kaka yangu issa michuzi kwanza ningependa kuanza na shikamoo.

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa Globu ya Jamii kwa kusoma taarifa na matukio mbalimbali duniani.Dhumini langu hasa la barua hii ni kuhusu matatizo yetu hapa UDOM college ya mawasiliano.

Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili college ya mawasiliano yaani (college of informatics and virtual education CIVE) na ninachukua degree ya uinjinia wa mawasiliano yaani B.sC in Telecommunication engineering.

Kaka michuzi college haina maabara ya maswala ya uinjinia yaani mpaka sasa hivi sijashika kifaa chochote kinachohusiana nauinjinia, ila mimi naamini kwa kasi hii ya majengo basi wange tutengenezea maabara ya muda mfupi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Pili college yetu haina walimu wa kutosha na wazoefu katika kutufundisha hasa sisi wanafunzi wa injinia yaani tunategemea walimu toka UDSM waje kutufundisha yaani part time na part time yenyewe ni ya wiki mbili.

Kaka yangu fikiria mwenyewe part time ya wiki mbili unaweza kumtengeneza injinia wa ukweli hapo naamini tutakuwa tunadanganyana na mpaka sasa hivi masomo matatu kati ya saba hayana walimu natun ategemea walimu toka UDSM waje kutufundisha.

Tatu mpaka sasa hivi hapa hamna mwanafunzi yeyote aliyelipwa ela ya special fuculty ingawa tulisaini katika form za bodi ya mikopo tunazungushwa yaani wanatuona kama watoto wadogo.

Mpaka nimefikia hatua ya kukuandikia barua hii inauma sana kwani dunia ya sasa ni ya ushindani ili niweze kushindana basi natakiwa kusoma katika mazingira yakiushindani nasi kama haya ninayo sasa hivi, katika maisha yangu nilikuwa na dream ya kuja kuwa super injinia lakini kwa elimu hii ya UDOM sitofika popote.

Yani inafikia hatua tunaitwa mainjinia slide (sumarry zinazotumika kwenye lecture). Najua blog yako ina watazamaji wengi na ndio maaana naamini kama ukionyesha barua hii kwanamna moja au nyingine itatusaidia.
Ni mimi mdogo wako jose

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Wewe kijana acha kelele. University watu wanajisomea wenyewe, hapo sio sekondari. Tena sikuhizi kuna hiyo virtual education, nenda ocw.mit.edu ukapate elimu ya kweli. Lecturer yupo pale kukupa mtihani tu. Ndio maana PhD za bongo hazivumbui kitu, wote wakiipata tu wanakimbilia siasa. Wanaishia kubomoa nyumba za walalahoi. Amkeni vijana, kama mpaka leo uko chuo na unategemea mwalim basi umasikini hautaondoka.

    ReplyDelete
  2. Jose

    Let me put this way, this is a nation distaster, 10 yrs down the road sijui Tanzania itakuwa na wasomi wa namna gani?

    Na hapo bado, mchezo utaanza kunoga pale nyie mtakapo hitimu na kuingia kwenye system na kuwa walimu and guess what? Have you ever wondered baada ya miaka yako 4 hapo UDOM unatoka na kuwa mwalimu hapo hapo kufundisha products za Sekondari za kata???? Cha kusikitisha sana na kuwa sina hata uhakika kama serikali na wahusika wanaiona hii hali. Na hii East African Community nakuhakikishia miaka michac ijayo watanzania tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu,wa std unayoisema na std hii ya sekondari za kata sidhani kama watanzania wanaweza kuhimili ushindani

    ReplyDelete
  3. Kwa tunakoelekea sasa Mafunzo ya Sayansi ngazi ya chuo yanakua ni ya nadharia zaidi kitu kinachofanya kazi ya ajira au hata kujiajiri kua ngumu sana utakapoingia katika soko. Mimi nimehitimu UDOM mwaka jana ila nimekua nikitumia Video Training kutoka Marekani, zinauzwa na jamaa flani wa GreatDesign (www.greatdesign.co.tz), zimenifanya niwe katika real lab na ninamudu kufanya kazi zangu fresh sasa, kwa sababu zimetengenezwa katika Vitendo zaidi na Professionals. Ni nzuri sana even katika On Job Training.

