Babu Ambi wa Loliondo akawaambia wagonjwa kuwa wakae kwenye mistari tofauti kulingana na maradhi yanayowasumbua....
Yaani wenye sukari huku, wenye BP kule, wenye nyonga huku na wale wenye ukimwi mstari wao na wale wenye nyonga sugu pia mstari wao.
Watu wote wakajaa kwenye mstari wa wagonjwa wa kisukari na BP.
Mstari wa ukimwi ukabaki tupu....
Babu kuona wote ni wa kisukari na BP akasema.."Ah, haya basi ngoja hii dawa ya ukimwi niimwage".... (akawa anajiandaa kuimwaga..)
watu wote mistarini wakapiga ukelele mkubwa."aaah babu usiimwage.... usimwageeee.... tumejichanganya tu babu...! usiimwage......!!!!!"
NA BABU AKATAHAYARI
hii habari, iwe ya kweli ama ya uwongo si nzuri. inanyanyapaa watu wenye ukimwi na bw. michuzi kama una-control vinavyopostiwa humu tafadhali usikubali habari kama hizi.
ReplyDeleteHii kali kuliko zote. Kumbe dawa ina grade tofauti. Wenye ukimwi wanataka ya kisukari mbona mambo yatakuwa balaa.
ReplyDeleteKUDADADEKI HILI NENO LA LEO NI KIBOKO
ReplyDeleteMDAU
Mimi nafurahi kwa wazo hilo. Ingetokea babu agrade watu kwa magonjwa, nadhani wale wenye magonjwa ya aibu wasingeenda. Na si hayo tu kuna wengine wanatafuta kutolewa mikosi sababu wamejaribu kwa waganga wengine wameshindwa hivyo hii haipo kwenye ajenda ya babu lakini watu wanaweza kuamini kuwa dawa yake ni kiboko ya kila kitu. je vikojozi watapenda wajipange kwenye msitari wakwao? Ndo maana kwa madaktari milango inafungwa ili watu wasisikie shida za wenzao.
ReplyDeleteutani mzuri.
ReplyDeletehalafu we unayesema unyanyapaa, kwanini watu wa ukimwi wanataka attention kubwa wakati wakiambiwa kondomu waligoma?
hahahha, ni kichekesho tuu mbona hapo juu umewaka ghafla una ukimwi nini?
ReplyDeleteBabu atasingiziwa mengi mwaka huu.... lol
ReplyDeleteYaani nimecheka sana... Weee acha kuchekesha watu kumbe hizo dawa ziko tofauti....ahhh Tanzania kuwa na ukimwi kumbe bado tabooo...He wenenuwajitangaza ukikutana na mtu yuko happy happpy. aNakwambi mimi HIV positive...15 years now. Lakini wanasema ukweli ...I don't wish this to anyone..It is hard to deal with it....Lakini sio jambo la kujificha tena...
ReplyDeleteMi siamini habari hii, kwanini babu awatenge watu kimagrupu kama dawa ni ya mti mmoja??? Huyu aliyeweka hii habari anataka kutuchekesha tu wasomaji wako kaka Michu na nimecheka sana kwakweli.
ReplyDelete