Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili makao makuu ya Wizara ya Maji, Ubungo, jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya
Rais Jakaya Kikwete akiwasili Wizara ya maji
Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na uongozi wa Wizara ya Maji
Juu na chini ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Maji wakati alipoitembelea makao makuu ya Wizara hiyo ubungo jijini Dar es Salaam leo
Mzee hapa kazi tu....
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya muda mfupi baaada ya kuwasili katika makao makuu ya Wizara hiyo Ubungo jijini Dar es Salaam leo

NA VERONICA KAZIMOTO – MAELEZO


Rais Jakaya Kikwete amezitaka halmashauri zote nchini ziwajibike katika kusimamia miradi mbalimbali ya maji ili kuwasaidia wananchi kupata maji safi na salama.

Akizungumza na wafanyakazi wa Wizara ya maji alipotembelea wizarani hapo, Rais Kikwete amesema halimashauri zina jukumu la kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia miradi hiyo iweze kufanya kazi kikamilifu na hatimaye kurahisisha upatikanaji wa maji.

“Halimashauri lazima zitambue kwamba katika bajeti wanazopanga kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo kamwe zisisahau mradi wa maji kwani hakuna asiyefahamu umuhimu wa maji katika maisha ya binadamu,” amesema Rais Kikwete.

Naye Waziri wa maji Profesa Mark Mwandosya amesema katika kipindi cha 2006 na 2010, Wizara yake kupitia program ya maendeleo ya sekta ya maji imejenga na kukarabati miradi ya maji zaidi 4,000 yenye vituo vya kuchotea maji zaidi ya elfu 9,000 ambavyo huhudumia watu wapatao elfu 2,700.

Mwandosya amesema wizara yake inaendelea kuviimarisha vyama vya watumia maji kwa kutoa miongozo na mafunzo ya njia bora na endelevu za kusimamia miradi ya maji.

Waziri Mwandosya amebainisha kuwa Wizara yake inaendelea kugharamia sehemu ya uendeshaji, ukarabati na uimarishaji miradi hiyo ya maji na sasa hivi ina mpango wa kukarabati miradi iliyochakaa ili iweze kutoa huduma kama inavyotakiwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hivi huyo JK ameongea na hawa watu wanawoitwa DAWASCO? Maana kazi yao ni kununua magari ya kifahari tu na kazi hakuna! Nasema kazi hakuna kwa sababu sisi wananchi tunahitaji kuona maji yanatoka na si kuona mashangingi yakiwa yamepakwa rangi nzuri mitaani. This is not our interest! C'mon JK fanya kweli hapo DAWASCO. Tunahitaji mtendaji wa shoka si wakubabaisha babaisha kama huyo anayeendesha sasa. Atakupa sababu lukuki lakini mbona hayo hatukuyaona wakati wa Mtalemwa? JK tunakuaminia babake, rekebisha hiyo kitu DAWASCO.

    ReplyDelete
  2. Jamani what`s up na hizo pen kwenye mashati ya hao viongozi wetu? ndio fashion siku hizi au?? Am just wondering.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...