Abiria wa basi la kukodi kutoka wilayani Nzega, wakisukuma gari lao lililokwama katika mpaka wa mbuga ya wanyama ya Serengeti na Loliondo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jumatano , walipokuwa wakielekea kijiji cha Samunge, mkoani Arusha kwa ajili ya kunjwa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

Na Waandishi Wa MWANANCHI

KIKAO cha kutafuta njia bora ya kuwawezesha wananchi kupata tiba ya magonjwa sugu huko Loliondo kilichoongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na viongozi wa mikoa sita wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Isdore Shirima na mwenzake wa Mara, Enos Mfuru kimeahirishwa katika kile kinachoaminika kuwa ni hadi pale maazimio yake yatakapopata baraka za Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

Lukuvi aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya kuahirisha kikao hicho saa 3:35 usiku kuwa bado kuna mambo ya kujadiliwa kabla ya kutoa tamko rasmi.“Kikao kimeahirishwa tumepeana majukumu, kesho Mkuu wa Mkoa wa Arusha atakuwa Loliondo kuongea na Mchungaji Ambilikile Mwasapile na kujionea hali ilivyo kwa sasa na wengine wamepewa majukumu mengine, hivyo kesho (leo) tutakuwa na la kuwaambia baada ya RC kurudi," alisema. Kwa habari kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Dah inaniumiza sana kuona ni jinsi gani serikali inavyohandle this situation kipumbavu namna hii,mpaka dakika hii hakujafanywa utafiti wowote wa kuthibitisha ubora na uhakika wa hayo matibabu,then munakurupuka kutengenezea watu access ya kuifikia hiyo dawa,incase kama yatatokea madhara nani atakayebeba hili jukumu?wizara ya Afya ipo wapi itoe tamko la maana.
    Ni lini viongozi wetu watakuwa creative wa kuweza kusolve such a simple situations,munashindwa kweli kuorganize waliokunywa dawa muwapime ili kujua ukweli wa matibabu,ni wagonjwa wangapi wanaokufa kwenye hiyo foleni simply kwa sababu hakuna mtu wa kuwaongoza kwenye huu uozo?
    Media zote za East Africa zinatucheka kuwa watanzania bado ni wale wale wa "majimaji war",hawajaelimika,na mimi pia nawasupport.
    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  2. waziri alishatoa tamko siku nyingi tuu zilizopita na akaaitwa mdini. Na mkuu wa mkoa wa huko, bwana Shirima alikataa katakata kusikiliza kauli ya waziri wa afya na akasema kwamba yeye hawajibiki kwa waziri wa afya. Endeleeni kwenda loliondo tuu kwa babu na wote mtapona.

    ReplyDelete
  3. huyo mchangiaji wa kwanza ujifunze kutumia lugha nzuri. Na sio kwakuwa uko utumwani instanbul ndo unaropoka tu. Hatujajua wakubwa hao wanazungumzia nn so ngumu ku-judge.

    Hii ni nchi yetu, twaitumia tutakavyo. Hatujali wengine wanasemaje ilimradi twaishi kwa amani bila kuuana. Watasema sana.

    Kuhusu loliondo naonelea kuna haja ya nchi kuthibiti wanaoingia toka nchi za nje kupata dawa. Wanapaa anga letu bila ruhusu na kutua loliondo. Hilo mie nimelishuhudia kwa macho. Ni wakati sasa wa serikali kupata mapato ya flyzone zetu sio watu wanapaa nchini wanavyotaka.

    Na hata wanaoingia kwa mguu. Napata picha hii dawa ingekuwa uganda au kenya tungeingia kwa shida na serikali zao zingetumia nafasi hizo kupata kipato.

    Naomba serikali ilifanyie kazi sualaa hilo.

    ReplyDelete
  4. ChakubangaMarch 26, 2011

    I dont understand how comes the minister of health who is constitutionally is dealing with all healthy matter issued a warning to stop people using that medicine until farther test, then another minister Mr. Lukuvi whom I dont even know what exactly his ministry is responsible with issued another statement over running and undermining previous statement.

    The worst is now the government is allowing this old man to held them ransom, what a shame !

    ReplyDelete
  5. Hivi waziri wa afya bado ni Prof mwakyusa? Hii kali saana, hata yeye imemshinda!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...