Katibu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto)akibadishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 46.8 na Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa(kulia) jana jijini Dar es salaam.Msaada huo ni utatumika ukarabati na ujenzi wa njia za usambazaji wa umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, Ujenzi wa Daraja la Rusumo lilipo mpakani mwa Tanzania na Rwanda na ujenzi wa Kituo katika Mpaka wa Nchi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. du kwa kweli kutoa ni moyo usambe ni utajiri. yaani jamaa wajapani pamoja na kasheshe zoote kwao lakini bado tu wanatukumbuka wamatumbi duu!!
    Mungu awasaidie wajapani. najua watu watasema may be wanania zao lakini sidhani.
    mimi nawapa big up sana tu wanasaidia sana hawa jamaa.

    ReplyDelete
  2. Mimi nina swali. Japani wamepigwa na Tsunami hata mwezi haujapita. Mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanatoa harambee kuisaidia japani kukabiliana na maafa ya tsunami. Swali ni hivi, japani ina uwezo gani wa kutoa misaada ingali wao wenyewe wanahitaji msaada? Hii misaada ina masharti gani? Tusije angalia tunaweza rudishwa enzi za utumwa. Hoja zinakaribishwa.
    Mdau kwa obama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...