Asalaam aleykum Ankal,

Mimi nina kero binafsi inayonichanganya akili kwa muda mwaka sasa, na ninaomba mawazo ya wadau Globu ya Jamii wanisaidie. Naishi ughaibuni na nina mpenzi wa kike wa kizungu ambaye nipo naye kwa miaka 4 sasa. Huyu msichana anataka tuoane na mimi pia nampenda ingawa swala la kuoa bado linanitatiza kwa sababu moja tuu, Uzungu wake.

Sina mpango wa kuishi ughaibuni na nina mpango wa kurudi nyumbani, bongo mnamo mwezi october wa mwaka huu 2011. Niko njia panda katika vitu viwili, kwanza nampenda huyu mtoto ingawa sitaki kuoana naye. Pili nina hamu sana na mapenzi ya kinyumbani ya kukaangiwa mahanjumati ambayo siyapati kwa huyu binti.

Tatizo liko sehemu moja.... simjui msichana hata mmoja wa kibongo hapa nilipo, au hata nilipokuwa bongo ambaye ana mwanamme mmoja tuu. Ninaposema msicha nina maanisha wale ambao wapo chini ya miaka 28, kwa tafsiri yangu. Kila mmoja nimjuaye ambaye yupo kwenye mahusiano siyo mwaminifu kwenye mahusiano yake. Sisi wanaume wa kibongo ndiyo labda tumelogwa, maana yake sisi uaminifu ndiyo hatuujui unaandikwaje. Sasa, swali langu ni kwamba...jee nijitwishe mzungu, au nipige chini na nichukue "risk" ya kubeba mwali wa kibongo huku nikiomba mola kwamba awe mwaminifu? Ingawa sijawahi kumuona hata m_bongo mmoja mwaminifu.

Siyo wazungu wote waaminifu kwenye mahusiano. Lakini wapo wazungu waaminifu. Jee waafrika (wabongo) waaminifu wapo? Ingawa anko kama ukiiona hii mada haina mshiko kwa blog ya jamii, then famillah, yote kheri.

Mdau Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. kwanza ni vigumu sana kumpata mtu bila kujua tabia yake,natumahi kuwa huyo uliyenaye unamjua vizuri sana tabia na kila kitu kwa hiyo kama unaweza ukamshawishi kuja kuishi huku dhani itakuwa ni nzuri zaidi lakini ukishindwa naomba utumie muda wako mwingi kumtafuta yule ambaye utaona hatakufaha kwenye maisha yako na usikurupuke tu utaju juta baadaye.......ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  2. Kama unampenda mzungu wako kwa dhati nakushauri umuoe na uje kuishi nae Bongo. Suala la mapishi sio tatizo, wapo watu wengi hawana ajira huku Bongo na wanajua kupika sana vyakula vya kiswahili. Ni kiasi cha kumpata mtu wa kumfundisha na atajua tuu kupika.

    ReplyDelete
  3. USHAURI, JIULIZE KWANZA WEWE BINAFSI, JE WEWE KWANZA NI MWAMINIFU???
    HUWEZI KUTEGEMEA KUPATA MWAMINIFU KAMA WEWE BINAFSI SIO

    ReplyDelete
  4. Pole sana kaka kwa shinikizo ulilonalo!
    Kwa ninavyofahamu mimi linapokuja suala la mapenzi ya kweli ni mioyo tu ya wawili wapendanao ndiyo inayowasiliana, na si macho, wala kiungo chochote kile. Zaidi ya hapo itakuwa ni tamaa ya mwili tu.Pia ni lazima ufahamu hutakaa upate mke asiye na kasoro yeyote ile kulingana na vigezo vyako.Cha msingi ni uvumilivu, yaani unayapokea mapungufu yake. Kumbuka pia nawe hujakamilika na wala hutatimiza kila kitu atakachokitaka mtarajiwa wako.Mimi nakushauri, kama mmependana na huyo msichana kwa kiwango ulichosema naomba umuoe, na MUNGU atakubariki...ishu ya vyakula vya kibongo si kitu, mnaweza kuja sometimes bongo mkapikiwa na ndugu, dada, mama, pi wanaweza mfundisha huyo shemeji yetu, ili awe anakupikia.Nakutakia maisha mema, kwa MUNGU binadamu wote ni sawa.

