Marehemu Col. Wariael Barnabas Pallangyo

Familia yaBarnabas Pallangyo na familia ia Leonard Kajala Sengo wanasikitika kutangaza kifo kwa majonzi makubwa kwa mpendwa wao Col. Wariael Barnabas Pallangyo (ltd) kilichotokea ghafla tarehe 28/03/2011 Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

Col Pallangyo amewahi kushika nafasi nyingi za uongozi za jeshi,akiwa kamanda wa vikosi vingi, task force training officer Uganda na sehemu nyeti za Jeshi

Marehemu ataangwa leo tar 30/03/2011 saa 4 asubuhi nyumbani kwake Tangi bovu mbezi beach baadae saa saba mchana kutakuwa na ibada na kutoa heshima za mwisho kwenye kanisa la Lutheran Mbezi beach.

Saa 9 mchana itaanza safari ya kuelekea Meru, Arusha, kwa mazishi yatakayofanyika tarehe 31/03/2011 saa 9 mchana.

Bwana ametoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana na lihimidiwe.

Tunakuomba Bwana uiweke roho ya kipenzi chetu mahala pema peponi - AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mungu Mwenyezi akuweke mahali pema peponi Col Pallangyo.
    Ulikuwa mtu mpole na myenyekevu kwa wote licha ya cheo chako kikubwa na kazi yako nyeti jeshini.
    Ulikuwa mcha Mungu sana na tutakukumbuka sisi uliotuacha nyuma kwa unyenyekevu wako.
    Mungu alitoa na Mungu ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe.
    Na ulale salama Col Pallangyo

    ReplyDelete
  2. Dady tutakukumbuka kwa ucheshi wako, pengo ulilotuachia kamwe halitazibika, tunajua ya kuwa kimwili hatuko nawe ila kiroho tuko nawe. TULIKUPENDA SANA LAKINI MUNGU KAKUPENDA ZAIDI. TUNAKUKUMBUKWA SANA. MWENYEZ MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI, Upumzike kwa Aman. AMEN.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...