Mkutano Mkuu wa mwaka 2011 wa TFF unaanza Machi 26 mwaka huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
Mkutano huo utakaoanza saa 3 kamili asubuhi utafunguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi.
Mkutano huo utakaokuwa na ajenda 16 utamalizika Machi 27 mwaka huu.
Wajumbe wa mkutano ambao wamefikia hoteli za Valentino iliyoko Mtaa wa Aggrey na Spice Inn, Mtaa wa Lumumba.
Ajenda za mkutano ni;
Kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kusoma na
kuthibitisha ajenda, kuthibitisha muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama, kupitisha taarifa za utekelezaji wa Kamati ya Utendaji, kupitisha taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2011, uchaguzi wa nafasi zilizo wazi, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF (kujadili mikoa mipya), kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na wanachama au Kamati ya Utendaji, Mengineyo na Kufunga kikao.

Taifa Stars inacheza kesho? mbona mnafanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Mmeiandaa vipi timu ya Taifa?Huo mkutano mtaufanya saa ngapi? acheni ubabaishaji! ilishindikana kusogeza mbele mkutano huu na nyie kupata muda wa kutosha kuiandaa timu yetu? Ole wenu tukifungwa!!!!!
ReplyDeleteMtu kutoa maoni yake isionekane kuwa ni utovu wa nidhamu, lakini mtu unaposoma ajenda za mkutano Mkuu kama huu hazitajwi kamili baadhi ya vipengele vya mambo ambayo hata sisi Watanzania tungependa tuyaone yakijadiliwa.
ReplyDeleteTunabaki na swali! Je, mikakati gani Tanzania inaweka ili kuziweka na kuziwezesha timu zetu za soka kuweza kushinda katika mashindano ya kimataifa? Taifa Stars siku zote ni kufungwa tu na viongozi wa TFF na mabosi wote wa michezo kutoka Wizarani wanapokutana kama hivi, kazi ni kujadili kuhusu mambo mengine ambayo sisi Watanzania wa kawaida hatuyafahamu kwa vile hayaanikwi hapa tuyaone na sisi tupate nafasi ya kuyajadili kwa faida ya nchi yetu.
Katika kipindi cha maoni katika kituo kimoja cha redio ya kidini hapo Tanzania (Radio Maria Ijumaa tarehe 25 machi) kuna mtoa maoni Tobias Kifaru alitoa maoni mazuri sana kuhusu timu yetu ya Taifa Stars, ambayo kwa maoni yangu mimi niliyaona maoni yake (Kifaru) kuwa TFF wanatakiwa kuyaangalia na ikiwezekana wayafanyie kazi.
Viongozi wa TFF ama Wizara husika wasiposikiliza maoni ya Watanzania, nchi haitaweza kuendelea katika michezo ya aina yoyote aslani!. Hayo ndiyo maoni yangu mimi kwa leo. Ahsanteni Washiriki wote wa mkutano mkuu wa TFF na ninawatakieni heri na baraka katika shughuli hiyo ngumu.
Peters Mhoja - Sweden
Mobile: +46 70 511 47 69