipokuja Bongo kunyoosha mgongo baada ya kubeba maboksi kwa miaka?
    Nilikaa bar moja, jina kapuni,akaja kisura, pande la binadam, akaanza kuisifu pamba yangu etc,to cut the long story short, she discovered I was sort of dull,melancholic. Akaota makucha na kuanza kunichambua. Nina hakika kabisa nilikuwa na uturi wa aftashevu, lakini jamaa akaniambia nanuka sabuni ya punda.

    ReplyDelete
  39. cku ile ulipotoa mada ya mambo ya soka la ulaya nlikuona wa maana lakin leo kwa hli nimekushusha "P" kabisaaaaaaa, wewe kama ulishobokewa na wanawake wachache huko ndo una generalize kwa wote....hvi unafkiri ni kila mwanamke anatetemekea hvo vichenchi vyenu mnavyorudi navyo????? bwana cku hzi kila mtu anajua kuitafuta hela ati, na ndo maana tunapewa nafasi kwani tunaweza.... hii mada yako ya leo for real haiko gender sentive kabisaaaaaaa. Habar gani kuhusu wanaume wanaowatetemekea na kuwashobokea wanawake wanaotoka abroad ili watumie chenchi walizorud nazo??? Na kwa taarifa yako hao waliokushobokea walikuwa kikaz zaidi kwani kazi yao ni kukuchuna hzo chench zako na zikiisha wanakuacha solemba wanachuna mwingine.Ukitaka kuthibitisha hlo hebu jaribu kukaa miez kama sita hvi bila kutuma chochote uone kama atapendwa mtu hapo. Cku ingine ufikirie kwanza kabla ya kuweka mada zako.

    ReplyDelete
  40. Ukweli unauma. Siyo bongo tuu! Africa nzima inabidi tubadilishe mawazo kuhusu maisha ya ndoa kuwa kina mama ni wa kufanya professional jobs + kucare nyumba + watotot. Mama akimaliza kazi mbio anawahi kurudi nyumbani kuwahudumia watoto. Kina baba walioko africa wanakimbilia nyumba ndogo na Bar. Njooni huku muwaone wakina baba wakiafrica wanavyofanya hakuna housegirl au houseboy nyie wawili ndiyo mtajipanga kuwatunza watoto. Kila mtu akifunga ofisi mbio kuwachukua watoto shule au kwa yaya maana usipowachukua ontime utalipishwa dola au mapound mengi tuu. Kila mtu anakimbia nyumbani. Mama anapika na kupanga meza baba anosha vyombo na kutoa vyombo. Baada ya hapo tena ma-homework yanasubiri, huku hata vidudu wanahomework. Subutu ukimbilie bar utajikuta kizimbani next day. Hii system lazima ihamishiwe bongo.Wanasheria jamani mnafanya nini? Family laws ziko wapi? Maana ni lazima kila mzazi ashiriki 100% kwa malezi ya watoto siyo kuwaachia ma-housegirl na wao wanafanya wanavyoweza. Hii mada ni nzuri sana na nadhani wanaume walioko aferica watajifunza kuwastarehesha wake zao na si kuwaacha nyumbani. Sisi (mimi na mume wangu) tunapanga siku gani tunatoka hivyo tunawapeleka watoto kwa ndugu (dada au kaka) then tunajirusha na wao wakitaka kujirusha wanatuletea wakwao. Then tunapanga family out na watoto. Huko bongo watoto wengi hata soda hawajawahi kuinywea hotelini! KINA KAKA PENDENI WAKE ZENU!

    ReplyDelete
  41. mimi ni mwanamke bongo nimeolewa na mume wangu anamshiko mzuri sana yaani napata kila kitu, ila mume wangu kurudi nyumbani saa nane, tisa ucku, nakuwa boared kishenzi nakaa tu nawafanyakazi, nipo online na wabeba box all time napata romantic zao, sio kama nataka pesa zao kwani mimi pesa sio issue ila wakitua bongo natoka nao coz they me me happy. wanaume zetu wa bongo achane tabia za kwenda baa bila wake zenu, wake zene sio furniture kuwa sinawekwa living room. asante mbeba box kwa mada hii nzuri sana.

