


Na Magreth Kinabo,
MAELEZO-Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekabidhi pikipiki mbili za matairi matatu aina ya Bajaji kwa wasanii wa Kikundi cha Survival Sisters zenye thamani ya shilingi milioni 9.5.
Msaada huo umekabidhiwa jana (leo) jijini Dar es salaam na Kaimu Mnikulu Mkuu Kassim Mtawa kwa niaba ya Rais Kikwete.
Akikabidhi pikipiki hizo kwa wawakilishi wa Kikundi hicho Mtawa alisema kuwa Rais alitoa msaada huo baada ya kupata ombi la vyombo vya usafiri kutoka kwa wasanii hao ili waweze kuboresha kazi zao na kufika katika matukio mbalimbali kwa wakati.
Naye Msanii Irine Malekela alimshukuru Rais kwa kuwakubalia ombi lao na kuwasaidia vyombo vya usafiri ambapo vitawawezesha kuchukua vifaa vyao vya muziki kuelekea kwenye kumbi mbalimbali kwa ajili ya kutoa buruadani.
"Tunamshukuru Baba Kikwete kwa msaada wa vyombo hivi kwa vitatusaidia katika shughuli zetu na kuondokana na adha ya kulala katika kumbi kwa sababu ya shida ya usafiri iliyokuwa ikitupata mara kwa mara" alisema Irine.
Aidha aliongeza kuwa msada huo pamoja na kutumia kwa shughuli zao za kimziki zaidi pia watakuwa wanatumia katika shughuli za kibiashara ili kukiongezea kikundi mapato zaidi.
Kwa upande wake Ratifa Abdallah alisema kuwa vyombo hivyo vitawasaidia kufika katika sehemu mbalimbali kwa wakati na hivyo kuanza kutoa burudani itakayotuwezesha kujipatia fedha kwa ajili yetu na familia zetu.
" Msada tuliopata leo utatusaidia kutupa kipato kwani wakati mwingine tulishindwa kuhudhuria katika matukio mbalimbali kwa sababu ya kukosa usafiri na hivyo kukosa fedha....hatua ya Mheshimiwa Rais kutusaidia ametupa moyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuboresha kazi zetu ili ziweze kuwa nzuri zaidi."alisisitiza Ratifa.
Kikundi hicho kina wasaini watatu ambao ni Rebeca John , Irine Malekela na Ratifa Abdallah.
Hivi bajaji ni gari au pikipiki?
ReplyDeleteratifa au latifa? jamani kiswahili kinakuwa taabu je kimombo inakuwaje? mara utaona mathara badala ya madhara, akuna badala ya hakuna,mafuno badala ya mavuno, kudunda sindano badala ya kunga sindano. tutafika kweli jamani???
ReplyDeleteHongera Survival Sisters! Endeleeni na kazi nzuri.
ReplyDeleteKweli kiswahili kigumu lakini ukitaka kumkosoa mtua basi na wewe jipange vizuri kwanza. Kunga sindano ndio nini? Ni afadhali mtu aseme kudunda sindano nitamwelewa kuliko kunga sindano...
ReplyDelete