    ReplyDelete
  5. ACHA UASHERATI WEWE. PLUS HII SI BLOG YA MAPENZI
    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  6. Yaani wewe umeniudhi kweli???? Eti hakuna wanawake waaaminifu....! Naomba nikuhakikishie wako wengi sana na mimi mmoja wao, nimekuwa kwenye ndoa zaidi ya miaka 15, sijawahi kucheat!!!
    Naomba nikuambie kuwa kile upandacho ndo unachovuna! Kama wewe si mwaminifu, kwanin upate mwanamke mwaminifu??!!!
    Kwa taarifa yako wako mabinti wazuri ambao wanampenda mungu na wala hawajaguswa na mwanaume, na ziko ndoa nyingi tu ambazo wanampenda Mungu wala hilo swala kucheat halipo hata kwenye akili zao!

    ReplyDelete
  7. Kwanza kabisa, unampotezea huyo msichana wa watu wa kizungu mda wake, huna mapenzi nae, usingeongea kama ulivyoongea iwapo unampenda, unamchukulia kama yeye ndie yuko desparate kuwa na wewe! wewe sio muoji, iwe kwa mswahili mwenzio au kwa mzungu! kila siku mwizi atamuona kila mtu mwizi mwenzie, wasichana wa kibongo waliotulia wapo kibao, iwapo tuu wataona umetulia na sio mapepe, iwapo unataka aliyetulia na wewe ni mapepe, andika umeumia! naona katafute mke convent kwa masister, pale utapata sampuli unayoitaka.
    Nana.

    ReplyDelete
  8. Huyu kwanza atuombe radhi wasichana wa kibongo kwa kusema kwake hatujatulia,Yeye nahisi kazoea kuwaona wasichana wa kimjini wanafanya mapenzi kama sehemu ya kujipatia pesa basi akaona ni wote tuko hivyo? Siku hizi mambo hayo hayapo watu wanapiga kazi, wanasoma na kufanya biashara na sio kucheat / Umalaya.
    Wanawake wapo kibao wanamjua Mungu na wametulia tuli katika ndoa zao.Si mamiss now days pia wamebadilika ni wamama na wanandoa zao maana zamani watu ndio walikuwa wanasema vibaya,kwahivyo ukome kabisa kutudhalilisha.Kumbe ndio hivyo mnaakaaga huko Ulaya na kuanza kutusema kwa mabaya?

    ReplyDelete
  9. kikubwa tunachoangalia ni mapenzi,kama unampenda bibie nakushauri muoe.raha ya wazungu wanapenda sana kujifunza,atajifunza tu mapishi..mapenzi yashachakachuliwa huku,hakuna mwanamke wala mwanaume ambaye ni mwaminifu..fata moyo wako ila shirikisha pia na akili..kila la kheri..au kama vipi njoo kwangu...me natafuta mchumba

    ReplyDelete
  10. Pole sana mdau! Kwanza waombe radhi mama zako na dada zako (Wanawake wakiafrika/wabongo)na baba zako wanaume wa bongo kwa kuwakosea heshima. Hakuna watu wenyekujiheshimu na waaminifu duniani kama hawa wabongo mpaka wanaonekana kupitwa na wakati. Ni kweli sio wote waaminifu na wenye kujiheshimu lakini tukilinganisha kwa asilimia hawa wabongo waaminifu (wakiwemo mama na baba zako) ni wengi zaidi kuliko hao wazungu.
    Kwakuwa tayari umeishatilia shaka suala la kumuoa huyo mzungu nakushauri ni vyema umuache ili ukija bongo uje uoe binti mzuri ambaye hutokuwa na shakanae unapokuwa mahali popote. Ninahakika utapata mdada wakibongo mwenye sifa zote unazozitaka ikiwemo uaminifu.
    Lamsingi ufahamu uaminifu ni tabia. Tabia ya uaminifu ipo kwa binaadamu yeyote mwanamke na mwanaume, wa rangi yeyote wazungu kwa waafrika. Hivyo achana na suala la uafrika na uzungu. Mzarau asili ni mtumwa.

