Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Abeid Mwinyimsa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Afande Barlow wakiangalia kwa makini utoaji wa tiba unakofanywa na Dada Margareth Mutalemwa huko Urban Centre 'uzunguni' Tabora
Mkuu wa mkoa akiwa na wakuu wa ulinzi na usalama wa Tabora eneo la tukio
Askari polisi akiombewa kabla ya kupata dozi
Picha na Habari na Mkala Fundikira
(pichani akiwa na Dada Magreth) wa Keronyingi blog

Baada ya kumaliza kutoa dawa kwa watu waliokwenda kwake tangu saa kumi alfajiri,jioni hii nilipata nafasi ya kumhoji Magreth Mutalemwa (40) mwenye Mume na watoto wanne,na mahojiano yetu yalikuwa kama ifuatavyo:

Keronyingi- Dada pole na kazi, unaitwa nani?
Magreth- Asante, naitwa Magreth Mutalemwa
Keronyingi- Unaweza ukaniambia pana nini hapa kwako mpaka watu wamejaa kiasi hiki?
Magreth- Mimi hapa natoa huduma ya maji
Keronyingi- Huduma ya maji kivipi?
Magreth- Nawapa watu wanaokuja hapa huduma ya kikombe cha maji
Keronyingi- Ili kiwasaidie nini?
Magreth- Kinawatibu magonjwa wale wote wenye kusumbuliwa na magonjwa mbali mbali
Keronyingi- Ni tangu lini na vipi wewe umejua unaweza kutibu watu?
Magreth- Tangu tarehe 21/March/2011
Keronyingi- Enhe nieleze ilikuaje?
Magreth- Nilikuwa nikipata msukumo baada ya kuoteshwa kabla ya tarehe 21 na kuidharau ndoto ile nilianza kupata matatizo lakini baada ya kuanza kufanya yale niliyotakiwa kufanya matatizo yakaisha ndio mpaka leo natibu watu.
Keronyingi- Dawa yako ina mchanganyiko wa vitu gani?
Magreth- Ni mti mmoja tu, ambao nauchemsha na kuwapa watu wanywe.
Keronyingi- Je umepata kuwasikia watu wengine wanaotoa tiba kama wewe ambao ni Mchungaji Mwasapila, Babu dogo wa Mbeya?
Magreth- Ndio mimewasikia
Keronyingi- Unawazungumziaje?
Magreth- Ah ninavyoona mimi huu ni uwezo wa Mwenyezi Mungu tu, kwani katika uoteshwaji wangu nakumbuka sauti iliniambia tupo watatu na tumetunukiwa roho safi kufanya shuhuli hii ya kutoa tiba. Kwa hiyo naamini hao ni wawili na mimi ni wa tatu na ndio tuliotunukiwa.
Keronyingi- Pole kwa kazi na nashukuru sana
Magreth- Asante, karibu tena.

Mpendwa mdau nataraji kuendelea kukuletea habari toka kwa Magreth Mutalemwa mpaka nitakaporejea jijini Dar. Endelea kufutilia maendeleo ya dada na tiba yake toka urban quarter, Uzunguni,Tabora

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Mpo watatu? je akitokea na wa-nne utasemaje? Na akawa na uwezo kuliko nyie?

    ReplyDelete
  2. Nimesikia kuna mkakati wa waganga wa kienyeji wote pamoja na wachawi waliokubaliana wote wajitokeze nchi nzima kudai kuwa wameoteshwa kutoa tiba.

    Ndio maana wote wanaigiza mtindo wa kutumia kikombe wakati waganga wote walikuwa wanatoa dozi mbali mbali. Na wote wamekubaliana watoze sh. 500 tu kumuigiza mchungaji.

    Lengo lao ni kuishinikiza serikali iwafungie wote wanaotoa tiba ikiwemo mchungaji kwa kuwa mchungaji ameharibu soko lao.

    Kawaida waganga walikuwa wanaomba kuku, mbuzi na walikuwa wanatoza pesa nyingi lakini ili kupambana na mchungaji wameamua kutoza sh. 500