    ReplyDelete
  4. Naomba kukujibu Anonymous wa kwanza,

    Masomo ya Technology siyo sawa na masomo ya longolongo kama political scince, economics, accounts, law na mengineyo kama hayo. Masomo ya Technology yanahitaji technical practicals ambazo kama huyu mwanafunzi hakupewa, basi nakwambia kamwe hawezi kuja ku-achieve anachotakiwa ku-achieve. Nakupa mfano mdogo tu; wanafunzi wanaosoma masomo ya Arts na Biashara kwenye secondary schools umeshawahi kuona wakiwa na maabara? Je umeshaona wakidai kuwa na maabara? sasa huyu mwanafunzi anayesoma Chemical Engineering, do u think kwamba ataweza kufanya mchanganyiko mzuri wa chemicals ili uje kupata wewe mtumiaji wa mwisho? By the time anapewa chance hiyo akiwa kazini basi atakuwa anafanya experiment! Guess what? By the moment we unapata hiyo chemical unakuwa ni specimen consumer na hivyo inaweza kukudhuru. Angalia mitaala ya wenzetu nje ya nchi, masomo yote yanayohusiana na technology yana-practicals za kutosha, na ndo maana wanakuwa competent na hivyo wanaweza ku-competent successfully kwenye soko letu la ajira wakati wale wanaosoma hapa wanabaki kubong'aa tu!

    Mimi ni mtaalamu wa ICT nimeisha-attend course kadhaa ambazo zinatolewa kwenye institutions zetu hapa kama vile UCC n.k. Believe me, hizi institutions ni chache sana zenye utamaduni wa kutoa practicals na hivyo basi course zao mara nyingi zinakuwa shallow. Nili-attend the same course in India na hapo ndo nilipofunguka macho kwa vile niliweza kupatana na international certication yangu ambayo iliambatana na practicals za kutosha ambazo zinanisaidia katika kazi zangu sasa. Mimi nilisoma masomo yangu ya Degree katika chuo kimoja maarufu hapa Tanzania katika experince yangu, tumekwisha wahi kumwondoa Dean of Students kwa vile alikuwa ha-support practicals kwa ubahili tu! Lakini baada ya kupigana sana, tulifanikiwa kupewa practicals za kutosha kwa vile Director wa ICT Directorate alikuwa akitu-support.

    Kama haitoshi hivi karibuni nimekuwa nikipokea wanafunzi wa field hapa ofisini kwangu, but most of them they know the theory part of the discpline, na ukiwauliza wanakujib kuwa hawana practicals chuo. Kama tuna nia ya kuelekea kwenye East African Community effectively, basi concern ya mwanafunzi huyu wa Telecommunication wa UDOM inabidi tuiangalie kwa makini na kui-support for the way forward. kwa sababu kama siyo mdogo wako wewe basi huyo ni mdogo wake yule ambaye kesho atashindwa ku-compete kwenye ajira na hivyo atakuwa jobless while Wakenya/Wauganda watapata ajira hiyo hiyo, hivyo ataendelea kuwa ombaomba. Fikiria pia juu ya wadogo zako wanaokuja, watoto wako na wajukuu zako, naomba kwenye hii forum tusiwe tuna-ROPOKA toa mchango na kama hauna hoja ya msingi ni bora ukakaa kimya. NO RIGHT TO SPEAK WITHOUT RESEARCHING

    ReplyDelete
  5. Anony 12:32
    Suala la mtu kujisomea mwenyewe lipo, lakini kumbuka jamaa angeongelea suala la technolgy.Huwezi kuwa injinia kwa kusoma vitabu peke yake au kwa kuangalia training video. Unahitajika kuingia maabara kwa ajili ya kucheck theories na kudizain.Kwa hiyo jamaa ameongea ukweli mtupu.
    Lakini kwa level ya bongo, hiyo inatosha kwa sababu nchi haidizaini wala kutengeneza kitu chochote chenye akili kama computer, camera, calculator or micro controllers.
    Wewe soma tu, practical utajifunzia kazini.Angalia hata magraduate wengi wa vyuo vyetu vya bongo hasa upande wa technology ni watupu kiasi kwamba hawawezi kucomptete kimataifa.
    Thanks

