MAREHEMU SHELA SHOMARI MGOWA
(Mama Rahma Mshana au Mwalimu Shela)

Kwa niaba ya Familia ya MR.Shomari Rashidi Mgowa(OCD Simanjiro-Manyara) na MRS Halima Shomari Mgowa wa Same Hospital- Kilimanjaro, MR.Mshana wa Manispaa ya Iringa (Mume wa Marehemu). na MR&MRS Masoud Msemo wa Dar es salaam , Tunapenda kuwashukuru wale woote waliofanikisha mazishi ya Dada yetu mpendwa kwa njia moja au nyingine na wale waliopata udhuru kwani majibu yao yalidhihirisha tosha tupo pamoja katika msiba huu mzito, Uliotupata katika Familia ya Mr.Shomari Mgowa (baba wa Marehemu) na Familia ya Mr.Mshana (Mume wa marehemu).

Tunapenda pia kuwashukuru Wafanyakazi na majirani wenzake na marehemu waliotokea Iringa na Same,Wafanyakazi na majirani wenzake na mume wa marehemu waliotokea Iringa na Same, Wafanyakazi na majirani wenzake na Baba na Mama mfiwa waliotokea Simanjiro,Same,Kibaha,Arusha.

Pia tunawashukuru Ndugu woote waliofika kwenye msiba huu mzito waliotokea Arusha, Morogoro,Pwani, Same, Kilimanjaro,Dodoma, Mwanza, Tanga,Dar es salaam, USA,Italy na Sudan.Bila kumsahau Mchungaji aliyeendesha misa siku ile. Kwa wale ambao hawakuweza kupata taarifa haraka tuma email hii: mariamshomary@yahoo.com

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
Asanteni wote
Mariam Shomari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...