    ReplyDelete
  3. SASA INABIDI TUWE MAKINI SANA, MAANA NAONA HATA NGUVU KUU YA DOLA IPO MAHALI HAPA, ILA CHA KUJIULIZA, KWANINI MAGRETH KAJITOKEZA BAADA YA BABU? KWA NINI AWE KAOTESHWA KIKOMBE KAMA BABU? JE HUYO MR. DREAM MAIKER YUPO TANZANIA TUU? JE MTI HUO NDIO KAMA WA LOLIONDO? NAONA AFANDE ANAOMBEW\A AAPEWE KIKOMBE, JE IMANI ZETU ZINAELEKEA WAPI? MMMH HAYA BWANA YA KAISARI MPE KAISARI, ILA TUWE MAKINI MAANA BUGURUNI DAR KUNA DOGO, MBEYA KUNA MMAMA TENA NA KESHO UTASIKIA MICHUZI NAE ANATOA KIKOMBE, NADHANI BABU INAWEZEKANA KAOTESHWA SINAUHAKIKA, HUU NI MTAZAMO TUU

    ReplyDelete
  4. babu wa loliondo yeye kasema hakukuwa na mtu mwingine wakati anaoteshwa...dada katuambia wapo watatu dah kweli hii na sanaa ya kuwateka watu akili....jaman sio kila ndoto ina maana kadili tunavyoyafikiria matatizo yetu ndio hayo tunayoyaota usiku wake.....sasa kama siku nzima unafikiria mzizi fulan ni dawwa usiku utaota tu na kutuambia umeoteshwa na mungu.....

    ReplyDelete
  5. INASIKITISHA SANA,HII INAONYESHA WAZI WAZI SERIKALI NA WANACHI WAKE WAMEKATA TAMAA YA MAISHA KABISA,NA BADALA YA KUKAA CHINI KUFIKIRIA NI JINSI GANI TUTAPATA UMEME NA KUMALIZA UFISADI SMMEBAKI KUONGELEA VIKOMBE....MUNGU ISAIDIE NCHI YANGU INATIA HURUMA NA AIBU

    ReplyDelete
  6. Huyu dada nafikiri amefanya sanaa moja kubwa sana.....anaonekana kabisa kaiga ili atoke kimaisha....hizi ndoto babu hakutuhadithia kuwa walikuwa watatu. Na yule wa mbeya ahojiwe kama kweli walikuwa watatu?

    ReplyDelete
  7. Ujanja kuwahi, MICHUZI nawe ota haraka uwahi la sivyo vya kuota utakuta vimekwisha

    ReplyDelete
  8. Dada umekosea wewe si wa tatu bali ni wa nne: BABU LOLIONDO, FUNDI BAISKELI ROMBO, DOGO MBEYA, na wewe DADA TABORA! Ila ninachoona wewe umeamua kubalance agenda kwani watajwa wengine wote ni wanaume. Sasa time imekamilika naona kwani kila jinsia na rika zote zimeoteshwa. KAZI KWELI KWELI

    ReplyDelete
  9. Nimeoteshwa nifungue BLOG yangu haraka sana na itavuma kuliko Blog zote. Pia nimeambiwa matangazo yote ya Biashara nisitoze zaidi ya Shilingi 50,000/=. Nimekatazwa pia kutumia umeme wa TANESCO kwani upatikanaji wake una walakin. Nimeambiwa nitaletewa Genereta baada ya kutibu wagonjwa 100 wa kwanza na wanablogu wengine woote watakuwa chini yangu( hata huyo anayeitwa Ankal)na yule anayeendesha baiskeli kule Iringa.

    Kipara Siugonjwa, Mikanjuni Tanga.

    ReplyDelete
  10. Michuzi aoteshwe wakati tayari WANAYE NABII YOHANA MASHAKA WA WOLSTRITI. Nasikia Yohana mashaka anagawa kikombe kikubwa, ukinywa tu unakuwa tajiri na jiniasi.Mashaka ni nabii wanne

    ReplyDelete
  11. Kwa wapendwa watanzania wote
    nimeoteshwa na mungu dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.Kikombe cha maji ya miwa yaliyoombewa unakunywa ni sh 300 tu,ni rahisi kuliko babu.Huna haja ya kusafiri mbali ninapatika hapa magomeni dar es salaam mtaa wa mfipa,uliza kwa braza utapelekwa.Tafazali njoo na chenji kamili.
    braza wa magomeni

