Waziri mkuu,Mizengo Pinda afanya ziara ya siku moja katika kiwanda cha Sukari TPC Ltd mkoani Kilimanjaro huko Moshi na kuona shughuli za uzalishaji sanjari na kutembelea mashamba ya kiwanda hicho ambapo aliridhishwa na juhudi za wawekezaji hao.
Waziri mkuu,Mizengo Pinda akikagua uzalishaji
katika kiwanda cha Sukari TPC Ltd MoshiMwenyekiti wa bodi ya kiwanda cha sukari cha TPC,Arnaud Dalais,akikabidhi msaada
wa sukari kwa ajili ya waathirika wa mabomu yaliyotokea Gongo la Mboto,kwa waziri mkuu,Mizengo Pinda aliyekuwa katika ziara ya siku mbili mkoani Kilimanjaro ambapo alitembelea kiwanda hicho na hospitali ya rufaa ya KCMC.
Habari na picha na mdau Na Dixon Busagaga.


UONGOZI wa kiwanda cha Sukari cha TPC Ltd cha wilayani Moshi mkoani
Kilimanjaro umetoa msaada wa tani 10 za sukari kwa wathirika wa mabomu
wa Gongolamboto jijini Dar es salaam yaliyotokea mapema mwaka huu.

Mwenyekiti wa bodi ya kiwanda hicho,Arnaud Dalais,alikabidhi msaada
huo jana kwa waziri mkuu,Mizengo Pinda aliyekuwa katika ziara ya siku
mbili mkoani Kilimanjaro ambapo alitembelea kiwanda hicho na hospitali
ya rufaa ya KCMC.

Tukio la milipuko ya mabomu katika ghala kuu la Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililoko Gongolamboto lilitokea Februari
17 ambapo mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu 30 na 135 kujeruhiwa
huku maghala 23 kuteketea kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...