    ReplyDelete
  42. acheni kumshambulia mbeba box.katoa changamoto kwa wala vumbi kufanya kazi kwa bidii na kurudi nyumbani kuhudumia familia zao. wengi wenu mnaenda kwa vimada immediately after work kama sio bar! kama mnabisha tutaweka majina yenu hadharani..kula tano mbeba box.kwi kwi kwi

    ReplyDelete
  43. Kumbe unataka ngono ngonoka ukija mchukue demu wangu niukufanye kitu mbaya, na picha ntakupiga nawenzio Cali ntawapa.
    Njoo bongo watu wanapiga pesa sa EPA ambazo wewe utabeba boxi millioni huzioni.

    ReplyDelete
  44. Pole sana ndugu mbeba box wa US, ila mi naona wanachokifanya wanaume wenzetu wa kibongo ndio hicho ambacho wewe ulienda kufanya ukiwa hiyo vocation yako, coz uliendakushinda na wake za watu W Sands, so hapo kuna tofauti gani na anaeshinda bar na wanawake wengine au kwenye Mpira?
    Kazi na umri bro inaelekea ushabeba box sana na imefika wakati wa kupumzika coz umechoka mwlili mpaka akili ya kufilia, Sitki kuamini kama wabeba box wote tuna akili kama zako za kupaka marashi na kuchukua demu wa mshikaji wako kisa tu jamaa wako anakitambi,,,,,,weka maada zilizoenda shule mbba box

    ReplyDelete
  45. Kwanza napenda Kumpoa BIG 5 mkurugenzi wa Wabeba Mabox,
    Unajua Michuzi hii mada iko serious sana japo wanachi walio bongo wataipinga sana.
    Kaka michuzi ni lazima watu waspend time na familia zao. kama ni kuangaklia manchester waambie waambatane na wenzi wao. Michuzi mimi nakupa ukweli hili nimeliona sana nikiwa vekesheni tanzania baada ya kubeba mabox huku ughaibuni,
    Michuzi mimi nawaonya sana wabongo kukaa idle na mamipira tuu. Nakubaliana kabisa kuwa hii tabia ya wanaume kukimbia familia kisa manchester na liverpool wataendelea kuibiwa wake zao tuu,
    Hata wewe Misupu uwe makini sana uwe unatulia nyumbani na mamsapu wako siyo kila siku uko kwenye sijui white party, sijui nini vile..

    Mjadala uendelee

    ReplyDelete
  46. uncle, wewe umesahau kiswahili nini? embu andika MKURUGENZI vizuri ,sio MKURUGEZI..!

    ReplyDelete
  47. Kaka ametoa maoni yake lakini hawezi kuwakilisha watu wote ambao wako nje ya nchi. Mimi nikiwa mwanamke ambaye niko chuoni hapa MSU nimekutana na ndugu zangu na watanzania ambao wanaheshima sana na wanakwenda shule, kufanya kazi ili kujiendelza kimaisha na kuweza kusaidia nyumbani Tanzania siku moja. Tukikutana tunabadilishana mawazo jinsi ya maisha yanavyokwenda. Tafadhali mtoa maoni, jiwakilishe peke yako kwa kuwa uko minority kwa uwezo wa fikra zako. Usiwatuhumu ndugu zetu nyumbani kwani ni wafanya kazi wa hali na mali, wamesoma na tunashukuru kwamba wanaendeleza nchi yetu mpaka tukirudi tunaweza enjoy. jaribu kuwasiliana na watu wenye fikra tofauti na zako unaweza benefit na kubalisha mwenenndo wako. Si jambo la kujivunia kuchukua wanawake wa watu, na si ajabu huna date huku Marekani yangu ni hayo.

    ReplyDelete
  48. umekoswa kazi ya kufanya. kama ungekuwa na kazi ya kufanya usingekuwa na muda wa kufikiria utumbo kama huu. naomba kusema kwamba huyu anaejiita mwenyekiti anaongea kwa niaba yake mwenyewe na kwa ajili ya kuchafua vijana wengine wanaoishi nje.