    ReplyDelete
  6. its true jaman hapa UDOM-CIVE tunasoma kinadharia..tumesoma Networking but till now kuna wanafunzi hawajui hata hiyo SWITCH inafananaje..its true kwamba juhudi za mwanafunzi ni muhimu but mwalimu yupo ili kumwonyesha mwanafunzi aweke hizo juhudi zake wapi. Mimi ningeomba wahusika walichukulie jambo hili kwa mtazamo wa kina maana tunakoelekea taifa letu litaoutsource mpaka zile sekta nyeti zinazotakiwa zishikwe na watanzania. Ni hayo tu

    ReplyDelete
  7. Mimi pia na-support mada ya kuwa serious katika kuimarisha taaluma ya vitendo katika masomo ya sayansi. Na nimeshuhudia wanafunzi wa sayansi wakikosa kujiamini katika maofisi wanayoajiriwa kutokana na kukuta vifaa mfano vya Network (Routers, Switches nk)vikiwa vipya kabisa machoni pao na kushindwa kutoa mchango wowote tatizo litokeapo.
    Kama mchangiaji hapo juu alivyosema, Video za masomo ya Sayansi hasa Information Technology zinasaidia sana sana hasa kwa mazingira yetu haya, na mimi ni mmoja wa watu waliofaidika na njia hii ya ufundishaji. Baada ya kuwasiliana na www.greatdesign.co.tz waliopo hapa Dar es Salaam, nimeweza kujifunza mambo mengi sana.
    Lakini hata hivyo, bado tunao wajibu wa kuikumbusha serikali kuwa huko tunapoelekea kwa mfumo huu wa nadharia sana katika masomo ya sayansi, hakuoneshi dalili nzuri kama kweli tupo serious kunyanyua wasomi wetu hapa nchini. Jitihada za wazi kabisa na madhubuti lazima zichukuliwe mapema kunudhuru hili jahazi kwa kuongeza vitendea kazi kwa wanafunzi wetu ambao maisha na uchumi wa nchi unawategemea ktk kuendeleza nchi kwa ujumla, na kuondokana na dhana ya kuwa wakodoaji macho katika Dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.

    ReplyDelete
  8. Mdau wa UDOM,

    Kwanza nakupa pole kwa yanayoendelea hapo chuoni kwenu! Ombi lako ni la msingi sana, madhumuni ya kuanzisha hivi vyuo vya uhandisi ni kuona Taifa linapata WAHANDISI bora na wenye tija kwa nchi yao. Kukosekana kwa Practicals kwenye sylabus yenu ni upungufu wa kimkakati na kiutendaji wa kiuongozi hapo chuoni kwenu. Jaribu kufukiri kwamba ombi lako haritajibiwa for the next three years, what should you do now???? Nakushauri unavyopewa "bumu" lako jaribu kusevu kiasi kidogo cha pesa kukusaidia wakati wa likizo. Nafahamu kuna kitu kinahitwa Practical Training, jitahidi sana kutafuta sehemu ya kufanya hizi training, hata kama chuo chako hakitakuwa na pesa za kukulipa, unajuhudumia mwenyewe kwa savings ulizofanya. Ni kiti dhahiri tulicho kuwa tunafanya sisi wenzako tulipokuwa tunasoma. Wakati unasubiri serikali ikusaidie muda unakwenda na ushindani wa soko la ajira ndivyo unavyozidi kukua.
    Kaka yako,
    Telecommunications Engineer (Former UDSM student)

