

Rais wa chama cha waandishi wa habari za michezo duniani (AIPS Gianni) Merlo ametaka nchi wanachama wa chama hicho ikiwemo TANZANIA kuvishawishi vyama vya soka na kamati za Olimpiki ili zisaidie vyama hivyo.
Merlo amesema vyama hivyo ni wadau wakubwa wa waandishi wa habari za michezo hivyo havina budi kusaidia vyama vya waandishi wa habari za michezo katika masuala mbali mbali.
Amesema shirikisho la kandanda la dunia FIFA imeahidi kuiongezea AIPS msaada iliyokuwa kwa asilimia 50 zaidi.
Rais huyo ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa AIPS unaofanyika mjini Seoul, Korea ya Kusini ambapo Tanzania kupitia chama chake cha waandishi wa habari za Michezo nchini TASWA inawakilishwa na Makamu Mwenyekiti wake Maulid Kitenge na katibu Msaidizi George John.
Kwa upande wake, TASWA kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Maulid Kitenge, imesema itazungumza na TFF na Kamati ya Olimpiki nchini Tanzania TOC ili kuona inasaidia chama chake katika masuala mbali mbali mbali ikiwemo fedha za kuendesha mafunzo mbali mbali kwa waandishi wa habari za Michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...