    ReplyDelete
  49. Poleni sana wabeba maboksi wote pamoja na mkurugenzi wenu,kuna watu wamekaa ulaya na marekani kifaida zaidi kwa maana ya kupata elimu nzuri zaidi na wamerudi na wana vitengo vya ukweli zaidi na bado wana utu na ubinadamu si anachozungumzia huyo mkurugenzi. Jamaa hana akili hata moja. Huyu alizungumzia kupoteza kwa muda sasa hivi anapoteza mud mwingi kutunga story za ujinga na uwongo. Gucci nn wewe fala wakati watu hatununui bali tunaagiza chizi wewe na tunaweza kukubebesha maboksi hata hapa coz ninachopata wewe unapata hata kwa miezi 6.
    Cha msingi waheshimu waliopo nyumbani kama wanavyokuheshimu, wa2 tushakaa nje zaidi ya miaka 10, na watoto wa bongo wanakuja kila mwaka kutumia pesa us na ulaya unaongea nn wewe?mbona mshamba sana? Hukuwahi kufikiri na kidogo sana na unachopata sasa ndo maana una dharau za kijinga,jua tu kuna vijana wa bongo wanasomesha wadogo zao ulaya na kila mwaka wanawatumia nauli kuja tz na hawabebi boksi bali wanatumiwa pesa za matumizi ili wasipoteze muda wa maboksi bali wasome.

    ReplyDelete
  50. Bwana michuzi, mimi binafsi nineipenda hii mada ingawa sizikubali hoja za mkurugenzi wa wabeba boksi. Aliyoyasema yamechanganyika mchele pamoja na pumba, kwa hiyo ni kazi ya msomaji kuchambua mchele upi na pumba zipi. Kwa hiyo basi, tafadhali, uamuzi wa kwamba mada itundikwe au itiwe kapuni uendelee kubakia wako, na wewe pekee ndiwe uwe na uamuzi huo. Achana na wanaosema...."oooh mada kama hii haina maana, itiwe kapuni, tujadili jinsi ya ku-transfer human capital"... n.k.

    Haiwezekani mada moja ikawa na maana kwa kila mtu, kwa sababu nina hakika wapo watu ambao hawaoni umuhimu wa mada ya "ku-transfer human capital". Ingawa hiyo haiifanyi mada hiyo isiwe muhimu kwa wengine.
    Hii mada ya mkurugenzi wa wabeba box, ni tatizo la kimsingi sana kwa jamii, na linasababisha watoto kuwa na makuzi yasiyokuwa na baba. (fatherlessness). Kama baba yako anarudi nyumbani saa 8 usiku kila siku ni sawa na kutokuwa na baba.

    Nakutakia kazi njema anko, lakini kama ninavyokuomba, uamuzi wa mwisho uendelee kubaki kwako.

    ReplyDelete
  51. Mtoa maada amechanganya mambo ila kuna mengine ni point. Kwa kweli tabia ya wanaume kushinda bar inachangia sana wanawake kuwa na vidumu sijuhi vibajaji. Si wanaume mnajitia nyie ndo marketable sana, mwanaume mmoja vimada sita alafu mnasingizia nilikuwa naangalia Manchester. Sasa na sie tunajibu mapigo. Hatutafuti pesa nje ila ni penzi mnalo tunyima. Kama ni ukimwi tutafute wote. Mtaisoma namba. Michuzi hii mada iweke front page ili ijadiliwe upya kesho. Ni muhimu kurekebishana tabia

    ReplyDelete
  52. NAONA MADA HII IMEKUA KALI SANA. Michuzi inabidi upate Bodyguard.

    Lakini hii mada imefanya watu wengi wa comment na vile vile wawe na umakini. Nafikiri mkurugenzi wa Wabeba Maboksi ametaka kufikisha ujumbe kwa kutumia style nzuri sana. Ujumbe wake ni hivi

    1) Usipoteze muda , jenga taifa na familia yako

    2) Mpende mke wako na haswa jipende wewe mwenyewe na maana ya hii ni mazoezi, achana na beer kila siku na vile vile chukua muda ukae na familia yako.

    Sasa kwa kutumia Propaganda na stories.. Mkurugenzi ameweza kuwakamata kimawazo na vilevile proof ipo kwenye comment.

    Katika posti zote za michuzi, Mkurugenzi amepata comment nyingi sana.. Usiseme ujaguswa.. mimi nimekuguswa na vilevile nitabadilika.

    KWELI TUMEZIDI.. BAR TUPO KILA SIKU KAMA MASHOGA.

