JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU TOZO KWA WAGENI WANAOLALA KATIKA HOTELI NA MAKAMBI YA WAGENI NDANI YA HIFADHI ZA TAIFA
UTANGULIZI
Katika magazeti mbalimbali yaliyochapishwa tarehe 25.03.2011 kulikuwepo na taarifa zilizohusu kutenguliwa kwa maamuzi ya Waziri wa Malisili na Utalii Mhe. Ezekiel Maige kuhusiana na ongezeko la tozo za watalii wanaolala katika hoteli na kambi za wageni ndani ya Hifadhi za Taifa (Concession fee), wakati wa kikao cha pamoja cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kilichofanyika tarehe 24/03/2011 jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo ya Bunge ilipitia na kujadili taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu TANAPA za Mwaka 2008/09
UFAFANUZI
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika mwaka wa fedha 2008/09 lilipendekeza kuongezwa kwa tozo za watalii wanaolala katika hoteli na kambi za wageni ndani ya Hifadhi za Taifa. Ongezeko hili lilifuatia vikao vya pamoja baina ya TANAPA na wadau mbalimbali katika sekta husika ambapo wengi wao walikubaliana na ongezeko hilo.
Hata hivyo wadau wachache katika sekta hiyo ya hoteli hawakuridhika na uamuzi huo wa kuongeza tozo hiyo na waliamua kupeleka suala hilo wizarani wakitaka kusitishwa kwa uamuzi huo wakidai kuwa utaathiri biashara zao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, wakati huo, Mhe Shamsa Mwangunga ilikubaliana na pingamizi hilo la wadau ambao hawakukubaliana na ongezeko hilo na kuliagiza shirika la hifadhi za taifa, TANAPAkusitisha utekelezaji wa tozo mpya.
Hivyo, Mhe Ezekiel Maige, Waziri wa Sasa wa Maliasili na Utalii, hakuhusika moja kwa moja na binafsi kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
MSINGI WA ALIYEKUWA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII KUKUBALIANA NA PINGAMIZI HILO
Aliyekuwa Waziri wa Malisili na Utalii, Shamsa Mwangunga alikubaliana na pingamizi lililowasilishwa kwake kwa kuzingatia masuala kadhaa ya msingi yafuatayo:-
Ushindani wa Kibiashara: Vivutio vya Utalii vinavyopatikana Tanzania vinafanana kwa kiwango kikubwa na vile vinavyopatikana katika nchi jirani kama Kenya na Afrika ya Kusini hususani utalii wa wanyamapori.
Hata hivyo Tanzania tofauti na Kenya na Afrika ya Kusini haina uhakika wa usafiri wa ndege wa moja kwa moja. Mathalani, Kenya wanawasafirisha watalii kwa kutumia Shirika lao la ndege kutoka vituo 78 duniani kote na kuwapeleka Nairobi moja kwa moja, Afrika ya Kusini wao wanasafirisha wageni kupitia Shirika lao kutoka katika vituo 84 duniani kote moja kwa moja hadi Afrika ya Kusini.
Kutokuwa na ndege zinazofanya safari za moja kwa moja nchini, wageni wanaofika nchini hulazimika kutumia muda mwingi njiani na hivyo kutumia gharama nyingi zaidi katika kutembelea hifadhi zetu.
Ongezeko lolote la tozo lingemlazimu mgeni kuendelea kulipa zaidi anapoamua kutembelea Tanzania na hivyo wageni wengi wangeacha kufika nchini na badala yake wangetembelea nchi za jirani ambazo gharama za mgeni kutembelea huko ni za chini kulinganisha na Tanzania
Sera ya Utalii: Sera ya Taifa ya Utalii inayotekelezwa nchini ni ya wageni wachache lakini wenye kulipa zaidi (Low Volume High Yield Tourism) Hata hivyo kulingana na uwekezaji uliopo nchini mathalani, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuna vitanda 2,128 huku hifadhi ya Maasai Mara ikiwa na zaidi ya vitanda 4,000 . Kutokana na ukweli kuwa kuna uhaba wa hoteli ndani ya hifadhi ya Serengeti, wageni wanalipa zaidi kuliko hoteli za Masai Mara. Kwa mfano, katika hifadhi ya Serengeti, hakuna Hoteli inayotoza chini ya Dola 150 kwa siku wakati hoteli za Masai Mara zinatoza hadi Dola 40.
Kulingana na uwiano huu, na ushindani ndogo wa bei katika hoteli za Serengeti, ongezeko lolote lile la gharama lingelazimu wenye hoteli nchini kuongeza gharama ambazo zingepaswa kulipwa na mgeni. Ndiyo maana baadhi ya wamiliki wa hoteli walikubali kwa kujua kuwa mzigo usingekuwa wao bali wangeupeleka kwa wateja wao na hivyo kufanya hoteli za Serengeti kuwa ghali zaidi!
Tabia ya wafanyabiashara kuongeza bei kwa pamoja: Pamoja na kwamba wafanyabiashara walishirikishwa na kukubali, uzoefu uliokuwepo na unaoendelea hadi sasa ni kuwa wamekuwa wakipandisha bei ya huduma zao kila wakati serikali inapopandisha tozo zake. Aidha, ongezeko la bei ambalo wamekuwa wakiweka wakati mwingine ni kubwa hata kuzidi ongezeko la tozo lililowekwa na serikali na hivyo kutumia mwanya huo kuwaumiza wateja na kuathiri sekta ya utalii na sekta zingine.