    ReplyDelete
  11. Mdau

    Achana na mzungu njoo bongo huwezi kukosa mdada wa ukweli. Kuna usemi huku kwetu unasema "Stay away from pork and a white girl".

    ReplyDelete
  12. Huyu jamaa ana zake, mzungu wa watu si binadamu tu kama wewe? eti swala la kumuoa linakutatiza kwa ajili ya uzungu wake. Complex tu zimekujaa.
    Halafu eti wanawake wakibongo sio waaminifu... wewe una matatizo...

    Kimoja tu ndio umelenga:Wanaume wa kibongo. Kweli hapo ni kama tumelaaniwa... mnajijuu wenyewe, mwingine analalamika eti kawaombe msamaha baba zetu... , wakati mababa kibao wenyewe ma-player wana mademu kibao.

    ReplyDelete
  13. Ebana unaweza ukambadilisha huyo mzungu ukamshape kadri unavyo taka,coz anaye kupenda atataka akuridhishe kwa hali na mali,so it is easy kumbadilisha uliye naye,ila tu awe tayari na umfundishe kukaanga hayo mahanjumati maana usitegemee ata google kujua mila zenu. Interest ni kitu muhimu kati yenu mzifanye zilandane.

    ReplyDelete
  14. KAKA wasikudanganye hawa, watoto wakibongo karibia wote sio waaminifu trust me. macho juu juu. Endelea na huyo mzungu mzee and you will be happy na stress free.

    ReplyDelete
  15. Wewe unakuja Bongo na kuchukua wadada wa kasino na night clubs unategemea upate mwaminifu. Oa mzungu wako na sisi hatuna shida na wewe Westerner utatutesea mabinti zetu bure. Oa mzungu akupigishe deki, ufue na kumpikia. Usitupotezee muda. Unadhani kwa kuwa huko majuu ndo wanawake walotulia watakupapatikia wakati wewe kicheche. Utaishia kutembea na hao hao macho juu na ku generalize kuwa wote hatujatulia. Usitupotezee muda oa mzungu wako. Ulaya ilikuwa zamani unadhani leo hii uje from nowhere nani atakukubali. Walotulia hawaparamii watu.

    ReplyDelete
  16. nani kasema wabongo sio waaminifu?? mimi ni mtanzania na nimwaminifu kwa mpenzi wangu iyo ni tabia ya mtu maana wapo wazungu ambao pia wasiowaaminifu pia,na ninafahamu wasichana wengi tuu ambao ni waaminifu.Tena hii ni dhana iliyojijengeka kati yetu,mimi naona ni dalili za kutojiamini yaani insecurity.igawa sikatai kuwa wapo wasio waaminifu ila sio wote kama ulivojaribu kuelezea.
    jambo jingine kuhusu uyo mzungu mbona siku hizi ni suala la kawaida watu wa mataifa tofauti kuoana, kama ni mapishi atajifunza na vyote unavotaka ni wewe tu kumueleza unayoyataka, ushauri wangu muoe uyo unayempenda.

    ReplyDelete
  17. ndugu yangu angalia sana hawa watu weupe nikisema hivyo sina maana mimi ni mbaguzi, ila tu nakutaadhalisha na haya kama uyajui..., hakuna mapenzi baina ya mweupe na mweusi, bali kwa sababu flani!!(reason)..... hayo lazma uyafahamu ndugu yangu,......sasa sikiliza mwanamke wa home ndio bora, kwa nyongeza tu hata akikosa rahisi kuelewa (nyumbani hakuna court wala nini, wazee wapo, viongozi wa dini wapo, ushauri ndugu jamaa na marafiki, pia hata mila zetu zipo)na hakuna vitisho vyovyote ambayo utaviface 'sijui karatasi hii sitaki kusain mara sijui nini!? basi tu ili mradi wewe ni foregner, nimeongea kwa mafumbo kidogo kama ni mwelewa maana unasema upo nje ya tanz... kaka hizi adha za wanawake hawa wote tunazo hapa, so usijaribu kucheza na hizo hazina za nyumbani kumbuka ndio mama zetu, please! angalia kwa makini na pia andaa kizazi chako bora, sio wewe baba unasema na mtoto anasema! we acha tu!
    home ni bora kaka!! huku ughaibun ni mtihan ila maisha tu, watu tunavumilia mengi, usidhani hata wao wadada weupe wanatupenda la hasha! ni kwa sababu tu, nimesema hapo juu., nadhani unaelewa nikisema hivyo.
    mdau japn.