    MAREKANI UKIONA BAR INA WANAUME WATUPU NI BAR YA MASHOGA.. TANZANIA NI BAR YA KAWAIDA.

    KWELI WEWE MLALAHOI NA MTANZANIA NI MASIKINI WA KUTUPA SANA.. KINYUMBA CHAKO NA KAGARI CHAKO AMBACHO NI USED KUTOKA JAPAN NI MAVI.

    ETI PRADO..AU CHASER?? THAT'S NIL.. NOTHING..

    Focus kuweka hadhi na heshima kwenye ndoa na familia yako.

    Achana na kukesha bar.

    MADA NI NZURI.. ELIMU IPO KWENYE HADHITHI..UJUMBE UMEFIKA..

    KAMA FATAKI.. INACHEKESHA LAKINI KUNA UJUMBE.

    ReplyDelete
  53. ANKAL ANKAL MICHUZI.. YAANI HII MADA IMENIGUSA SAAAANAAA.
    Mimi nimeolewa january siwezi kutaja siku kwani mume wangu anapenda kusoma blog yako.

    SASA hivi hayupo nyumbani.. toka asubuhi atoke yeye hajarudi. Sasa hatasimu yake huwa apokei kisa kelele nyingi bar. Kuna mechi.

    Kinachoshagaza ni hili.. hapa kwetu nimeweka dstv na beer zipo kwenye friji. Lakini yeye anasema lazima awe na marafiki zake..

    Najuta sana hii ndoa sijui kama tutafika.. naogopa kila siku tukifanya mapenzi atanipa ukimwi.

    Mungu wangu Mungu wangu sijui nifanye nini?????

    Mada hii imenifanya nitoe machozi kabisa maana hili ndilo jambo linanitesa sana kwenye ndoa yetu.

    MIMI NI MSICHANA MZURI, SINA MTOTO, NIMESOMA NA NINA MASTERS NA KAZI SAFI..

    KWA MWEZI NAPATA MILIONI 5 MSHAHARA .. Lakini sina mtu anayenituliza kimapenzi.

    Nifanye nini? Nafikiria sana niachane nae lakini familia itaona mimi kichaa.. Hasa baba na mama yangu..

    Nao vilevile ni matajiri.. lakini baba yangu mambo yake yaleyale..

    Wanaume badilikeni.

    Kuna rafiki yangu wa zamani yupo marekani.. huwa tuna chat sana.. yeye yupo tafauti na maneno yake ni matamu wakati wote.
    Natamani sana ni cheat lakini mimi ni mke mwema.

    Mwenzi ujao naenda marekani kusomea mambo fulani kwa kampuni nayofanyia kazi(kwa muda) nafirikiri NITATOKA NA MBEBA MOBKSI WANGU WA NEWYORK.

    NAOGOPA SANA LAKINI SINA NJIA, WOTE TUTAKUWEPO KARIBU NA NAJUA TU NITALAINIKA. MAANA WIKI ZINAPITA MIMI MKAVU.

    WADAU NIFANYEJE?
    Mume wangu tayari kitambi kimetoka na tayari yuko hoi dakika mbili uwanjani.
    Mbeba boksi wangu yeye ni gym kila siku na yupo fit.
    I love that. mwa..
    Mada safi michuzi. Asante kwa kuwa hodari.. nikikuona Regency au Nyumbani Lounge drinks on me

    ReplyDelete
  54. wapingao mada hii ,wengiwao ni wanaume wenye matumbo makubwa au vitambi,
    kwasisi wanawake tulio kwenye ndoa tunaumia na hii swala.
    wanaume wengi ni wabinafsi na wao ndio chanzo kikubwa cha kuleta magonjwa nyumbani,tena huko kwenye mabar,hafuati tu mpira.