    ReplyDelete
  12. EE hii ni kali sana yaani nyie watoa Maoni mmeniuwa kabisa yaani sijui maneno mnayapata wapi,nilikuwa na stress zangu lakini imebidi nicheke kwa maneno yenu,ni kweli michuzi awahi kuota maana hizi pesa zinampita akija kujidai anaota baadae atakuta mwana si wake.Hiyo ndo Bongo Bwana home unachemsha ubongo unakaza boot na kujipanga kuingia mzigoni wa hali ngumu ya maisha ya watanzania waliao machozi ya samaki alijiimbia marehemu Remmy!Lakini naona mdau hapo juu unaonekana kumtetea Babu wa Loliondo na kumkandia magret,kwani mimi naona wote sawa tu maana ujanja kuwahi,,Sasa hivi hakuna njia nyingine ya kusurvive na hali mbaya ya Bongo ni kubuni maisha,kwani wakale polisi?Viongozi wenyewe wanaenda kupata kikombe,na mpaka askar polisi,itakuwa raiya!viongozi wakati wote ndo mfano mzuri sasa wanaelimisha watu kunywa kikombe,,,,Kama kweli tunakimbilia kunywa tu vikombe Hospital zitabaki tupu na hakuna kushughlikia maji umeme barabara na usalama barabarani,ajira,ambavyo ndo shida kubwa ya wabongo.EE Mola tunusuru na matatizo haya!Maan sasa watu tunamkufuru Mungu Mola alisema niombeni nitakupeni kama kweli mtu unafunga safari na kujuwa huyu mwenzangu ndo mwenye kuoteshwa ya kweli na Mungu na akimuomba Mungu tu anapewa ukajidharau wewemwenyewe kwa utukufu wake Mungu utaumia kwani hata watoto wadogo mbona wanapata shida na kufa ghfla kama huko Japan walivyozolewa na tsunami,wamemkosea nini Mungu,si Malaika tu hao hawana dhambi,Acheni kumshirikisha mwenyezi Mungu!,,Iko siku ya siku kila mtanzania anaejitokeza Ulaya ataitwamganga au mchawi!hata huko Oman na South Africa watanzania tunajulikana kwa Ushirikina na Uganga,,Ni hayo tu!Ni Ahlam wa UK

    ReplyDelete
  13. Watanzania wengi kutokuwa na Elimu na Ujinga umewatawala,na ndiyo maana ni rahisi sana kudanganyika!Imani yao ni ndogo sana kwa Mungu na ndiyo maana wanaamini kwa kila jambo wanaloambiwa!Hiyo yote ni biashara tu!Mbona wasifanye matibabu bure kama ni kweli wameoteshwa?Hiyo ni dili tu!hakuna tiba hapo!Je Wenye utalaam mkubwa ulaya eti washindwe kugundua tiba ya magonjwa sugu,halafu wao wa kijijini ndiyo waweze kutibu watu?Serikali nayo imefumba macho badala ya kuwaelimisha wananchi na kupiga marufuku utapeli huo lakini imenyamaza kimya tu,sijui kuna nini hapo?Watanzania amkeni sasa acheni kudanganywadanganywa tupo mwaka wa 2011 sasa!

    ReplyDelete
  14. dhana ya kikombe, mti, kuchemsha na kunjwa ni ya kizamani sana, kwa sisi generation X nikioteshwa basi itakuwa kwamba "Yeyote yule atakaye access blog yangu na ku-tweet maombi yake basi atapona" Hapo vipi?
    Alex Bura

    ReplyDelete
  15. mi sifahamu ina maana watanzania wote wana magonjwa SUGU? Basi kunatisha sana huko Tanzania,kule Zanzibar je hakuna alooteshwa-niliskia kuna dogo mmoja anaitwa Ustadh Salum NDIO ALOANZA HAYO AU VIPI WADAU? Sema yeye naona hanywishi watu vikombe yeye anakuombea dua tu-USHIRIKINA WOTE HAO KUSIJE KURIPUKA MAGONJWA MKAULIZA MCHAWI NANI

    ReplyDelete
  16. mshikaji hapo juu unaonyesha kuhusudisha uzungu sana. shauri lako watu wanapona we utabaki kusema hadi majuu waseme. you had a point but puting that ideal of people from majuu does not bring sense. discovery can be done anywhere and by anybody that we call creativity so usikubili wa majuu. kikubwa tunangalie ukweli wa haya mambo na kutoa maamuzi na kama yanaukweli basi acha watu wapone subiri ukishindwa hospitalini utaenda tu kunywa kikombe.

    ReplyDelete
  17. mhhhhh sisemi...........yangu macho

    ReplyDelete
  18. Michuzi umefanyaje mbona siwezi kukopi huyo anon wed mar 30 01:08:00 PM 2011 ili nimjibu kuwa hayo mawazo ni ya ovyo sana (ama unaogopa watu wanao-copy na ku-paste? - Hata ikikosewa wao wamo tu!). Ulaya wanatumia miti hiyo hiyo bali wanaongeza Value / ama wanapaki vizuri wakirudi be mara 2000. Wewe kama unauwezo wa kusoma blog hii basi sikutegemea mawazo kama hayo. Nimekusamehe najua ni ulimi/keyboard/kalamu imeteleza

    Observer

    ReplyDelete
  19. huyo dada ni muongo jamani msidanganyike.

