Ndugu Michuzi,napenda kuchukua fursa hii kukusalimu wewe na timu yako nzima hapo nyumbani.Kwa niaba ya kanisa la Umoja International Outreach lenye makao yake katika jiji hili la Dallas Texas;napenda kuwajulisha watu wote kutoka Afrika ya Mashariki na sehemu zingine kuwa tutakuwa na ibada maalumu siku ya Jumapili tarehe 3.04.2011.
Ibada hii itaongozwa na Mchungaji DEO LUBALA (pichani) ambae ni kiongozi mkuu wa kanisa la World Alive lenye makao yake makuu hapo nyumbani Tanzania.Tunaomba kwa wale watu ambao hawaishi hapa Dallas lakini wana ndugu, jamaa na marafiki katika jiji hili wawahimize kuhudhuria katika ibada.Hii itakuwa mara ya pili kupata kibali cha kuwa na huyu mtumishi wa Mungu ambae amekuwa akimtumikia Mungu sehemu mbali mbali duniani.
ANUANI;
UMOJA INTERNATIONA OUTREACH CHURCH
6411 LBJ FREEWAY DALLAS TEXAS,75240
MUDA NI SAA KUMI NA MOJA NA NUSU MPAKA SAA MBILI USIKU (5:30PM-8:00PM)
MAWASILIANO:214 554 7381,682 552 6402,214 773 6697



Vikombe vitatolewa? kama hakuna vikombe basi mimi sipotezi muda wangu.
ReplyDeleteHongera sana Deo kwa hatua uliyofikia kimaisha hasa katika kueneza NENO LA MUNGU.
ReplyDeleteNaamini huyo uliyenae kwenye picha ndiye my wife wako, hongera zake nyingi kwa kukutunza na kukufanya umeremete.
Unasalimiwa sana na wale wote tuliokuwa nao DSA na JKT Ruvu.
Massoud
wow that is truly man of God,
ReplyDeleteGod bless you and may He continue using you mightily!
Mrs Kulaba.