CHAMA cha Waandishi wa habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJAtz) na Mtandao wa wa Wasanii Tanzania (Arterial Network Tanzania) Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya wasanii 13 wa kundi la muziki wa taarabu la Five Star vilivyotokana na ya ajali mbaya ya gari iliyotokea Usiku wa tarehe 21/02/2011 katika barabara kuu ya Iringa-Morogoro kwenye eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Mikumi.

Arterial Network Tanzania na CAJAtz tukiwa wadau wa masuala ya sanaa hapa nchini, tunatoa salam za rambirambi kwa familia za wafiwa, Wizara ya Habari Utamaduni, vijana na Michezo, Baraza la Sanaa na Taifa (BASATA) na wadau wote wa sanaa hapa nchini kutokana na msiba huo mkubwa na wa aina yake kupata kutokea katika medani ya sanaa hapa nchini.

Tunaamini kwamba taifa na sekta ya sanaa ya Tanzania imepata pigo kubwa sana kutokana na msiba huo na kwamba vifo vya wasanii hao vimeacha pengo kubwa ambao haikuwa rahisi kuzibika katika medani ya muziki.

Vilevile tunawapa pole majeruhi katika ajali hii na kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili hatimaye waweze kurudi katika hali yao ya awali na kushiriki shughuli za sanaa.

Hassan Bumbuli

KATIBU MKUU

CAJAtz na ARTERIAL NETWORK TANZANIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...