    ReplyDelete
  20. Babu wa LOLIONDO kikombe chake cha BATI
    Yule DOGO wa MBEYA kikombe chake cha PLASTIKI
    Huyu SHANGAZI wa TABORA kikombe chake cha UDONGO
    Huyo mpya atakaeoteshwa inabidi ajiandae na aongeze ufundi ili akubalike vinginevyo kazi itakuwa kubwa.

    ReplyDelete
  21. The bush us still in the African. whether you like it or not

    ReplyDelete
  22. jamani mimi niko kasulu, leo kuna jamaa hapa kaanza kutoa dawa, tayari kachemsha mapipa mawili ya dawa na anangojea wateja. nikiweza ntaleta picha baadae, ngoja nisubiri mvua iishe maana tope kibao hapa mjini kasulu kama kawaida, ntaenda mtaani then ntaleta habari zaidi. naona vikombe itakuwa kila mkoa sasa, hakuna mwisho tutakuwa na regional hospital za kikombe kila mkoa. subirini wa kusini ya tanzania, kule kwa ndugu zangu wangoni waku...

    ReplyDelete
  23. Watanzania amkeni..Mie naomba kuuliza how many people have been cured so far na kuna proof yoyote..you people need to realize that we are living in a civilized world..!!

    ReplyDelete
  24. SWALI KWA JAMII SASA KAMA NIKIOTA NIMEBAKWA ITAKUWAJE???

    ReplyDelete
  25. HATUNA ASKARI HAPA

    ReplyDelete
  26. Hapa hatuna viongozi wala polisi.

    Mpaka sasa hivi JW ndo wenye akili serikalini.

    Nimekubali kwa nini wanajeshi ndo viongozi wa kweli.

    ReplyDelete
  27. Ni kweli mdau hapo juu uyasemayo,kama kweli wameoteshwa si watoe bure bila hiyo mia tano?maana hiyo mia tano ni nyingi kwa watu wa vijijini,kwani mwenyezi Mungu ni wa kila mmoja sio Athmani hapendelei huyu afaidike na kikombe kwa mia tano tano na huyu akose
    Pia wewe mdau unaesema Ulaya ndo wakuletee hii dawa kwani hayo madawa wanayokupa yanatoka wapi si huko huko kwenye miti alikotia mwenyezi Mungu Baraka zake!Inaonyesha unaabudu sana wazungu na pia mdharau kwao mtumwa ndugu yangu,acha hizo!na wao wenyewe ndo walitutengenezea hivyo virusi vya ukimwi na sasa wanashindwa kuutibu,!sina maana kuwa naitetea Dawa ya Kikombe ila kweli kumuomba Mungu sana isije kuleta madhara baadae!Na kama kweli kuna waliopona basi
    Mwenyezi Mungu azidishe Baraka zake iwaponyeshe na wengine walioinywa isije kuwa na madhara hapo baadae maana nasiki huwo mtu kuna sehemu zake ni sumu,Mwenyezi Mungu atunusuru watanzania wote 'Amen',,,Ni Ahlam UK

    ReplyDelete
  28. Hii inaonesha wazi kuwa watanzania wameadhirika kielimu yaani huwezi hata kuamini mawaziri wazima kweli wanazweza kufunga safari kwenda kunywa maji ya matakataka ? hii haikubaliki kabisa labda tuseme vyeti vyao si sahihi kabisa hawa mawaziri wetu, mimi nazani mkombozi sahihi wa watanzania ni CHADEMA.

    ReplyDelete
  29. PhatlorenzoMarch 30, 2011

    Kinachoniudhi zaidi ya kusikitisha ni dhana ya kuiga tuliyonayo. Tunafanya "copy and paste" in almost kila kitu. Kwa mafano Mtu anaweka cherehani hapo mbele ya nyumba, jirani yake naye kesho ananunua cherehani, mtu anafungua duka, kesho na mwingine anaanzisha duka similar anauza bidhaa zile zile, kwa bei ile ile. Sasa kuna hii, babu wa Loliondo na vikombe vya shilingi 500 na wengine wanaiga hivyo hivyo, kama huyu wa Mbeya. Kwa nini watanzania hatufikirii na tunakurupuka tu? Kwa nini usifikirie tofauti zaidi ili ukaja na mpango, ama mkakati mzuri zaidi wa biashara badala ya ku foto kopi kazi za wengine? People needs to be creative....wakati mwingine, sio vibaya kusoma kwanza biashara ya mwingine na kuangalia ni vitu vipi vya kuboresha vitakavyo ongeza thamani kwa mteja. Imebidi niliongelee hili..sio kwa lengo la kutibua imani za watu, la hasha ila ni kuongelea zaidi tabia ya kuiga biashara na concepts za wengine.

