Miezi hii ndio mizuri kuweza kuuona Mlima Kilimanjaro kwani mawingu huwa hamna hasa nyakati za asubuhi na ukiwa mji wa Moshi mambo yanakuwa kama unavyoona

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Naam ni muda muafaka na mlima waonekana vizuri sana ! Ila hoja yangu niielekeze kwenye huo usafi na umaridadi wa mji wa Moshi ! embu ona hiyo keep left(round about)Garden yake ipo safi ! and well maintaned,angalia kituo cha basi ! ukilinganisha na hapa kwetu Dsm ni maajabu sana vituo vya mabasi vimegeuka majalala ! open space majalala ! kwenye island za mabarabara majalala ! mitaro majalala ! mito midogo majalala ! na hata ukipita kwenye hizo ofisi za serikali za mitaa ni majalala ! Jamani mlioshika zamana ya kusimamia haya mambo mpooooooo ? au ndio mwarudisha kwanza gharama za uchaguzi ? Tuige na tujifunze toka kwa wenzetu wa moshi mbona kwao yawezekana ! kuna kipindi fulani kulizuka harambee ya usafi wilaya ya kinondoni na hata Radio Clouds walikuwa wadau kwa hili lkn waweza sema Kinondoni ndio twaongoza kwa uchafu ! Wakuu wote wa kusimamia haya masuala simamieni jamani ! waelimisheni wana wa nchi juu ya usafi !.

    MZUSHI

    ReplyDelete
  2. ...aah mndenyii!

    ReplyDelete
  3. Napita hapo kesho asubuhi na BA nikitokea kwa queen hopeful nami ntauona vizuri.asnte kwa PICHA nzuri kaka MICHUZI.

    ReplyDelete
  4. Hiyo Bustani inatuzwa na Bonite Bottlers kiwanda cha soda cha Mh. R.Mengi

    ReplyDelete
  5. asante kwa kutuwekea mambo matamu na mazuri ya nchini mwetu kaka michu!! kweli mji wa moshi+muonekano wa mlima kilimanjaro vinaleta mvuto wa hali ya juu. napenda kushauri wadau wa maeneo ya jirani au wanaoweza kuwa ktk safari maeneo ya karibu na moshi wajaribu kuwa wanafanya ata day trips to the first point (mandara)- Maundi crater ambapo ni kivutio cha awali na kuona kibo peak kwa ukaribu fulani ukiwa katika natural environment breathing very fresh air that comes around mount Kilimanjaro. Kwa wale watakaopenda kufanya day trip ni rahisi sana kwa mtz wa kawaida coz park fee ni tsh elfu moja mia tano per person per day then ukipata guide mkaelewana vizuri ni kati ya tsh elfu 15 na elfu 20, utakachojiongezea hapo ni kubeba tu maji ya kunywa ya kutosha na ka-lunch box thereafter you are just enjoying the beauty of nature. mapumziko yanaweza kuwa kufanya this kind of day hiking na ukafurahia kuwepo Tz.

    Ni hayo tu kaka michu naamini wazalendo watafurahia zaidi kuwepo Tz.

    ReplyDelete
  6. ruwa oko mangi!!!! nyumbani kuzuri.leka tupu.

    ReplyDelete
  7. ndo maana nakupenda michuzi huwa unawarusha watu roho sana kwani kwa kuwaonyesha uchagani roho zinawauma sana lakini ndo hivyo wenzetu wachaga washapiga hatua wako mbele cheki mazingira mwenyewe.

    ReplyDelete
  8. Proud to be mangi sana tu...Kwetu kwetu nani anabisha? Halafu ukienda kule mndenyi kila mtu amefagia nje kwake. Huoni hata vumbi...Kuondoa vimbi tulikua tunamwagia maji kila siku jioni na ile hewa tena saaafiiiii...Kweli wachaga tuwasafi sana tu. Angalia hata manurse wa KCMC walivyo wasafi......Jibu tosha sio lazima msimamiwe kufanya usafi. Anza na wewe peke yako..Usitupe taka mahali pasipo takiwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...