    ReplyDelete
  55. NAUHAKIKA KABISA MTOA MADA HANA ELIMU KABISA! MAMBO YA AMERICA, EUROPE N.K ILIKUWA ZAMANI SIKU HIZI TUNAKWENDA VACATION TU. M BEBA BOX FANYA VIIU VYA MAANA KWA WAZEE WAKO NA SIO KUKAA WHITESANDS, WHITESANDS KITU GANI BWANA HATA MIE TU NAISHI KWANGU AMBAKO NI KUZURI NAKUNAFACILITIES NZURI KULIKO HAPO WHITE SANDS. WABEBA BOX MUELIMIKE WEKEZENI NYUMBANI UMRI UNAKWENDA MTAZEEKA TUONE KA HATA HAO WANAWAKE MTAWAWEZA PIA HATA HIZO BOX KA MTABEBA MTAKUFA MASKINI! KUKAA MAREKANI SIO ISSUE ISSUE KUWA NA VITEGA UCHUMI MASKINI WA ROHO NA AKILI NYIE.KWA MTU MWENYE AKILI HAWEZI JIVUNIA NGUO AU PERFUME HUO NI USICHANA WA HALI YA JUU!!!!!

    ReplyDelete
  56. Na nyie wanawake mnalalamika sana mara nyingi huwa mnalalamika kuwa mmechoka! Na hiyo ndio sababu inawafanya wanaume waangalie alternatives! Ila mtoa mada bado yuko nyuma hajaelimika ingawa ana exposure ya kutosha maisha ni popote haijalishi ni wapi na nguo kila mahali siku hizi zinafika na zote zinatoka hapo china sio mbali so wadau msitishike na nguo angetembea tembea hapa bongo angekutana nazo nyingi tu wachina wanaleta quality ile ile tofauti wao wananunua kwa dollar ama Euro na hapa kwa Tshs. Exposure haijamsaidia!!!!!

    ReplyDelete
  57. Duh

    Mi nadhani tabia ya umalaya ipo moyoni kwa mwanamke au mwanamunme, yule anayetongoza mke wa mtu ni malaya na mke anayekubali ni malaya, wapo wajane ambao wamebaki hivyo mpaka uzee, ni kwa sababu tu hawakuzaliwa malaya, na wapo wanawake ambao wana pepo la ngono na tunawaona, hata mumwewe afanyaje atatoka tu, na ni waongo sana, mara oh, mume wangu hanifikishi, unajua sana, kumbe anatafuta namna ya kukuibia, anascreem kabisa na kuvunga eti umemfikisha...wizi mtupu

    ReplyDelete
  58. UPUUUZI MTUPU HUU! SITAKI KUAMININ KAMA ULICHO KIANDIKA HAPA NDICHO UNACHO KIAMINI, KAMA NDIVYO HIVYO WEWE NI MPUMBAMBAVU KULIKO MTU YOYOTE DUNIANI, KATIKA DUNIA YA SASA KUWA NA MAWAZO KAMA YAKO BORA UFE TU, VIJANA WENGI SASA TUNAKWENDA HUKO MAREKANI KAMA VACATION NA SIO KULILIA KUISHI HUKO KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI NA KWA TAARIFA YAKO MADEMU WENU WA HUKO WANATUSHANGAA SANA TUNAWEZAJE KUJA HUKO NA KURUDI NYUMBANI TENA VACATION WANAWAPONDA NYIE MNAOSHINDWA KURUDI NYUMBANI NA WANATAKA KUOLEWA NASI BYTHEWAY HIVI HIZO HELA ZENU ZA KUJINYIMA MKIJA BONGO MNAKAA WEEK MOJA ZIMEISHA MNAANZA KUKOPA OOH NIKIFIKA MAREKANI NITAKUTUMIA KUMBE NDIO MNANAVYOZITUMIA NA MACHANGU POLENI SANA

    ReplyDelete
  59. Tembo Dume umenifurahisha saaaaaaaaaaaaana. Sina sababu ya kusema mi niko wapi ila ukisoma hizi comment utaona jinsi wanaume wakibongo wanavyochachawa kusikia kuwa mademu zao wanabanjuliwa na wabeba box. Wabongo mkatae msikatae mkubali msikubali mademu wenu wataendelea kubanjuliwa na wabeba box kwa kuwa wanajali si sababu ya GUCCI hiyo perfum ametoa tu kama mfano nyie endeleeni kuwatch hizo gemu za manchester watu wala raha hahahahahahaha. Mbaya zaidi mademu zenu wanajua kuwa hao ni wabeba box na wafuta mavi ila wana kisu na wanajali na kujua mapenzi watu weeeeeeweeee wabeba box oyeeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...