Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, (Vodacom Group ) Pieter Uys, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare. Rais Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi (Vodacom Group) , Pieter Uys, (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare (kushoto) na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba, wakati wa ujumbe wa kampuni hiyo ulipofika Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini.
Rais Jakaya Kikwete, akiagana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi (Vodacom Group) Pieter Uys baada ya kuktana na ujumbe wa kampuni hiyo Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya kuongeza uwekezaji nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare. Kulia ni Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba.
Rais Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni hiyo, Mwamvita Makamba, wakati alipoongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu za mkononi, (Vodacom Group) , Pieter Uys (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietlof Mare

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jamani Mwamvita..tunavyokuhusudu ukavaa suti nzuri hivyo na viatu vyekundu? Mbona makubwa hayo?

    ReplyDelete
  2. Mwacheni mtoto wa kisambaa avae anavyotaka. Ana amani moyoni kwa vile ana pesa za kumtosha hata akivaa msivyotaka.

    ReplyDelete
  3. suti blue viatu vyekundu ?????? mchemsho

    ReplyDelete
  4. Jamani siku hizi ndio fesheni kuchanganya rangi kama hamjui, ukivaa rangi zinazo fanana unaonekana wa mwaka 47 kwa hiyo anaenda sambammba na wakati, sie tuliobaki nyuma ndio tunaona kachemsha

    ReplyDelete
  5. Jamani Watz acheni hayo hadi naogopa kurudi home maana huku Ughaibuni
    tunavaa tunavyotaka hatuvai mnavyotaka, ukijiagalia kwa kioo ukaona unapendeza na umeoga ukapaka mafuta na kapafium kidogo basi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...