    ReplyDelete
  30. Tanzania kweli ni noma. Nimeamini kuwa tusicheze na system jamani, kuna watu wamesomea kugeuza mijadala ya kitaifa haki ya nani. Sasa hivi hakuna DOWANS wala mikutano ya nanii, ni masuala ya Kikombe tu. Watanzania wakija shituka kumekuchwa 2015!!. Nilikuwepo, Michuzi usibanie hii kitu

    ReplyDelete
  31. JAMANI WATANZANIA TUNAELEKEA WAPI MAANA TANAACHA KUJADILI MAMBO YA MAANA YA KUJENGA NCHI TUNAJIKITA KWANYE VIKOMBE NA KIKWETE YUPO NA SERIKALI YAKE WAMETULIA KWANI HAMNA MTU ANEYEONGELEA UPUUZI WANAOUFANYA WA KUARIBU NCHI YETU NA KUPONDA MALI. HAO WATU WOTE SINA UHAKIKA KAMA WANATIBU ILA NI HALI MBAYA YA MAISHA NDO IMECHANGIA WATU KUWA HIVYO. SASA KAMA WATU WOTE HAO WAKO KWENYE FOLENI YA VIKOMBE NANI ANAFANYA KAZI ZA KUJENGA NCHI? MAANA WATU HATA HOSPITALI WANAENDAGA KWA MPANGILIO SIO WOTE WANAKWENDA MARA MOJA KUSUBIRI. SASA KAMA WATU WAZIMA WANAGAWA VIKOMBE BADALA YA KUANGALIA MAMBO MUHIMU KAMA EMEME, MAJI, ELIMU n.k WATOTO WATAJIFUNZA NINI WALIOKO MASHULENI SI NA WAO WATAACHA KUSOMA NA KUJADILI VIKOMBE KWANI HATA WALIMU NAAMINI WATAKUWA KWENYE FOLENI.
    INAUMA SANAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA KIKWETE NA SERIKALI YAKO ACHIA NGAZI KWANI HAMNA MAANA KABISA NYIE NI ZIROOOOOO.

    ReplyDelete
  32. Oooh poor Tanzania,Jamani wenzangu haya ya kweli? Hakuna atakayeweza kujibu ndiyo au hapana, Na kama ni ya kweli mbona Serikali yetu kimya haija advertise business kwa nchi zingine? Na kama si kweli mbona wakubwa wa vyeo vyao wanapata kikombe? We should think twice before we take anything to our mouth, Unajua mimi naona watu wangefanya checkup kabla ya kunywa kikombe ili statistics ziwepo za waliopona na ushahidi wa vyeti vya daktari tena itapunguza foleni kwamba watakaoenda wameshakuwa na uhakika kuwa wanaumwa but hii ya kufuata mkumbo ndo inafanya wengi kusema wameoteshwa wakitaraji kupata pesa. Ooh my love God help us, reveal our eyes so that we can see beyond. Mi naogopa sana mwisho wa watu wanaosema Mungu amesema au ameniotesha kumbe si Mungu ni wao wenyewe, hasira ya Mungu ikishuka itafanya hata nchi iharibiwe. Ndoto zipo sikatai ila kuna aina nyingi za ndoto, kuna zile ndoto ambazo ulipolala ulikuwa unawaza kitu fulani then ukakiota hicho, au kuna ndoto zinazokuja kutoka kwa shetani na pia za Mungu si kila mtu anaweza kupima ndoto wengi wanaangalia costs kabla. Pia Wachungaji wazuri watz mpo? Je wizara inayohusika ipo? na JK upo?

    ReplyDelete
  33. Anoy wed 30,03:56:00

    Usijali akitokea mganga mpya atatumia KIFUU CHA NAZI.

    Isipokuwa nahisi kama vijindoto vinakujakuja lakini yangu inataka nifungue kibanda cha juice na ndoto yangu imelenga ktk JUICE YA CARROT ili iwape nuru au mwangaza watu.Nitajua leo usiku nikilala itakuwaje.

    ReplyDelete
  34. hizi ni siku za mwisho jamani, tunatakiwa kuwa makini sababu tutayumbishwa yumbishwa,shika sana kile ulicho nacho mtuyeyote asije akakunyang'anya...sali sana na soma neno la Mungu utapata ufunuo juu ya hayo yote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...