    ReplyDelete
  18. Uyu jamaaa ndo walele kalaghabao, hii so globu ya mapenzi au unataka tu watu wajue kuwa una mdhungu???
    what a loads of crap?

    ReplyDelete
  19. Mamako hakuwa mwaminifu nini?acha kutukana dada zetu wake mama zetu shangazi zetu

    ReplyDelete
  20. This is so funny, naona sasa Michuzi blog inapamba moto. Jana tulikuwa na mbeba maboksi wa US, leo tuna mdau ya mapenzi na mzungu. Wera wera wera.

    Mdau from UK.

    ReplyDelete
  21. PAMELA SHUBI TAG MIKOCHENIMarch 22, 2011

    Kaka yangu wasichana waaminifu wako kwa YESU,from tha bible MALI MTU
    HUPEWA NA BABAYE BALI MKE MWEMA MTU HUPEWA NA MUNGU, ukitaka mke mwaminifu uje kwa Yesu. yeye ndiye mweny wake waaminifu.inaelekea wewe sio mwaminifu ndiyo maana unaona wengine ni wachafu kama wewe.

    ReplyDelete
  22. Namsikitikia huyo dada wa Kidhungu maana hajui kuwa unampotezea muda tu. Na wewe ndugu yetu si muoaji umekaa humu unaonekana kama vile unadhani unamfanyia feva dada wa watu. Kama wewe unapenda sana chapati na maandazi sawa wapishe wanaume waendelee na huyo dada maana kuna wajuba wangekuwa wameshaoa siku nyiiingi!! Unadhani yeye ndugu na marafiki hawasemi kuwa "unafanya nini na huyu Mmatumbi?" "anakutumia tu halafu ataoa mtu wa kwao!!" Namuonea huruma dada wa watu kakaa na Mkwere anatema broken miaka 4 kakuvumilia kisa mapenzi, kumbe mtu hana hata mpango...Ingekuwa binti yako halafu Muitaliano mmoja kala vyombo miaka 4 halafu anadai hataki kumuoa kisa mweusi ungejisikiaje? Pambaff!!!

    Mdau Boston, US

    ReplyDelete
  23. Pole sana kaka kwa kifupi tatizo lako linafanana sana na mimi though wmzungu wangu siyo kama wako kwa maana kimtazamo tulitofautiana coz yeye kuja kuishi Africa hataki kabisa. Ila kaka nawe cjui kama una msimamo katika huo uhusiano wako ingawa una miaka 4 sasa. Swali je huyo mwenzio anajua kama huna mpango wa kumuuoa na pia sababu unazotoa kaka hazina hata msingi kwann usimuoe huyo mzungu?
    Pili napenda kutetea kuhusu mabinti wa bongo ila si wote coz umetaja aina ya miaka yaani 28. Kaka ukweli ni kwamba Bongo mabinti waaminifu wapo wengi sana ila kiimani lazima umuombe mungu akupatie mke mwema coz hali mbaya sana bongo. Mabinti wamekuwa zaidi ya wasanii wanajua sana kuigiza usoni kumbe rohoni hawapo ukifanya mchezo utakuja kuwaolea wenzako, hasa hiyo age ya 18 hadi 28 katika kumi basi mwaminifu mmoja na kumpata huyo ni zali la mentali au kwa sala tu kaka.Wapo kibiashara zaidi na dada zangu wanaofatilia huu mjadala wanalijua hilo ila ukweli utabaki palepale kwamba wapo waaminifu.
    Mwisho naomba kukushauri uoe tu huyo mkeo as long as home wapo fair na kwao binti wapo fair kuishi naye africa na cha msingi anaupendo wa dhati then sioni haja ya kuhangaika kutafuta mwengine kama unaye.Angalia ushampotezea muda na ushasema kuwa mnapenda wezi jua labda ndo aliyekupa Mungu na mshafahamiana vzr sana. Ni hayo tu