    ReplyDelete
  9. Hamia UDSM..hicho chuo cha kisiasa zaidi

    ReplyDelete
  10. Mchangiaji wa kwanza unasikitisha!! Masomo ya Technology si siasa, yanahitaji practicals.Ni lazima uwe na busara, mtu mzima tena msomi anapotoa hoja kama hii public ujue mambo si shwali hata kidogo.
    Najua Michuzi unaweza usiweke mchango wangu!!!!!
    Napenda kusema UDOM imeanzishwa kisiasa, na wanasiasa wanaendelea kuitumia kisiasa, hii ni hatari sana.Wao wanacho jali ni namba ya wanafunzi bila kujali ubora wa elimu.Tulitangaziwa mkonga wa mawasiliano utakapofika, kila mwanafunzi ataweza kupata interneti lakini wapi, wameisha chakachua.
    Wanazidi kujenga majengo ya kichina kila kukicha, majengo yanavuja kila mvua inaponyesha, mipasuko kila mahali.ipo siku yataanguka na kuzika watoto wetu, mtakuja niambia.
    Nanyi wanafunzi muwe na akili, haki haiombwi, inapiganiwa,katika madai yenu yote unapotokea mgomo huwa ni fedha tu na chakula. ubora wa elimu unawekwa kando. Kumbukeni mnalipa ada kupitia mikopo na mtakuja kulipa. Umefika wakati sasa wa kudai walimu, tena wenye hadhi ya kufundisha chuo kikuu, si wa degree moja ambao ndo walimu wenu.
    Ingieni mtaani mdai elimu bora, walimu, practicals,internet, TV, kila kitu kwani kupata habari ni haki ya msingi ya MTz, daini vitabu.
    Waache usanii, utaanzishaje programme bila walimu,bila vifaa n.k

    ReplyDelete
  11. chuo cha kata udom

    ReplyDelete
  12. unonymous wakwanza karopoka. Anafanya watu wana doubt intelligence yake. Jamani tujue tofauti ya forums, Hii sio facebook

    ReplyDelete
  13. Registrar of Engineers - TzMarch 23, 2011

    Tatizo lako litashugulikiwa haraka sana na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

    Tunakushukuru kwa taarifa hii kwani nchi lazima iwe na wahandisi bora na sio bora mhandisi.

    Msajili

    registrar@erb.go.tz

    ReplyDelete
  14. Namuunga mkono mtoa maoni wa pili. Mfumo wa elimu wa nchi yetu unatakiwa kuangaliwa na kurekebishwa haraka sana. Kuna methali inasema (kama nipo sahihi) 'Aongozwae na kipofu hutumbukia shimoni'. Kwa bahati mbaya, shimo hili sio 'physical' kiasi kwamba unaweza kukuruka na kutoka. It is about culture, moral and thinking deterioration which cannot easily be recovered.

    ReplyDelete
  15. Kwako wewe mwanafunzi unayesomea degree ya "Mawasiliano Anga". Fikra za kushika vifaa vya ufundi katika masomo ya juu nakuomba uziondowe. Elewa kuwa wewe husomei Ufundi Mchundo, unasomea "Uhandisi".

    Katika masomo yote ya juu hasa upande wa uhandisi mwanafunzi hufunzwa nadharia zaidi katika kila kitu kwa lugha ya mahesabu. Wewe kama ni mwana mahesabu hutaona kama hamfundishwi kitu.
    Kama ungekuwa mwana mahesabu,kila component na mtiririko wa umeme katika fezi zake zote ungezielewa na kufurahia masomo yako. Kwa sababu ungeelewa vizuri sana na kwa upana zaidi.

    Lakini kutokana na maelezo yako hapo inanionyesha wewe hujiwezi kimahesabu.Wewe ni "Kiwete" wa mahesabu. Nakushauri ujiengue haraka katika fani ya "Mawasiliano Anga" jiunge na Political Science ili ukaendeleze kupiga "Ngebe".

    It's Great To Be Black=Blackmannen

    ReplyDelete
  16. MImi nimesoma IT bila hands on ni vigumu kuelewa..Walimu sio sana lakini maabara ni muhimu. Kama unalab ya nzuri basi uatakwenda huko na kitabu chako na kufanya vyote lakini kama hakuna lab hiyomajor wangeiondoa kwa sasa...Check MIT inavyodunda u na lab zao ni koboko....

    ReplyDelete
  17. wewe blackmannen huelewi unachosema na silazima uchangie iyo mada hapa tupo katika kujenga zaidi , kesho na kesho kutwa mdogo wako atatupwa udom halafu utashindwa la kuongea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...