Hali hii inatokea hasa kwa kutambua kuwa hakuna mamlaka ya kudhibiti bei za hoteli. Hivyo, wenye hoteli wamekuwa wakitoza bei kutegemea ushindani uliopo. Pamoja na hayo, kwa kuwa waliowekeza kwenye hifadhi ni wachache mara nyingi wanafikia uamuzi wa pamoja wa kupandisha bei.
Mtikisiko wa Uchumi: Katika kipindi hicho kulikuwa na hali ya kuyumba kwa uchumi wa dunia na hivyo kuathiri sekta ya utalii. Uamuzi wowote wa kuongeza gharama katika kipindi hicho ungeweza kuathiri idadi ya wageni wanaotembelea nchi yetu, hasa kwa kuzingatia ushindani uliopo na ukweli kuwa gharama za kutembelea nchi yetu tayari zilikuwa juu.
Hivyo basi busara za aliyekuwa Waziri wa Malisli na Utalii wakati huo, zilipelekea kusitisha mapendekezo ya ongezeko la tozo kwa nia njema ya kutoathiri sekta ya utalii nchini.
HALI ILIVYO SASA
Baada ya kuimarika kwa hali ya uchumi duniani Waziri wa Maliasili na Utalii wa sasa, Mhe. Ezekiel Maige, ameiagiza Bodi ya TANAPA kuongeza concession fee. Aidha, ameliagiza shirika kufikiria njia bora zaidi za kukusanya ushuru huo. Maagizo hayo yalitolewa kupitia Bodi ya Wadhamini ya TANAPA katika kikao chake kilichofanyika Kempinski Hotel Dar es Salaam tarehe 20 Desemba 2010.
MWISHO
Wizara inafafanua kuwa hakuna mgongano wowote uliopo kati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na Wizara ya Maliasili na Utalii. Maamuzi yaliyofanyika katika kipindi cha 2008/09 yalifanyika kwa nia nzuri ya kuinusuru sekta ya utalii nchini isianguke kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mtikisiko wa uchumi duniani na tayari Waziri wa Sasa wa Maliasili na Utalii Mhe Ezekiel Maige, alikwisha kuliagiza shirika la hifadhi za taifa TANAPA kuongeza tozo hilo.
Aidha, katika kusimamia uwiano wa bei na huduma katika sekta ya Utalii, Serikali kupitia sheria ya utalii namba 11 ya 2008 imeanzisha utaratibu wa kuziweka hoteli katika madaraja ya ubora ili bei ziendane na ubora wa huduma zinazotolewa.
George Matiko
MSEMAJI WA WIZARA

Ndugu zangu,
ReplyDeleteMajibu haya yanaonyesha namna gani watendeaji wengi serikalini ni wababaishaji. Hayo sio majibu ya kuweka hadharani kuonyesha namna gani waziri alifikia maamuzi.
1. Kwa nini mahoteli Kenya yatoze dola 40, na Serengeti dola 150, je wizara hilo linawahusu vipi? Mimi nilidhani huo ndio ulikuwa mwanya wa waziri mwenye dhamana kukazia hukumu ya tozo kwani wanawatoza zaidi watalii, na maana hiyo hata wakilipa kodi bado faida yao ngelikuwa kubwa kuliko wakenya. Lakini ingelifanyika hivyo Kenya, ni wazi wangeumia maana mapato yao ni kidogo.
2. Suala la watalii kuletwa na mashirika ya ndege ya nchi husika halina mashiko hata kidogo. Je, sisi wageni wetu hutokea Kenya tu? Je, anasahau ya kuwa Kenya airways ina ubia na Precisionair ambayo ni ya watanzania ipa? Je, waziri anataka kutuambia kwa kuwa Kenya airways inaleta watalii hivyo bei ya nauli inayotoza ni ndogo kuliko mashirika mengine? Je, gharama za kuendesha shirika la ndege nazo ni nafuu tu kwa Kenya airways na si kwa mashirika mengine? Au, Kenya airways hutumia maji badala ya mafuta! Vipuri hununua Gerezani hivyo kulipa Tshs?
Je waziri anasahau kwamba wakati wa msimu wa watalii shirika la KLM huongeza ndege an safari zake kwa ajili ya watalii wanakwenda kanda ya kaskazini? Je, na hawa nao huenda Kenya kwanza, halafu ndio warudi Tanzania?
Nimesikitishwa sana na majibu hao. Hapo moja kwa moja kuna masilahi binafsi, na ndio maana kamati ya bunge imetumia lugha ya tafsida kwa kusema kulikuwa na 'mazingira ya rushwa'.
Mdau
This is funny: Kuwa na shirika la ndege ni kigezo kidogo tu. swala hapa ni kuwa na usafiri unaofikika katika nchi husika, Tanzania imeona ongezeko la mashirika ya ndege na safari zao zaidi ya maradufu kwa kipindi cha miaka mitano, sasa kuna mashirika kama Emirates,Swiss Air,Qrter, SAA,Ethiopia, Turkish, BA,YemenAir, Zambezi,Zambia, AirMalawi, prescion,Kenya Airways nknk,
ReplyDeleteHawa wote wanaziba pengo la mgonjwa wetu ATCL, whats mater is demand and suppy of the ticket in terms of its competitiveness,
So swala la mfano wa SAA na KA si kitu kabisa,
Swala ni kunedelea kutangaza utalii...dola 10-50 si kitu kwa nchi za ulaya, marekani, na Asia zilizoendelea,
Greedy , papara ...hahah kila mtu anajifanyia lake....This is very interesting...
ReplyDelete