    ReplyDelete
  24. Nimesoma maoni yenu yote, na naungana na baadhi ya watu hapa. Huyu jamaa, mimi naona anaishu zake binafsi na kama anataka ushauri ina bidi atuambie ukweli na sio kutudanganya. Dada zetu bongo siku hizi wameelimika na wametulia kama baadhi ya watu wanavyo kushauri hapa, kama unataka kuoa nyumbani lazima utafute muda wa kwenda nyumbani ili uweze kumtafuta huyo mwandani wako. Ushauri wapili nakuomba usitafute wakwenye internet. Naungana na mdau wa Japan hapo juu, hawa wazungu mapenzi yao ni ya muda tu, mimi nilikuwa naye namejijifunza mengi sana kuwa mwangalifu sana na hilo nadhani unaelewa ninavyosema.

    ReplyDelete
  25. Inaelekea wewe ni mwizi ndio maana unahisi kila mtu ni mwizi kama wewe. Wanawake wa kibongo nani asiyewataka huku niliko. Ni hot commodities hawa wadada kwa vile hawana papara kama wakikenya au ukitaka japo kusmell home kidogo (uganda) Wewe labda unatabia mbaya ndio maana unaona kila mtu kutoka bongo atakua na tabia kama yako basi mtakuwa hapa kaliki huko nani kwenu.

    Kwanza hata hawa wazungu ni matata kuliko wakikwetu. Hawa wanapenda wanaume weusi na kama amekupata wewe weka rafiki zako mbali kwa vile kama una rafiki mweusi akiongea vizuri na yeye amepata na ukirudi usiku unakumbatiwa vizuri tu kama vile hamna lililosibu ulivyokua haupo.

    Kwanza inaonyesha huna mapenzi ya kweli miaka minne bado unamzungusha mtoto wa watu? Kwanini unapoteza muda wake hivyo? hata ukienda bongo na hata ukipata mswahili itakua tabu. Ukipenda mtu kwa ajili ya kitu fulani hakuna raha kabisa. Mpende mtu kwa jinsi alivyo na sio nini ataweza kukufanyia. kama ni mpishi yupo lakini sio mke unaoa ukiwaza kuwa umepata mpishi. Ukimpenda mtu hujalia anajua nini wala nini. Mimi mtanzania lakini napika kila siku na wife ni mtanzania...

    ReplyDelete
  26. Acha uoga oa Mzungu wako usitake kuleta za kiswahili eti madikodiko, mtaenda kuyala Zanzibar kule forodhani muoe binti wa watu huko

    ReplyDelete
  27. ACHANA NA MADEMU WA KIBONGO USIJE UKALOST. WEWE KAA NA MZUNGU WAKO NA HAKIKISHA UNAPATA MAKARATASI .
    UJINGA WA KURUDI TANZANIA ACHANA NAO KABISA.. KWANZA MAJI HAKUNA, UMEME TATIZO, MBU NA VILE VILE MAJAMBAZI WENGI.

    KAA NA MZUNGU (PINK CAT) HEEE HE HE HE HE.. CHUKUA DEMU KWA CHINI BONGO KILA UKIRUDI.

    SASA UKICHUKUA DEMU ZA BONGO HAKIKISHA NI MIAKA 18 MPAKA 20 USICHEZE JUU YA HAPO.. WATAKULOGA KAKA YANGU.

    ACHANA NA UJINGA.

    MIMI MBEBA BOX WA USA NA KILA NIKUTUA BONGO HUWA NACHUKUA NDIZI MBICHI... YAANI 18 YEARS MPAKA 20.

    MAISHA YA NDOA TANZANIA NI UCHAFU MTUPU.. WENGI WANAWAKE WANAPENDA WANAUME NJE YA NDOA.

    MIMI KILA NIKIRUDI NA NYOFOA WAKE ZA WATU.. NA MAGIRLFRIENDS..

    HAMNA NOMA

    POA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...