Mwana Libeneke mkuu wa Iringa Francis Godwin akiwa kazini na Ankal kwenye michezo ya wana habari ya kugombea kombe la NSSF katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe, Dar

Nategemea kuondoka jijini Dar es Salaam asubuhi hii kurejea mkoani kwangu Iringa.

Rai yangu kwa wamiliki wa Blogu wote kuheshimu kazi za wengine hata kama kuna tukio umelipenda kutoka katika blogu nyingine ni vema kutaja chanzo cha habari husika ama Blogu iliyochapisha tukio/habari husika.

Binafsi sijapendezwa hata kidogo na Blogu ya kashavudodo kwani mmiliki wa blogu hii kazi yake ni kukopi kila kitu na kuweka katika blogu yake kama kazi hiyo ameifanya yeye nasema huo ni wizi na nina uwezo wa kuchukua hatua kwa kazi zangu.

Naomba Kashavudodo na wengine wenye tabia kama hii kuiga mfano kwa wakongwe wa Blogu ambao wakipenda tukio kutoka blogu nyingine lazima chini wataje chanzo cha habari husika.

Napenda kuwaomba radhi wadau wa blogu yangu ya www.francisgodwin.blogspot.com kwa usumbufu uliojitokeza hadi baadhi yenu kuniuliza kama blogu ya kashavudodo inamilikiwa na nani na ina mahusiano na blogu yangu.

Nasema hivi, blogu hiyo haina mahusinano hata chembe moja na blogu yangu ila imekuwa ikifanya ufisadi wa kazi za blogu yangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. POLE UMESEMA UKWELI KUHUSU HILO. WANABLOG WAHESHIMU KAZI ZA WENZAO NA WANAPOTUMIA KAZI ZA WENGINE BASI WATOE TAARIFA KUWA WAMEPATA WAPI KAZI HIYO

    ReplyDelete
  2. Mambo ya blogging nadhani Watanzania tumeyavamia bila kujua hasa mantiki yake (huu ni mjadala mrefu sana). Michuzi, wakati unawasilisha mjadala wa teknohama (hasa blogging) kule Ukerewe, ulisema Tanzania kuna blogs kama 200-300? (Sina uhakika.) Sasa, zote hizo zina kazi gani? Au MALENGO gani?

    Bahati mbaya tuna blogs chache sana ambazo ni za kipekee; wanapost mambo tofauti kabisa na wengine, wana malengo tofauti, na hata hadhira yao ni tofauti.

    Kitu ambacho tunaona sasa hivi ni watu "kugelezea" kila kitu kutoka kwenye blogs nyingine. Matokeo yake unakuta posts 10 hizo hizo kwenye blogs 10-20! Sasa, unabaki kujiuliza, kunani pale? Matukio ni yale yale, picha ni zile zile, matangazo ni yale yale, n.k.

    Ni sawa watu wote kutuhabarisha habari nzito (kama ile ya Gongo la Mboto) kwa mpigo, lakini hii ya ku-copy & paste kila kitu - bila hata kuweka chanzo - inaudhi. Wengine wananakili mpaka makosa...

    Kwa mfano, huyo 'kashavudodo' kagelezea hadi matangazo!

    ReplyDelete
  3. Daaaaah.....Kweli nimeona na mimi nichangie japo kiasi hapa kweli Kashavu dodo amekosea sana sana yani kacut paste mfumo kama wa Ankal inasikitisha sana.....ni vizuri sana kuweka Chanzo cha Habari maana bila kufanya hivyo ni Wizi.....kuhusu kuweka habari zinazo fanana katika blogs mimi naona wakati mwingine ni sawa maana si wote wanajua blog fulan ndo mana utakuta habari zinaendana...ni sawa na magazeti mbona yote yanaandika habari sawa kwa asilimia kubwa lakini mtu huchagua lile gazeti alipendalo....mimi naona blogs ni kama Gazeti lenye mfumo tofauti.......Naomba jamaa ajilekebishe kwa kweli....wanablog kwa kweli mimi nimesikitika sana pia.....Pole kaka Francis Mzee wa Matukio Daima.....

    ReplyDelete
  4. Jamani kucopy ndio ni muhimu kuandika ulikotoa habari hiyo hata kaka yetu hapa kuna vitu anapost lakini haandiki copyright ni ya nani....Lakiniuna mpenalty? No...Ni pole pole kuelezana na kufundishana watu waelewe umuhimu wa copyright lakini hiyo ya mdau hapo juu anayesema at kwanini TZ kuna blog nyingi? that is nonsense. Mablog ni mengi lakini ndio hapo unatakiwa kutofautisha a boy from a man....Hata huku kuna mablog mengi lakini very few are standing out na habari ikitoka kila mtu anaiweka na wengine wanacopy the same thing na kuandika tena lakini ujue kila mwenye blog anawasomaji wake. sasa mwandishi wa blog akiona kuna kitu kinamvutia au kitaingiza traffic kwenye blog yake yupo free kupost..sasa wewe kama unasubscribe kwa mablog kibao ndio ujiulize why you are doing that...Na ujue mablogger wanataka kupata wasomaji wengi sasa kama wewe unaona blog fulani huipendi au haiworth your time usiisome lakini sio ukatishe watu tamaa ya kublog...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...