Babu wa Loliondo

Babu Ambi wa Loliondo akawaambia wagonjwa kuwa wakae kwenye mistari tofauti kulingana na maradhi yanayowasumbua....

Yaani wenye sukari huku, wenye BP kule, wenye nyonga huku na wale wenye ukimwi mstari wao na wale wenye nyonga sugu pia mstari wao.

Watu wote wakajaa kwenye mstari wa wagonjwa wa kisukari na BP.

Mstari wa ukimwi ukabaki tupu....

Babu kuona wote ni wa kisukari na BP akasema.."Ah, haya basi ngoja hii dawa ya ukimwi niimwage".... (akawa anajiandaa kuimwaga..)

watu wote mistarini wakapiga ukelele mkubwa."aaah babu usiimwage.... usimwageeee.... tumejichanganya tu babu...! usiimwage......!!!!!"

NA BABU AKATAHAYARI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. hii habari, iwe ya kweli ama ya uwongo si nzuri. inanyanyapaa watu wenye ukimwi na bw. michuzi kama una-control vinavyopostiwa humu tafadhali usikubali habari kama hizi.

    ReplyDelete
  2. Hii kali kuliko zote. Kumbe dawa ina grade tofauti. Wenye ukimwi wanataka ya kisukari mbona mambo yatakuwa balaa.

    ReplyDelete
  3. KUDADADEKI HILI NENO LA LEO NI KIBOKO
    MDAU

    ReplyDelete
  4. Mimi nafurahi kwa wazo hilo. Ingetokea babu agrade watu kwa magonjwa, nadhani wale wenye magonjwa ya aibu wasingeenda. Na si hayo tu kuna wengine wanatafuta kutolewa mikosi sababu wamejaribu kwa waganga wengine wameshindwa hivyo hii haipo kwenye ajenda ya babu lakini watu wanaweza kuamini kuwa dawa yake ni kiboko ya kila kitu. je vikojozi watapenda wajipange kwenye msitari wakwao? Ndo maana kwa madaktari milango inafungwa ili watu wasisikie shida za wenzao.

    ReplyDelete
  5. utani mzuri.

    halafu we unayesema unyanyapaa, kwanini watu wa ukimwi wanataka attention kubwa wakati wakiambiwa kondomu waligoma?

    ReplyDelete
  6. hahahha, ni kichekesho tuu mbona hapo juu umewaka ghafla una ukimwi nini?

    ReplyDelete
  7. Babu atasingiziwa mengi mwaka huu.... lol

    ReplyDelete
  8. Yaani nimecheka sana... Weee acha kuchekesha watu kumbe hizo dawa ziko tofauti....ahhh Tanzania kuwa na ukimwi kumbe bado tabooo...He wenenuwajitangaza ukikutana na mtu yuko happy happpy. aNakwambi mimi HIV positive...15 years now. Lakini wanasema ukweli ...I don't wish this to anyone..It is hard to deal with it....Lakini sio jambo la kujificha tena...

    ReplyDelete
  9. Mi siamini habari hii, kwanini babu awatenge watu kimagrupu kama dawa ni ya mti mmoja??? Huyu aliyeweka hii habari anataka kutuchekesha tu wasomaji wako kaka Michu na nimecheka sana kwakweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...